bagabe
JF-Expert Member
- May 8, 2014
- 540
- 670
- Thread starter
- #181
Ok, achana na hao wanaokuona hauna akili sijui umemchezea bintu sijui kitu gani! Achana nao.
Hauhitaji sababu wala ruhusa kuachana na mtu.
Wala hauhitaji kutoa maelezo kwa mtu yeyote isipokuwa kwa huyo tu unaemuacha.
Usijilazimishe kuishi na mtu ambaye humtaki kwa kuhofia watu watakuonaje au kuogopa kumuumiza hisia.
Ukijilazimisha utaishi kwa majuto na pia huyo binti hatofurahia maisha na ataishi kwa mateso, maana hatopata anachotakiwa apate.
Kumsaidia mtu usiempenda ni kuachana nae, ili akapate watakaompenda.
Ninachokushauri jipe muda walau wa miezi kadhaa ukitafakari.
Ukiona bado 'humuelewi' achana nae mara moja, namna ya kuachana nae unaweza kuzingatia ushauri wa DR HAYA LAND ameeleza vizuri.
Kila la kheri na weekend njema.
Asante sana mkuu..naendelea nae