Nataka kujua fursa zinazopatikana wilaya ya Mpanda

Mwalimu Ntuntu

JF-Expert Member
Jun 3, 2016
305
279
Habari Wana Jamvi! Hongereni kwa Sherehe za mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka ujao!

Mimi ni mmoja wa wale wanaopenda kujua fursa kutoka maeneo mabalimbali ili kuimarisha mawazo fikra za uwekezaji.

Leo natamani sana kuijua Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi. Kwenye kuijua hasa upande wa fursa na huduma za kijamii....

Njooni Wana Mpanda.....mtujuze mazuri ya kwenu
 
Kwa upande wa kalambo ,ukiwekeza kwenye hotel unaweza kupiga pesa,ingawa mara ya mwisho nimekuta Kama Kuna majengo yanaanza kujengwa,(2018) ingawa sikudadisi Sana kama ni ya serikali au mtu binafsi.

Ila Kama utaamua kwenda kuwekeza kwenye hiyo sector naomba uni pm ili nikuunganishe na ndugu zangu wa pale pale kalambo(Kijiji Cha kapozwa) naimani unaweza kuwapa temporary employment na ikiwezekana parmanent kabisa
 
Hivi pale karibu na sumbawanga kuna eneo lilikuwa limewekewa manyaya mpaka juu na antena kubwa sana nilipouliza wakaniambia ni kwa ajili ya kuzitega radi zikiporomoka angani ziangukie hapo ni siku nyingi nimetoka huko je bado papo?
 
Mpanda sio wilaya, ni sawa na kusema unataka kwenda wilaya ya Iringa. We ungesema tu nataka kwenda Mpanda.
Kilimo ndio kwake huko, ila ujidhatiti kwanza.
 
Mpanda fursa ni kilimo na biashara za maduka ya mazagazaga yaani bidhaa mchanganyiko na maduka ya madawa kwenye vijiji vyake, maeneo ya kilimo ni mengi bei bado ni ndogo ila ya kulimia mpunga bei iko juu, ukitaka kuifaidi katavi njoo na ubunifu mzuri utapiga hela sana maana huku elimu bado sana na watu wengi hawana elimu.

Karibu sana Katavi
 
Mkuu naomba uni PM
 
Back
Top Bottom