Nilivyofanikiwa kubadili majina yangu yaliyokosewa NIDA

Kichwa Ze Don

Senior Member
Jun 7, 2017
174
298
Habari za muda huu ndugu zangu wa jamii forum, Watu (Wananchi ) wamekuwa wakilalamika juu ya hadha (usumbufu) wakati wakifuatilia juu ya kubadili majina Yao yalikosewa NIDA .
Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ombi lako la kubadili majina linaweza kukubaliwa Au kukataliwa inategemeana Na afisa wa NIDA kujiridhisha Na document zako ulizopeleka ..

HATUA NILIZOCHUKUA KUBADILI MAJINA YANGU MAWILI YALIYOKOSEWA..
1. Hatua Ya Kwanza Kiapo cha mwanasheria Au Mahakama kinachoomba kubadili jina kutoka A Kwenda B Kwa lugha ya kingereza wanaita DeedPol , Gharama Kwa mwanasheria ni 30,000/= maana zinakuwa jumla Karatasi 3 Ila ukienda mahakamani ukilia lia wataku charge 15,000/=

2.Hatua Ya Pili kupeleka kwa msajiri Wa Ardhi hizo Karatasi tatu ulizotoka nazo kwa mwanasheria au Mahakama . Kwa wakazi wa Dar es salaam unapeleka pale Ardhi kivukoni , unatakiwa kuambatanisha Vyeti Au Vitambulisho vinavyoonyesha hayo majina yaliyotofautiana , Kipindi kile walikuwa Wana charge 32,500Tsh/= Unakata Baada Ya Wiki (Siku 7) unafuata majibu Yako.

3. Hatua ya tatu kupeleka tangazo kwa mhariri wa gazeti la serikali , Gharama yake ni Elfu 20,000Tsh/= Kwa watu Wa Dar es salaam Ofisi ya mhariri wa gazeti la serikali wapo pale darajani Karibu na Fly Over ya Veta Mataa , Ukishalipia malipo yao Unaenda kutuma posta Kwa mhariri wa gazeti la serikali Dodoma , Unatumia njia ya EMS Gharama yake 15000/= Unakaa ndani ya siku 21unafuata majibu yako ., Ukiwa Unatuma kwa mhariri hakikisha unahambanisha copy vyeti Au Vinavyotambulisha taharifa zako.

4. Hatua Ya Nne Unapeleka NIDA , utajaza Ile form ya nida upya ya Kuomba namba ya nida , utaenda serikali ya mtaa barua ya utambulisho na kugonga mhuri wa mtendaji mtaa Au kata , Baada ya hapo unarudi NIDA Uhamiaji wagonge mhuri Wao Baada ya Hapo utaenda Kwa afisa wa NIDA mapokezi kwa ajili ya kukutolea control number ILA UTARATIBU WA NIDA KWA MTU ANAYEBADIRI MAJINA KUANZIA MAWILI UNATAKIWA KUANDIKA BARUA KWA MKURUGENZI WA NIDA.

5. Hatua Ya Tano Ikabidi Niandike barua ya Kuomba kubadili majina kutoka A Kwenda B Kwa mkurugenzi mkuu Wa NIDA , nikamhuliza Afisa Nida barua inakaa Muda Gani kujibiwa akasema ajui Ila Inaweza kukaa Hata miezi 3 Hata 7 majibu yakawa Bado , Nikasema Duuuh Hii Hatari.

6. Hatua Ya Sita Baada Kukaa Mwezi Bila majibu nikaenda Ofisi Ya Nida ,wakaniambia majibu ya barua Yangu Bado , Ikabidi Niende Makao Makao Makuu Ya Nida Karibu Na Ubalozi Wa Ufaransa nikafanikiwa Kupata Barua Iliyojibiwa Kuwa ombi Langu Limekubalika La Kubadili Majina Kutoka A Kwenda B . Nilivyorudi Ofisi Za Nida Wakanibadilishia Majina Kwa Gharama ya 20,000/=

Japokuwa Watu Wanalalamika Kuhusu Nida Ila Nida Wanafanya Kazi Safi Na Wanakuelekeza Hatua Hadi Hatua Ya Kufanya , Nimehamua Kutoa Elimu Hii Maana Watu Wengi wanachangamoto Hii

1696078681927.jpg
 
Habari za muda huu ndugu zangu wa jamii forum, Watu (Wananchi ) wamekuwa wakilalamika juu ya hadha (usumbufu) wakati wakifuatilia juu ya kubadili majina Yao yalikosewa NIDA .
Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ombi lako la kubadili majina linaweza kukubaliwa Au kukataliwa inategemeana Na afisa wa NIDA kujiridhisha Na document zako ulizopeleka ..

