Nataka kununua gari naomba ushauri!

Binti hakuna gari utakayotumia chini ya elfu kumi kwa siku !

Ngoja tuweke mambo sawa.
Mwenge - Posta ni kama 10km hivi. Ukifanya na kurudi inakua 20km. Na labda foleni + AC ni mafuta ya 5km, so kwa siku ni 25km bila misele mingine.

Vigari vinavyozungumzwa hapa vinaenda kuanzia 10km/lt - 15km/lt, so average au approximatee tufanye 13km/lt. Ndio kusema kwamba vitahitaji lita mbili kutoka Mwenge hadi Posta na kurudi.

Bei ya mafuta approximate ni Tshs 2,000/- kwa lita. So lita 2 ni kama Tshs 4,000/- kwa siku. Ndio kusema kua kwa yule wa siku tano za kazin atatumia Tshs 4,000 x 5= Tshs20,000 kwa wiki bila kuweka misele ya wikiend.

Hesabu hizi zimeweka assumptions mbalimbali kwamba kila siku unapita njia hiyohiyo tu. Pia Injini ya gari ipo kwenye same condition daily. Assumption ingine ni kwamba gari hii inakwenda 13km kwa lita, so kama inakula poa zaidi ya hapo, mafuta yanaweza kufika wikiend. Pia assumption ingine ni kua foleni + ac = 5km kwa siku, so kama vio viko chini ni faida zaidi.

Ukanyagaji wa kibati cha mafuta nao unachangia. Kama we unaendesha kama upo kwenye Formula one nalo ni tatizo pia.
 
mm ninayo jeetpatel ila kwa pesa uliyo nayo ongeza kidogo ni pm nikujulishe kama unataka kuiagiza kwa kampuni yetu ya kiloloma investment and extenal payment account.
 

Nimekupa mchanganuo hapo chini naona una hasira ya gari kuja kuliendesha ukubwani baada ya kuhustle sana wakati wengine toka wamezaliwa wameyakuta home..

Nimekupa mchanganuo hapo chini nenda kasome kisha uje ulete jibu mwenyewe..

Bei ya petrol ni 1990 per litre,,, ukiweka 20,000 unapata almost litre 10,,, ambayo inakupa km 120 sasa zigawanye hizo km mwenyewe kwa siku 5 za wiki working days kwa gari ya cc 1300 then ulete majibu hapa wewe mwenyewe...
 
Bugatti Veyron
Lamborghini Reventon
Aston Martin Vanquish.
Hizi gari used zinapatikana wapi wakuu?
 

Mkata kiu graduate wa mzumbe mkaazi wa mwenge tokea umeanza kazi una mwaka wa tatu. Na umenunua gari moja gx 100 as ulivyosema . Na umewahi kutumia magari kibao kutokana na wazazi means familia bora . Unawakilisha graduate wa mzumbe na wakaazi wa mwenge. Hivi nitakuoneaje wivu wakati hapa tunaona I'd tu? Wewe ndio graduate . Anyway naipenda nchi yangu tanzania na naionea huruma kuwa na watu wa aina. In short sipo tz na niliondoka huku muda mrefu ila kila mwaka narudi likizo na hata mwaka huu nitarudi so usifikirie kila aliyepo hapa katoka mzumbe au mwenge
 
Ingekuwa tanzania watu wanatumia mafuta ya elfu 20 kwa week moja basi nadhani watu wasingepaki magari coz of mafuta. Hata gari as long as ni gari hata ingekuwa na cc 1000 huwezi kutumia elfu 20 mwenge to posta na kurudi per week labda iyo barabara uwe unapita wewe peke yako haina hata trafik light bado pia haitoshi. Labda pikipiki
 

Ha ha ha ngoja nikupe ushindi naona unabadilisha mada sasa, maana ulianza na hakuna corolla 111 ya cc 1300, ukaja na hakuna gari inayotumia elfu 20 kwa wiki kwa umbali wa mwenge-posta,, sasa umeamia kwenye mambo ya makazi?
Sasa umekuja na sababu upo nje ya Tanzania so umbali wa mwenge posta hujui ukoje! Naona ni bora tumalize ubishani tumsaidie dada apate gari nzuri.

Ngoja nikupe ushindi kaka ili yaishe na samahani kama nimekukwaza
 
mm ninayo jeetpatel ila kwa pesa uliyo nayo ongeza kidogo ni pm nikujulishe kama unataka kuiagiza kwa kampuni yetu ya kiloloma investment and extenal payment account.

mkuu thax. kuna kampuni nitawaagiza na tumewahi kuitumia kabla.
 
PM kwa mchakachuaji192,vitz yake ni nzuri na bei sio mbaya,imeagizwa muda mfupi tu
 
 
Ahsante dadaangu neggirl kwa kuleta hili wazo hapa..umenisaidia sana manake i was trying to do the same thing...Shukrani pia zikuendee MKATA KIU Umeinogesha sana hii thread na umetutoa tongotongo wengi wetu...
 
Last edited by a moderator:

Mkuu average ni kwenye mwendo ambao uko na gia gani? Kwa foleni hizi za hapa mjini sijui kama utapata hiyo average yako.
 
Mi sio mtaalamu sana wa magari lakini magari kama vitz, Spacio fuel consumption yake ni ndogo japo sometimes mafuta yanatumika sana kutokana na matumizi yako wewe mwenyewe, spacio inatumia 1Ltr kwa 15km if i'm not mistaken

hapo kwenye fuel consumption kwa spacio sizani kama kuna ukweli! ninayo spacio cc 1598 matumizi ya mafuta ni lita moja kwa km 9 hadi 10. kwa masafa marefu ndo unaweza kwenda kwa km 12.
 
Your welcome SnowBall.

By the way... MKATA KIU kasaidia wengi hapa ingawa wengine wanamtupia mawe lol.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Sikudanganyi Daadangu unajua ni vizuri ukaujaua ukweli uweze kujipanga !

Haya MANI nitaufanyia kazi ushauri wake.
Off topic kdogo... Hyo avatar yako inatisha bana!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Haya MANI nitaufanyia kazi ushauri wake.
Off topic kdogo... Hyo avatar yako inatisha bana!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Sawa bibiye lakini usitishike ukiamua utaweza.

Off topic hii avatar mbona siombaya ki ivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…