Nataka Kupima...

Nataka Kupima...

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,334
Reaction score
23,940
NATAKA KUPIMA…

Ayayayaya….
We niache niende..niende niende….

Usiniulize kwanini sababu utanizingua, ukitaka jiunge na mimi mara ya mwisho ni lini we ulipima
Mi mwanzo sikuamini nikajuaga siezi ukwaa, kumbe mjinga ni mimi nayekula maganda meyatoa.

Oh uzinzi…uzinzi ulinifanya Muumba nikamzoea vibaya
Mi siezi pitisha hata siku bila kumuona Tina
Oh uzinzi…uzinzi ulinifanya Muumba nikamzoea vibaya
Na nina wengi ah..nimewapitia peeku.

Nataka kupima (PIMA)
Mi nataka kupima (PIMA)
Nataka kupima (PIMA)
Nikikutwa nianze dozi!!!!!

Ayayayaya….
We niache niende..niende niende….

Mi kwa uzinzi tajiiri, nkajivisha na taji la ubingwa
Sijali vimini-mini, ama wageti wanaofugwa ntawaomba
Kumbe wenzangu na mimi ni bure tu nlijisumbua
Wengine kama ishirini waliomba wakapewa na kavu wakagonga.

Oh uzinzi…uzinzi ulinifanya Muumba nikamzoea vibaya
Mi siez pitisha hata siku bila kumuona Tina
Oh uzinzi…uzinzi ulinifanya Muumba nikamzoea vibaya
Na nina wengi ah..nimewapitia peeku.

Nataka kupima (PIMA)
Mi nataka kupima (PIMA)
Nataka kupima (PIMA)
Nikikutwa nianze dozi!!!!!

Ayayayaya….
We niache niende..niende niende….kupima..kupima…

Wasalaam wapendwa,
Mentor!

NB:
Nimekaa nikafikiri, nimekuja kugundua WE ONLY LIVE ONCE..but if you live it right, ONCE IS ENOUGH. Nisingependa mwingine aje kuimba huu wimbo kama mimi.

Jitafakari…then jiulize, “NATAKIWA KUPIMA?” Nafsi ikikataa kwenda jiambie tu moyoni, “Ah, namsindikiza Mentor”..then, CHUKUA HATUA!!!!!
 
Jitafakari…then jiulize, “NATAKIWA KUPIMA?” Nafsi ikikataa kwenda jiambie tu moyoni, “Ah, namsindikiza Mentor”..then, CHUKUA HATUA!!!!!
Mentor naona kile kitengo chenu cha kupambana na Ukimwi kimeanzisha style mpya ya kusambaza ujumbe wao.

Back to topic.
Hongera kwa ujasiri ulio uonyesha hapa Jf wa kutaka kuijua afya yako ila sitegemei kama utaishia hapa hapa Jf, naamini utafanya kwa vitendo.

Usisahau kunPM matokeo yako kama hutojali.
 
saudari jibu hilo hapo...Cc: wengine wote mtakaoulizia majibu yangu:

...ukitaka jiunge na mimi mara ya mwisho ni lini we ulipima

...CHUKUA HATUA!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mentor Mkata kiu anajiunga na wewe.. So tunaanzia wapi AMREF au ANGAZA...

Ngoja nimuite na bi mdogo lara 1 nae aungane na sisi
 
Last edited by a moderator:
Mentor Mkata kiu anajiunga na wewe.. So tunaanzia wapi AMREF au ANGAZA...

Ngoja nimuite na bi mdogo lara 1 nae aungane na sisi

Muda wooote tangu utuambie unataka kupima kumbe ulikuwa bado? Au hii ni mara ya pili? Hahahaaaa......
 
Hii mara ya 3 hadi angaza wameshanizoea... Sema majibu ndio bado sijayachukua lol
mi mara ya mwisho nilienda kupima na beby wangu pale amref yaani majibu ni hapo hapo babu....
 
mi mara ya mwisho nilienda kupima na beby wangu pale amref yaani majibu ni hapo hapo babu....

Mi naenda na baby wangu pia ndio namsubiri twende Amref,,,,

It's foolish to fear what you can not avoid..

So no way out madam test lazima...
 
Hii mara ya 3 hadi angaza wameshanizoea... Sema majibu ndio bado sijayachukua lol

Hahahaaaaa..... Sasa majibu unamuachia nani huko ANGAZA?

