Nataka kufungua Studio ya Picha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kufungua Studio ya Picha

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Shomari, Jun 18, 2012.

 1. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Jamani wanajukwaa wenzangu. kwanza kabisa asalaam alaykum pia bwana yesu asifiwe sana. Mimi nina nia ya kuanzisha biashara ya upigaji picha katika maeneo ya jiji la Mwanza. kuna mtu yeyote mwenye uzoefu anayeweza kuniambia itanigharimu kiasi gani kufungua studio ya kisasa kabisa, na ni vifaa gani hasa ambavyo ninatakiwa niwe navyo?. natanguliza shukrani zangu za dhati.
   
 2. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  wewe hapo ulipo una kiasi gani? ina hiyo ya biashara na zinginezo, hakuna mtaji maalum wa kuanza nao, inategemea na malengo yako na uwezo wako. Ila ukitaka iwe modern photo studio tafuta mtaji usiopungua milioni kumi then, fanya business research kwenye photo studios nyingine, then andaa mpango wa biashara, kisha anza biashara.
   
 3. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,457
  Trophy Points: 280
  tafta printer flan za apson zinauzwa kuanzia laki sita, tafta professional camera canon, tafta computer yenye uwezo wa kutumia adobe photoshop, na tafta location nzuri umtafte designer apambe photo room yako. Kwa hesabu za haraka haraka kwa kuanzia mil 3 zinatosha
   
 4. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  maelezo yote ametoa elmagnifico sina la kuongozea
   
 5. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  elmagnifico na wengine wote kwa kweli nimefurahi na ninashukuru sana kwa mchango wenu, kitu kingine naona watu wengi sana wanatumia Nikon siku hizi, je , inakuwa na ubora zaidi kuliko Canon au ni fasheni tu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Buggy

  Buggy JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nikon na Canon zote ni camera nzuri tu. Ni kiasi tu cha kujua exactly model ipi utachukua. Mimi nimeisha tumia Canon D50, ni nzuri ingawa sasa kuna models nzuri zaidi. Na sasa natumia Nikon D5000, ni nzuri sana tu! Ni bajeti yako tu. Bei zake hizo ni kati ya $ 800 - 1500.
   
 7. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2013
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  nahitaji studio lights mkuu, wapi ntapata?? na aina gani ni nzuri??? na zenye watts ngapi zinafaa kwnye chumba cha 3m *3m
   
 8. jluvanda

  jluvanda Member

  #8
  Dec 20, 2013
  Joined: Jan 15, 2013
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kampuni ya Chinaworldbuz Company Limited (CWB) ni kampuni ya muungano wa vijana wa kitanzania na kichina waishio jijini Shanghai-China.Kampuni hii iliyoanzishwa february mwaka 2012 jijini Shanghai kwa Lengo la kuifikia jamii ya wafanyabiashara wa Tanzania na Africa kiujumla watakao kununua bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kutoka nje ya nchi (hususani China) kwa ajili ya kuboresha biashara zao.Kutokana na kuwa na changamoto nyingi zinazowapata wafanyabiashara wa Tanzania katika nyanja za kukataliwa kibali cha kuvuka mipaka(VISA REJECTION), ugumu wa lugha ya kichina( LANGUAGE BARRIER),kupata bidhaa bandia (FAKE GOODS)katika masoko madogo madogo ndani ya China na pia kukosa mahusiano ya moja (DIRECT LINK) na viwanda vitengenezavyo bidhaa mbali mbali nchini China. CWB ni njia sahihi ya kuweza kuboresha biashara yako bila kukutana na changamoto tajwa hapo juu, ni rafiki mwema wa biashara yako, ni njia sahihi ya kuweza kutimiza ndoto zako katika uwanja huu wa biashara. CWB,Tunatoa elimu ni jinsi gani ya kufanya kazi na sisi, tuna toa ushauri ni aina gani ya biashara mtu anaweza kufanya kulingana na mtaji wake, tunatoa maelezo ya kina kuhusu bidhaa zetu zote tuzitoazo mfano simu, tablets,nk. Kwa Sasa makao makuu ya ofisi za CWB yapo jijini Shanghai na ifikapo January 2014 ofisi zetu zitahamishiwa Ushirika Tower jijini Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea website yetu www.chinaworldbuz.com pia unaweza wasiliana nami kwa email juely2006@yahoo.com au justineluvanda@gmail.com, simu namba +8613524159707.  Usiwe na shaka kuuliza au kuhitaji mafafanuzi ya kina. Tupo kwa ajili ya kufikia mahitaji ya wafanyabiashara na watu wanaotaka kufanya biashara.  Asanteni.
   
 9. Deo Corleone

  Deo Corleone JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2013
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 14,660
  Likes Received: 2,526
  Trophy Points: 280
  We jaamaa wa china unazingua,kila post upo.
   
Loading...