Msaada: Nataka kubadili jina kisheria (NIDA)

Full charge

JF-Expert Member
Mar 1, 2018
1,550
1,422
Habari za muda huu wakuu,

Mimi ni Mkristo, nimeamua kubadili dini kuwa muislam kwa hiari yangu kabisa bila msukumo wowote.

Nimebadili jina langu la awali hivyo ningependa kubadili pia katika nyaraka zangu za kiserikali ikiwemo kitambulisho cha taifa (NIDA).

Je, ni utaratibu gani nifuate ili kuweza kubadili jina langu la awali na kupachika jina jipya ambalo litatambulika kisheria mpaka kwenye NIDA? Msaada wenu jamani naomba mnipe mbinu
 
kwa utaratibu uliokuwepo muda kidogo, kwanza andaa deedpoll kisha nenda ukaisajili kwa ofisi ya msasjili wa ardhi mkoa, kisha kaitangaze hiyo deedpoll yako kwenye gazeti la serikali.

Mwisho pata nakala ya gazeti la serikali, nakala ya deedpoll yako, viatambanisho vyako hasa vyenye uthibitisho wa jina unalotaka, kisha nenda ofisi ya NIDA wilaya uliyopo karbu nayo utapewa control number ya Tsh 20000/=

angalizo, kabla ya kufanya hayo jarbu kufika ofisi ya NIDA ili ueleweshwe kama una maswali zaidi au kama kuna mabadiliko ya muongozo watakupa, watu hao wako poa sana, watakupa elimu ya kutosha juu ya changamoto yako
 
kwa utaratibu uliokuwepo muda kidogo, kwanza andaa deedpoll kisha nenda ukaisajili kwa ofisi ya msasjili wa ardhi mkoa, kisha kaitangaze hiyo deedpoll yako kwenye gazeti la serikali. mwisho pata nakala ya gazeti la serikali, nakala ya deedpoll yako, viatambanisho vyako hasa vyenye uthibitisho wa jina unalotaka, kisha nenda ofisi ya NIDA wilaya uliyopo karbu nayo utapewa control number ya Tsh 20000/=
angalizo, kabla ya kufanya hayo jarbu kufika ofisi ya NIDA ili ueleweshwe kama una maswali zaidi au kama kuna mabadiliko ya muongozo watakupa, watu hao wako poa sana, watakupa elimu ya kutosha juu ya changamoto yako
Asante mkuudeedpoll ni nini?

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
kwa utaratibu uliokuwepo muda kidogo, kwanza andaa deedpoll kisha nenda ukaisajili kwa ofisi ya msasjili wa ardhi mkoa, kisha kaitangaze hiyo deedpoll yako kwenye gazeti la serikali.

Mwisho pata nakala ya gazeti la serikali, nakala ya deedpoll yako, viatambanisho vyako hasa vyenye uthibitisho wa jina unalotaka, kisha nenda ofisi ya NIDA wilaya uliyopo karbu nayo utapewa control number ya Tsh 20000/=

angalizo, kabla ya kufanya hayo jarbu kufika ofisi ya NIDA ili ueleweshwe kama una maswali zaidi au kama kuna mabadiliko ya muongozo watakupa, watu hao wako poa sana, watakupa elimu ya kutosha juu ya changamoto yako

Masuala ya ardhi ni title deed acha kumpotosha.
 
Habari za muda huu wakuu,

Mimi ni Mkristo, nimeamua kubadili dini kuwa muislam kwa hiari yangu kabisa bila msukumo wowote.

Nimebadili jina langu la awali hivyo ningependa kubadili pia katika nyaraka zangu za kiserikali ikiwemo kitambulisho cha taifa (NIDA).

Je, ni utaratibu gani nifuate ili kuweza kubadili jina langu la awali na kupachika jina jipya ambalo litatambulika kisheria mpaka kwenye NIDA? Msaada wenu jamani naomba mnipe mbinu
Huyo Sheikh aliyekubasilimisha mtumie huyohuyo kwa hayo mambo mengine
 
Masuala ya ardhi ni title deed acha kumpotosha.

usimpotoshe kama hujui kaa kimya deed utaipata wazara ya ardhi kwanza unaenda kwa wakili unamuelezea yeye ndio atakuandikia deed pol utachukua itaenda ardhi na huko ndiko utakuwa imebadilisha jina watakuambia urudi wiki mbili unaendea karatasi hiyo ya deed pol utakuwa umeisha maliza kuna malipo kidogo ardhi na wakili ni mapatano kama elfu 20 au 10
 
Dah! Umechagua njia ngumu sana ya kupita. Yaani kirahisi tu ubadili mpaka vyeti vya elimu, kitambulisho cha Taifa, nk!!!

Nadhani huo mchakato unaweza kukuchukua hata miaka 20 na usifanikiwe kuukamilisha.
 
Dini SI Imani TU. Baki na Imani hiyo mpya ila majina sidhani kama yana uhusiano wowote na dini...

Nakushauri acha majina Yako hayo hayo ila komaa kujua dini Yako hiyo mpya...!

Kwa nchi yetu utakutana na mlolongo mrefu ambao utakupotezea muda na pesa. As long as huvunji Sheria kubaki na majina Yako hayo Baki nayo.​
 
Waafrika sijui tuna shida gani , nani kakuambia kuna majina ya wakristo na waislam? Kwa taarifa yako kuna majina ya kiarabu , kifini, kijerumani, etc. Dini hazina uhusiano na majina Kabisaa ni ujinga tuliomezeshwa.
Waafrika tunahangaika sana na vitu vya ajabu ajabu alafu vya msingi tunatupa kule.

Unaweza kuta tu huyu fal amepata demu anabadilisha dini au ameshauliwa kuhusu jihad sasa anajioja mwanaharakati mkuu wa kiislam

Wabongo heshima kwenu,ujinga umetuzidi
 
Sikukatishi tamaa lakini Kwa uzoefu wangu nakuhakikishia hautafanikisha Hilo zoezi utajikuta umekwamia njiani na umetumia mda mwingi na gharama kubwa, Kuna uncle wangu ni Afisa mkubwa serikalini alioa muislamu akabadili Dini, alijaribu hicho kitu kutokana na mulolongo na mda akaamua kubakia tu na jina la kizungu
 
Waafrika sijui tuna shida gani , nani kakuambia kuna majina ya wakristo na waislam? Kwa taarifa yako kuna majina ya kiarabu , kifini, kijerumani, etc. Dini hazina uhusiano na majina Kabisaa ni ujinga tuliomezeshwa.
Dini hupumbaza sana watu mfano ndio huo unauona.

Dini zimefanya watu wajinga kua wapumbavu na mataahira kabisa.

Mungu wa kwenye biblia ama quran hayupo na dini ni utapeli kama utapeli
 
Back
Top Bottom