Nifanyeje ili nipate kitambulisho cha NIDA haraka baada ya kukipeleka kufanya marekebisho?

eskandria

Member
Mar 21, 2023
7
5
Habar zenu Wana jamvi niende moja kwa moja kwenye mada husika nmekua nikifatilia inshu ya NIDA. Toka mwaka jana hadi leo hii lkn sijafanikiwa jambo langu.

Kwenye kitambulisho changu cha NIDA kuna jina lilikosewa niliwafata nida wakanipa utaratibu jinsi ya kufanya ili warekebishe jina.

Nikafuata taratibu zote nikakamilisha toka mwaka Jana lakini hakuna mabadiliko yaliyofanyika. Mwaka Jana nilishindwa kuomba ajira kwa ajili ya NIDA mwaka huu ajira wametangaza kigezo bado ni NIDA.

Wanajamvi naombeni mbinu nifanyeje ili niweze kurekebishiwa nida ili na mimi nijumuike kwenye mchakato wa kutafuta hizo ajira. Naombeni msaada wa fikra maana penye watu wengi tunaweza kupata suluhu.

Asanteni
 
Kwanza Fanya maombi na nida yako usikose kuomba then ukipata hiyo Ajira ukaambiwa ukaripoti ndo uende na vielelezo vyako.
 
Back
Top Bottom