Nataka kumuhudumia mtoto peke yake

Nataka kumuhudumia mtoto peke yake

pakaywatek

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
4,710
Reaction score
6,372
Nipeni ushauri jinsi ya kumuhudumia mtoto bila mama yake kunufaika manayake sitaki huyu mwanamke aonje pesa zangu ninazotoa kwa ajili huyo mtoto, tangu nianze kutoa gharama za matunzo huyu mwanamke anazidi tu kunawiri inaniuma sana.
 
Haahahaaaaaaaa! Wanaume kwa roho za mchongoma siwawezi. Basi kuwa hutoi cash, kama lukuunapeleka luku, maziwa unanunua kabisa, nepi, pampers, unga, mafuta, kila kitu, nguo, sabuni, maji yaani hadi chumvi na sukari. kAMA ADA UNALIPA KABISAA. Unahakikisha hali senti tano yako.
 
pakaywatek

Wacha roho ya korosho mkuu,
Wewe uliona raha kujikunja na kumkojolea Dada wa watu sasa hivi amekuzalia mtoto unaona ngumu kuwatunza wote....
Tunza wote wacha roho mbaya..

Na Kama kuna mchepuko una honga hela afu mama mtoto unambania...hiyoo ni LAANA tupu..
 
Last edited by a moderator:
Mhh nani aliyeturoga sisi jinsia me
 
Dah!!

Binadamu tuna mitazamo hasi hadi baasi...!!
 
Kwani wakati mnatafuta huyo mtoto ulikojolea pembeni ukazimimina kwa mkono ndani ya kiungo chake cha uzazi. Peleka matumizi bila kubagua, huwezi kukwepa yeye kutokunufaika na matunzo yako. Peleka vitu zaidi na pesa kidogo.
 
Hizi ndo bifu za kipumbavu ambazo mwisho wake huwa mbaya sana mkuu badili huo mtazamo yani haiwezekani kabisa
 
Huo ni ubinafsi we mtu.una roho ndogo kichz.unahtaj maombi.uskute ata hanawiri kwa pesa yako.atapendeza tuu ata ufanyeje.
 
afu yawezekana kuna mchepuko unakula hela yako ....peleka matumizi mwanaume..
 
hamuwez kujua uyo mwanamke amemfanya nn jamaa msi hukumu...mm kid wangu nilimchukua nakaa nae ila mama ake stak ata kumsikia

Hata mimi naamini kuna jambo la muhimu hajalisema na hivyo hoja yake inakosa mashiko kabisa.

Siamini from no where mtu mwenye akili timamu anaweza kuzalisha hoja kama hii kichwani mwake.
 
Mhhh...furaha ya mwana mamiye so akinawiri mama na mtoto ana furaha mkuu...mama akiwa dhoofu kajichokea hana furaha ujue itamuathiri na mtoto wenu.Kwasababu stress zitakuwa zinamuandama na yeye.Be proud you are a responsible father na ondoa chuki/uhasama kati yako na mzazi mwenzio.
 
Hata mimi naamini kuna jambo la muhimu hajalisema na hivyo hoja yake inakosa mashiko kabisa.

Siamini from no where mtu mwenye akili timamu anaweza kuzalisha hoja kama hii kichwani mwake.

wapo mkuu wala usishangae.
 
pakaywatek

Lifikirie hili katika uwanja mpana zaidi, binafsi najua unachokiongelea lakini huna jinsi kwa asilimia mia moja kuweza kumzuia mzazi mwenzako asinufaike na pesa unayotoa

Inawezekana kabisa pengine ni mtu wa starehe sana hivyo kukosa muda wa kukaa na kumhudumia mtoto ipasavyo !!!INAUMA NA KUUMIZA MNO MOYO
Fanya hivi muwekee msichana wa kazi halafu jitahidi kununua vitu mwenyewe kuliko kutoa cash! Malezi ya namna hiyo yana changamoto zake nyingi tu
 
Last edited by a moderator:
hamuwez kujua uyo mwanamke amemfanya nn jamaa msi hukumu...mm kid wangu nilimchukua nakaa nae ila mama ake stak ata kumsikia

Safi sana kijana umeonyesha upovu sio yale yanayoropa tuuu
 
Back
Top Bottom