HATUA NILIZOCHUKUA KUBADILI MAJINA YANGU MAWILI YALIYOKOSEWA..

1. Hatua Ya Kwanza Kiapo cha mwanasheria Au Mahakama kinachoomba kubadili jina kutoka A Kwenda B Kwa lugha ya kingereza wanaita DeedPol , Gharama Kwa mwanasheria ni 30,000/= maana zinakuwa jumla Karatasi 3 Ila ukienda mahakamani ukilia lia wataku charge 15,000/=
2.Hatua Ya Pili kupeleka kwa msajiri Wa Ardhi hizo Karatasi tatu ulizotoka nazo kwa mwanasheria au Mahakama . Kwa wakazi wa Dar es salaam unapeleka pale Ardhi kivukoni , unatakiwa kuambatanisha Vyeti Au Vitambulisho vinavyoonyesha hayo majina yaliyotofautiana , Kipindi kile walikuwa Wana charge 32,500Tsh/= Unakata Baada Ya Wiki (Siku 7) unafuata majibu Yako.
3. Hatua ya tatu kupeleka tangazo kwa mhariri wa gazeti la serikali , Gharama yake ni Elfu 20,000Tsh/= Kwa watu Wa Dar es salaam Ofisi ya mhariri wa gazeti la serikali wapo pale darajani Karibu na Fly Over ya Veta Mataa , Ukishalipia malipo yao Unaenda kutuma posta Kwa mhariri wa gazeti la serikali Dodoma , Unatumia njia ya EMS Gharama yake 15000/= Unakaa ndani ya siku 21unafuata majibu yako ., Ukiwa Unatuma kwa mhariri hakikisha unahambanisha copy vyeti Au Vinavyotambulisha taharifa zako.
4. Hatua Ya Nne Unapeleka NIDA , utajaza Ile form ya nida upya ya Kuomba namba ya nida , utaenda serikali ya mtaa barua ya utambulisho na kugonga mhuri wa mtendaji mtaa Au kata , Baada ya hapo unarudi NIDA Uhamiaji wagonge mhuri Wao Baada ya Hapo utaenda Kwa afisa wa NIDA mapokezi kwa ajili ya kukutolea control number ILA UTARATIBU WA NIDA KWA MTU ANAYEBADIRI MAJINA KUANZIA MAWILI UNATAKIWA KUANDIKA BARUA KWA MKURUGENZI WA NIDA
5. Hatua Ya Tano Ikabidi Niandike barua ya Kuomba kubadili majina kutoka A Kwenda B Kwa mkurugenzi mkuu Wa NIDA , nikamhuliza Afisa Nida barua inakaa Muda Gani kujibiwa akasema ajui Ila Inaweza kukaa Hata miezi 3 Hata 7 majibu yakawa Bado , Nikasema Duuuh Hii Hatari
6. Hatua Ya Sita Baada Kukaa Mwezi Bila majibu nikaenda Ofisi Ya Nida ,wakaniambia majibu ya barua Yangu Bado , Ikabidi Niende Makao Makao Makuu Ya Nida Karibu Na Ubalozi Wa Ufaransa nikafanikiwa Kupata Barua Iliyojibiwa Kuwa ombi Langu Limekubalika La Kubadili Majina Kutoka A Kwenda B . Nilivyorudi Ofisi Za Nida Wakanibadilishia Majina Kwa Gharama ya 20,000/=
Japokuwa Watu Wanalalamika Kuhusu Nida Ila Nida Wanafanya Kazi Safi Na Wanakuelekeza Hatua Hadi Hatua Ya Kufanya , Nimehamua Kutoa Elimu Hii Maana Watu Wengi wanachangamoto Hii

View attachment 2767597
Nani kakudanganya deedpoll ni 30,000?
 
Naona ni usumbufu kwa muombaji..

kama wao ndio walipokea fomu wanayo na wanaona ni makosa yao wao..

Ingekuwa mtu kakosea hapo sawa hatua zote hizo.. ila sio wao kukosea na vi typo vyao vya kutokufanya kazi kwa umakini na kuwa na mtu wa kuhakiki vizuri kabla ya kupitisha.
 
aisee kuna jamaa yangu amepata hili tatizo inabidi nimjuze huu mlolongo
Binti yangu kafanikiwa kubadilisha, lkn huko ardhi hatukwenda. Shida ni kwamba wafanyakazi wa nida wao wenyewe hawana taarifa sahihi ya nini cha kufanya, ukienda leo unaambiwa kalete moja, mbili, tatu, kesho yake ukienda unakutana na mwingine nae anakwambia kafanye moja mbili tatu.....nenda rudi ni nyingi but tulifanikiwa
 
njia gani ulipitia mkuu
 
Back
Top Bottom