Nataka kufungua business training centre, msaada kwenu wana JF vitu vya kuzingatia

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Heshima yenu wana JFnataka kufungua business training centre kwa ajili ya kutoa mafunzo na semina ndogo ndogo za wajasilimali ambapo nitakuwa natoa mafunzo na semina kuhusu.

Mambo ya biashara, ushauri wa kibiashara, masoko na mifumo mingine ya kibiashara.

Hivyo nahitaji msaada wenu ni vitu gani muhimu vya kufahamu na kuzingatia kwa watu nitakaokuwa nawafundisha.
 
Kwanza wewe uwe certified kwenye hiyo field. Tumechoka watu wanaomwaga presentation za kudownload Google
 
Heshima yenu wana Jf nataka kufungua business training centre kwa ajiri ya kutoa mafunzo na semina ndogo ndogo za wajasilimali ambapo nitakuwa natoa mafunzo na semina kuhusu.

Mambo ya biashara,ushauli wa kibiashara, masoko na mifumo mingine ya kibiashara.

Hivyo nahitaji msaada wenu ni vitu Gani muhimu vya kufahamu na kuzingatia kwa watu nitakaokuwa nawafundisha.
Hii ni kali kabisa kabisa. Daktari anataka kumfanyia upasuaji mgonjwa lakini anaulizia ampasue namna gani? Nahurumia wanafunzi watakaojiunga kwenye hiyo ''trainning Centre'' yako. Kuandika kwenyewe maneno kwa kiswahili sahihi huwezi..
 
Kwanza wewe unamiliki makampuni mangapi na biashara gani ili uwe mfano?
 
Heshima yenu wana JFnataka kufungua business training centre kwa ajili ya kutoa mafunzo na semina ndogo ndogo za wajasilimali ambapo nitakuwa natoa mafunzo na semina kuhusu.

Mambo ya biashara, ushauri wa kibiashara, masoko na mifumo mingine ya kibiashara.

Hivyo nahitaji msaada wenu ni vitu gani muhimu vya kufahamu na kuzingatia kwa watu nitakaokuwa nawafundisha.

Hongera Mkuu kwa kutaka kuthubutu,

Key success factor or Critical success factor kwa biashara ya utoaji wa mafunzo ya kibiashara na ushauri wa kibiashara ni kuwekeza rasilimali zako katika kujifunza juzi za msingi za kibiashara...

Hizo juzi ni kama zifuatazo...

1. Ujuzi wa kuweka malengo..

Ukiwa na huu ujuzi utasaidia wafanyabiashara ambao wanafanya biashara lakini hawajui wanataka nini, wakipate lini, kwa kiasi gani. Ni vema kuwa na huu ujuzi.

2. Ujuzi wa kuweka mipango...

Ukiwa na huu ujuzi utasaidia wafanyabiashara katika uaandaji wa miongozo juu ya matumizi ya rasilimali muda, fedha na jitihada ili kufikia malengo. Ni vema kuwa na ujuzi wa kuweka mipango.

3. Ujuzi wa kuweka mikakati...

Utasaidia wafanyabiashara wasioelewa namna ya kuainisha maeneo ya kimkakati yanayoweza leta tija zaidi sokoni dhidi ya washindani. Ni vema kuwa na ujuzi huu.

4. Ujuzi wa kuchanganua soko...

Utamsaidia mfanyabiashara kubuni masoko, kuelewa ukubwa wa soko, kuongeza tija kiushindani, mauzo, usambazaji, n.k... Hili zoezi linafanywa kupitia tafiti.

5. Ujuzi wa kutunza kumbukumbu na usimamizi wa fedha.

Utawajengea uwezo wafanyabiashara wengi juu ya namna ya kuratibu mwenendo wa biashara yaani kujua kinagaubaga wapi biashara inatoka na wapi inaelekea bila kusahau kupunguza ufujaji wa fedha za biashara, kudhibiti matumizi na madeni ya biashara...

6. Ujuzi wa kuchanganua sekta,

Hakuna biashara isiyo na sekta, na kila sekta ina tabia zake, mahitaji yake na mwenendo wake.. Ukiwa na huu ujuzi utamsaidia mfanyabiashara kuona hatari na kuona fursa kirahisi sana... Hivyo ni vema kuwa na ujuzi huu maana kumshauri bodaboda si sawa na kumshauri mama ntilie au muuza vipodozi...

7. Ujuzi wa kusimamia rasilimali watu...

Hakuna biashara inaweza kukua bila rasilimali watu, hivyo wafanyabiashara wanahitaji majibu sahihi juu ya namna ya kudhibiti wafanyakazi wasio waadilifu na wasio wachapakazi ili kuleta tija zaidi katika biashara...

8. Ujuzi wa mawasiliano na ujuzi wa kutatua matatizo na ujuzi wa kudhibiti mazingira yanayoweza pelekea hatari kwa biashara.

To sum up..

Nakushauri Mkuu uzingatie kujinoa ktk hayo maeneo, na mafunzo yako yajikite katika kuwajengea uwezo ndugu zetu katika hayo maeneo.

Pia jifunze namna ya kuwatafuta hao wateja unaowalenga.

Nakutakia kila la kheri Mkuu.
 
Ajabu la kwanza la greate thinker mwishon mwa mwaka twentytwenty.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom