Hebu kaa nae chini uzungumze nae..na umueleze ukweli alipo kosea na ikiwezekana ajirekebishe na akaombe msamaha! Naona kama umeharakisha sana labda kama hii si sababu ya pekee!Unajuaje hayo matatizo hayaku sababishwa na hali yake?
Yani unataka kuvunja ndoa kwa sababu rahisi namna hii? Mbona ndoa yenu inarekebishika kama sababu ni hii pekee? Tafuta wakubwa wako ,baba,mama na wakwe na mkeo mkae muongee myamalize! Kuvunja ndoa si rahisi namna hii..hatu ukienda popote wata shangaa sana kama hii ndio sababu!
Hebu kaa na mkeo muongee hii ni sababu dhaifu sana kuvunja ndoa msamehe msonge mbele..yani nguvu uliyotumia kufunga ndoa ivunjwe kwa sababu hii?Utatumia miaka kumi kuvunja ndoa kwa sababu hii!
Kaa chini myaongee!
Funguka kijana tabia gani mbaya kazifanya kwa mama mkwe wake?
FEDORA Uamuzi wako ndio mbaya sana/ mgumu sana lakini kwa baadhi tu ya majibu yako niliyoyapitia inonekana kuwa kichwani ZIMO,, Busara yako inonekana sana tu,, ebu tafakari ikibidi kabla ya huo uamuzi washirikishe ndugu wa karibu pande zote kwanza uone matokeo ikiwem onyo kali mbele ya wadau wote
naona unafanya maskhara na uzazi eeh. Mimba na uzazi ni kitu kikubwa. vinakuja na hormones kubadilika badilika na usipoangalia zina-create long term problems. hapo mkeo anahitaji support ya kisaikolojia, emotional, etc. tatizo mijianaume ya kibongo haitaki kujielimisha na mambo haya. MSAIDIE MKEO ACHA KUBWABWAJA!
Kwenda zako ukute mama yako ndio moto anauwasha ukiwa haupo ukiwepo anauzima,mama wakwe na wifi hua na midomo sana hata wake pia sikatai
we una sababu zako tu zingine
iyo unayotwambia siyo sababu ya kumuacha mke
hata mahakama aiwezi kutoa talaka kwa sababu kama yako
labda umwache kienyeji lakini kisheria ngumu
Nimeshafunguka kwenye post za nyuma ngoja ni copy na kupest kwako
Ulioa kwa ajili ya mama yako? Acha ufala
Hebu Jaribuni kuwa waungwana. Kwani hata kama hajaona kwa ajili ya mama yake ndio aone mama yake anatukanwa afurahie? Mnachokifanya ni kujaribu kuinusuru ndoa ya mwenzenu sio kitu kibaya ni sawa kabisa ingawaje hajaomba ushauri isipokuwa ameuliza sheria inasemaje katika hilo la kumuacha mke kwa makosa aliyoyataja.
Jambo alilolifanya mkeo kweli sio la busara kabisa. Maana wote wenye akili timamu tunaelewa kuwa mzazi wa mwenzio ni kama mzazi wako kwa hiyo unatakiwa kumpa heshima tena ya ziada. Na ili familia yako iwe na amani ni lazima heshima iwepo. Je mapenzi yatatoka wapi utakapoona mama yako anatusiwa mbele yako? Lazima tukubaliane kuwa alilolifanya sio jambo jema.
Lakini pia ukimuacha sitashangaa kwa kuwa yapo mengi ambayo umesema mkeo ameyafanya lakini hujayaweka wazi hiyo ni kutokana na sababu unazozijua mwenyewe. Lakini katika kufanya maamuzi hayo pia uwe makini ukizingatia vigezo vyote vilivyopo na vile vile hakikisha umejua sheria inasemaje.
Ushauri wangu kwa wanawake: tubadilike zamani wanaume ndio walikuwa wana kila sifa mbaya unazozijua lakini sasa hivi ni wanawake. Wanawake tumekuwa tunajiamini sana hasa tunapokuwa tayari tumeingia katika ndoa ndio mtu anafyatua kucha alizokuwa amezificha.
Na wachangiaji mada hebu someni mada kwa ufasaha kabla hujachangia uelewe kwanza. Sio watu wanaropoka tu.
Hata kabla ya hiyo mimba alishaanza kunivunjia heshima mm kwa domo lake chafu
Una lako jambo. Inaonekana wewe ndio mwenye domo chafu, inawezekana hata ulikua humjali huyo mzazi mwenzako...mfewwww.