Nataka kumuacha japo ninampenda sana

Nataka kumuacha japo ninampenda sana

Ila maranying wanaokosea ndo huwa akili zinatulia sio rahis kurudia Kosa pia past watu wanakutana na vituvingi sana inawezekana pia hakupenda kuwa single mama pia lkn past yake ndo ikamfnya awe Bora Zaid Leo kama unampenda na unaamin anakupenda ilo ndo la muhimu
daaah naumia navitu vingi
 
Habari wakuu,

Naombeni kunisaidia njia ya kumuacha mwanamke unayempenda sana, yaani ukikaa dk 5 lazima umuwaze. Nahitaji kumuacha kwasababu zangu binafsi, ingawa ananipenda sana na mimi nampenda sana kutoka kwenye moyo wangu.

Cha kwanza amenizidi umri miaka 5, cha pili ana mtoto, cha tatu kashaachana na wanaume sita ambao mimi nimewashuhudia na bado sijui huko nyuma. Kwa jinsi ninavyompenda naelekea kuwa chizi kabisa, ameniteka ufahamu wangu na moyo ila nataka nimuache. Je, nitumie mbinu gani?

Asanteni.
Hapo dawa naona ni kuwa chizi tu. Naamini hatavumilia kuwa na wewe katika hali hiyo ya uchizi.
 
Wana matatizo mengi tu, cha kwanza wanafanya malengo na watoto wao yani wanaingia kwenye mahusiano kwaajili ya kutatua matatizo yake ya kiuchumi yeye na mtoto wake, kwa kifupi single mother %99 wanaingia kwenye mapenzi kwaajili ya kupata pesa za kulea mwanae tu yaani hawaangalii jambo jingine zaidi ya kutaka kupewa pesa tu ya kumlea mwanae.
Kweli kabisa mkuu , hapo ndipo single mother wengi wanapofeli
 
Kama umeweza kumpenda baada ya kujua ana mtoto,ni mkubwa kwako kaachwa mara sita na bado ukaweza kumpenda huyo ni size yako.Cha muhimu ni kuhakikisha wewe na yeye mnakuwa na maleno na mko serious kuyajenga.Unless.....
Sawa boss me sina shida kuhusu mtoto je kwa Dunia ya sasa Umri autokuwa shida sana ?
 
Habari wakuu,

Naombeni kunisaidia njia ya kumuacha mwanamke unayempenda sana, yaani ukikaa dk 5 lazima umuwaze. Nahitaji kumuacha kwasababu zangu binafsi, ingawa ananipenda sana na mimi nampenda sana kutoka kwenye moyo wangu.

Cha kwanza amenizidi umri miaka 5, cha pili ana mtoto, cha tatu kashaachana na wanaume sita ambao mimi nimewashuhudia na bado sijui huko nyuma. Kwa jinsi ninavyompenda naelekea kuwa chizi kabisa, ameniteka ufahamu wangu na moyo ila nataka nimuache. Je, nitumie mbinu gani?

Asanteni.
Vuta subira tu mkuu akuache yeye
 
Kama hauna malengo na mnataka kuwa tu na yale mahusiano ya kugegedana tu bila ndoa au kuishi pamoja naye mwambie tu waziwazi.

Ikiwa hayupo tayari piga chini. Kikubwa ili kukatisha urafiki ni kukatisha mawasiliano wadau huko juu wameelezea vizuri jinsi ya kukatisha mawasiliano
 
Kumbe lkn ni mtazamo sidhani km ni uhalisia
Ni uhalisi lakini siyo single mother wote, hizi tabia zao tumezishuhudia kwa ndugu jamaa na marafiki utakuta single mother kaolewa kazaa watoto,utakuta kafunguliwa biashara lakini biashara haikui inakufa kumbe kuchunguza anatumia pesa za mauzo kwa kumlea mtoto wake uko kijijini na kumjengea Nyumba bila mume kujua, na kisingizio chao watoto wengineo baba yao atawahudumia, na kumbuka huyo mtoto wake ana baba yake.
 
Kweli kabisa mkuu , hapo ndipo single mother wengi wanapofeli
Akili zao fupi fupi yani wao wana muacha baba mtoto ana kula maisha tu halafu majukumu ya kulea wanampa kijana mwingine hakuna mwanaume atakaye kubali kubeba Zigo la mtu mwingine na ukiona mtoto analelewa na baba mwingine huyo mtoto ni yatima kaokotwa tu au mtoto wa ndugu au rafiki ndiyo jamii inalea mfano mtoto wa Ruto aliyemchukua katika nyumba za kulea watoto.
 
Muue[emoji3525]
IMG_20210914_111349.jpg
 
Back
Top Bottom