Nataka kumpeleka mwanangu Bunge Primary, je nitakuwa nimekosea?

Machuchu

JF-Expert Member
Mar 31, 2017
1,260
962
Za leo wanajamvi.

Kutokana na kipatochangu kuwa kiduchu nashindwa kumpeleka mwanangu shule zingine kama St. ........ na International....... Napenda kumpeleka Bunge primary school ambayo [HASHTAG]#Nimesoma[/HASHTAG] mimi mwenyewe pale la I-VII. Je, nitakuwa nimekosea au nipo right.

Msinitukane wala kunikebehi naombeni ushauli tu.
 
Kuna watoto ninawafahamu wamesoma shule hizi hizi tulizosoma sisi, wazazi wao waliwekeza tu kwenye tuition za J'mosi. Vijana wale wanamaendeleo mazuri sana. Ni jitihada zako wewe mwenyewe kama mzazi na mtoto mwenyewe alivyo.
Asante sana
 
Kuna haja ya kufanyika study kati ya wahitimu wa st's na kayumba. Sio ya kuangalia matokeo no. Return ya education kati ya graduates hawa wawili.

Au ilishafanyika?
 
Matatizo wazazi wengi wanategemea mfumo wa elimu bila kuongeza jitihada za ziada kwa watoto wao. Baba hajui hata mwanae yuko darasa la ngapi.
 
Siyo kosa wala usifadhaike, katika maisha kupata na kukosa zote ni hali, ikiwa uwezo wako haukuruhusu kuwapeleka kwenye shule wanazolangua elimu, wapeleke kwenye shule wanazobania elimu, ila cha msingi akikisha unawatafutia mwalimu wa kuziba mapengo na kuwapa wasaha wa kufurahia michezo ambayo kwenye hiyo shule ya umma haipo.
 
Uko sahihi tena usiwe na shaka kabisa.
Mjengee utamaduni wa kujisomea vitabu mtoto wako tangu akiwa mdogo, Elimu kwake itakuwa rahisi sana.
Kuna dada tulisoma nae shule ya msingi Alikuwa anjua english kuliko nadhani hata waalimu wetu, Kila mtihani lazima aongoze, Kuja kufuatilia kumbe baba yake alikuwa anamletea waalimu wa kumfundisha home yeye na wadogo zake.
Mpangie ratiba vizuri, mwanao anaweza kufanikiwa sana kupitia hizi hizi shule zetu choka mbaya...
 
Jamaniiiii
 
Matatizo wazazi wengi wanategemea mfumo wa elimu bila kuongeza jitihada za ziada kwa watoto wao. Baba hajui hata mwanae yuko darasa la ngapi.
Shule za kayumba zina vingi vya kujifunza saana kama mwanafunzi atafanywa awe active(both teacher and parent) .

Kayumbas zina akisi uhalisia ukiachilia Mbali content.
 
Hii ndio sababu kuu. Kutwa kuringishia shule za gharama wanazosomesha...wengine nao wanaona isiwe taabu,wanafunga mkanda.
Imekuwa kama fashion flani hivi...
Unampeleka mtoto shule ya gharama, unatoa pesa yote, ukiambiwa mtoto anaugojwa matibatu yatagharimu milioni tano unapata pressure.
 
Shule za kayumba zina vingi vya kujifunza saana kama mwanafunzi atafanywa awe active(both teacher and parent) .

Kayumbas zina akisi uhalisia ukiachilia Mbali content.
Ukimpata mwalimu wa hizo shule za private awe anamfundisha mwanao J'mosi mnakubaliana kwa mfano laki moja kila mwezi ni nafuu kuliko hizo milioni 15-20 utakazolipa hizo shule za wenye nazo.
 
kama unampeleka mtoto bunge na hauna usafiri wa uhakika wa kumpeleka na kumrudishA AKAWA ANAPANDA DALADALA JUA UNAANDA KIBAKA,

Bunge ilikua zamani saizi watoto wa uswazi wako pale na tabia chafu
 
Za leo wanajamvi.

Kutokana na kipatochangu kuwa kiduchu nashindwa kumpeleka mwanangu shule zingine kama St. ........ na International....... Napenda kumpeleka Bunge primary school ambayo [HASHTAG]#Nimesoma[/HASHTAG] mimi mwenyewe pale la I-VII. Je, nitakuwa nimekosea au nipo right.

Msinitukane wala kunikebehi naombeni ushauli tu.
wakati mimi na wewe tunasoma Bunge,Forodhani,Muhimbili,Upanga,Olympio etc ndio zilikuwa shule bora za msingi.....
 
Back
Top Bottom