Twende nikusindikize nikusaidie kuyachukua hayo majibu yako..!!
 
Hahahaaaaa..... Sasa majibu unamuachia nani huko ANGAZA?

Twende nikusindikize nikusaidie kuyachukua hayo majibu yako..!!

Uyachukue yangu baada ya kupewa ya kwako kwanza..

Sio unanisindikiza unaishia nje..
 
Mi naenda na baby wangu pia ndio namsubiri twende Amref,,,,

It's foolish to fear what you can not avoid..

So no way out madam test lazima...
toka siku ile hujapima?nenda tu yaani kuishi kwa kujua afya yako ujanani raha kweli..ndo maana naringia papuchi yangu kwa raha zangu siku hizi...
 
Nimezoea kuona watu wanabadilisha nyimbo nzuri kuzifanya kuwa za kijinga. Bt this time kwenye historia yangu naona nyimbo ya kijinga imefanywa kuwa ya busara...
Shikamoo Mentor
 
kupima nini?

Mh! urefu wa prof. maji marefu

Mentor Mkata kiu anajiunga na wewe.. So tunaanzia wapi AMREF au ANGAZA...

Ngoja nimuite na bi mdogo lara 1 nae aungane na sisi

Thanks bro...waite na Mrembo by Nature, mimisa, christine ibrahim, sakapal, Kaunga, mzabzab, Mtambuzi, Asprin, dr. watu8, Elli, Rural Swagga ...et al..

mi mara ya mwisho nilienda kupima na beby wangu pale amref yaani majibu ni hapo hapo babu....

Naomba utusindikize Smile...:A S 20:

hapo Amref ni wapi Smile? na me nataka kupima serious

Kwani hapo amref mkifika mnakaribishwa na soda pia au?
 
Last edited by a moderator:
Km utakuwa umeumia ni pm tuanze ishi kwa matumain au wasemaje??
 
Kwa kweli hofu niliyoipata wakati naenda kupima Ukimwi miaka 5 iliyopita ni zaidi ya ile niliyoipata utotoni nikiwa na Aka kama 6 hivi nilipopata taarifa kwamba nitahitajika kwenda kukutana na mkasi kwa ajili ya kutoa ngozi kwenye Mtwangio wangu...Ilikua ni kwa Kairuki na ndio kwanza nilikua nimepata ajira yangu ya kwanza hapa town HR wa hiyo Company (ni ya kigeni) akasema anahitaji FULL MEDICAL CHECK-UP REPORT kufika hospitali nikapima kila kitu ila Ngoma nikaacha ...nikarudi faster kwa HR nikamkabidhi na kwa vile muda ulikuwa umekwenda ikabidi nisepe Maghetoni kupumzika.Kesho asubuhi HR huyo akasema kuna kitu cha muhimu kuliko vyote nimesahau hehehe Kupima NGOMA..nikazuga zuga pale job weeee mwisho nikapiga moyo konde maana hata Comfirmation Letter nilikua sijapatiwa.Ikabidi nirudi kwa Kairuki kufika nikaambiwa vp unahitaji ushauri wa DR kwanza kabla ya vipimo nikajibu hapana Basi wakanipima nikawa nasubiria jibu kwenye benchi....Mara yule jamaa wa Maabara huyo na vikaratasi anasoma majina akaita Rural Swagga....x9 hivi mimi kimyaaa ...nikanyanyuka nikaingia Bar flani hivi ipo nyuma ya Kairuki Buddha Blue nikapata kinywaji kuweka Ubongo sawa kumbe ndio kwanza nazidisha feelings .....nikakumbuka Game zote nlizocheza kuanzia O level mpaka University....Ila pombe noma nikajisemea potelea mbali watu wangapi nawajua wana Mdudu na wanakula Gudtyms to the fulest.:clap2:Basi nikarudi moja kwa moja mpaka Kairuki nikaulizia majibu yangu...Jamaa akauliza tena vp unahitaji kumuona DR kabla ya kupata majibu nikasema hapana Basi jamaa akafunguka akanipa hongera kwamba niko safi kabisa...Nakumbuka nilikua sijawahi panda Teksi kwa muda mrefu ila that day nilipanda Tax mpaka job nikampatia HR majibu yake....From that day nimepunguza kama si kuacha kabisa Ngono zembe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom