Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

Just imagine miaka mitano,5 years lakini anatafuta ushauri wa kumuacha.

Nimesoma kwa umakini nione popote alipotaja udhaifu wa huyo binti lakini nikakosa,mleta mada nakuambia nikiwa kama mtu mwenye experience ya kuishi na wanawake huyo ukimuacha utakuja kupata shida sana kuanza na mwengine upya sababu za kupoteza hisia siyo sababu za msingi na nashindwa kuelewa unapotezaje hisia na jinsia tofauti na yako.

Sielewi nini kimenikuta natamani hata aniroge nianze kumpenda upya.
 
Kitu sitaki ni kuutesa moyo wangu,

1. hivi ulianzaje kuwa kwenye mahusiano na mtu ambae humpendi na ukampa mimba? Mahusiano hayajaribiwi ni kama sumu haionjwi.
2. Au unaanzaje kulala na mtu kisa ulikuwa na stress ikabidi ujipoze usipo penda?
3. Huyo dada lazima aumie sana lakini ni bora nusu shari kuliko shari.

4. Mungu ana mipango yake ndo maana kaona huyo mtoto atateseka akamchukua mapema.

5. Usipoteze muda ukimaliza kusoma hapa, wewe mwambie ukweli muachane kabisa, na kama kuna kitu ulikinunua nae mwachie anza upya. Wewe si mwanaume bana? Anza upaya.

6. Leo hii mwambie kuwa humpendi

7. Usipo mwambia leo usiku mkalala wote nakuapia atapata mimba na utajuta kupuuzia nilicho kwambia. Na akipata mimba humuondoi tena.

8. Najua ataumia ila nae siku akipata ampendae kuna siku atakushukuru.

9. Wewe ndo humtaki so uwe tiyari
kupoteza baadhi ya vitu ambavyo mnamiliki, tumia busara mpe kila unachoona anatakiwa kupewa.

Hapa wabongo ndo tunafeli mzungu kama hakupendi wala hapotezi muda straight anakwambia sina hisia na wewe. Nyie mpaka uchomeke utest afu ndo uje na habari za kutokuwa na hisia. Mnakeraaaa.

Mwacha leo kabla yesu hajafufuka, mpaka yesu anafufuka awe na maisha mapya. Huwezi jua kwenye mkesha wa pasaka leo usiku anaweza kukutana na ampendae ufufuko ya Bwana yesu ukampa furaha ya milele.

Asante mkuu nimekuelewa sana.
 
aiseee Mungu aniepushe na wanaume wa sampuli hiii
Ndiyo waliobakia.Muende nao kwa steps.
Nifanyaje mkuu
Jipe muda wa kutafakari kuhusu miaka yenu mitano ya kuwa pamoja.Je,amekukosea nini?Amekikwaza kipi?Hisia zimeishaje?Elewa kwamba kila binadamu ana kiasi.Umekua naye kwa muda huo wote mapenzi yenu hayawezi kuwa kama ya siku ya kwanza.Yamedumu na kukua/kubadilika kulingana na muda na umri wenu wote wawili.Hamuwezi kuwa vilevile kila siku.Jaribu kuvaa uhusika wake halafu uachwe tu bila sababu ya msingi.Kwani nini kimebadilika kwake?
Utabadilisha wenza kadiri utakavyo lakini kupata mtu perfect umtakaye si rahisi.Tuliza akili na uzitumie kiufanisi.Akili,mwili na wakati vitakusuta.Havitakuambia uache utoto umekua.Shtuka na uchukue jukumu lenye hitimisho jema.
 
Back
Top Bottom