Bee Venom: Zao la Sumu ya Nyuki na uvunaji wake

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
374
509
Screenshot_20210912-071321~2.png

Nchini Tanzania ni kama maeneo mbalimbali barani Afrika, kumekuwa na ufugaji wa nyuki kwa ajili ya uvunaji wa mazao yake ili kujipatia fedha lakini bahati mbaya kumekuwa na uvunaji wa mazao machache huku mazao mengine yakiwa hayajulikani.

Kwa ufugaji wa kisasa Nyuki huvunwa mazao sita ambayo ni Asali (Honey), Nta (Wax), Chavua (Pollen), Gundi ya Nyuki (Propolis), maziwa ya nyuki (Royal Jelly) pamoja na Sumu ya nyuki (Bee Venom). Hapa katika makala haya, nitazungumzia zaidi uvunaji wa zao la Sumu ya Nyuki kwa kirefu ambao ninaufanya katika shamba langu (Nyuki Farming).
Ukweli zao hili halifahamiki sana kwa wafugaji wengi kutokana na kukosa maarifa ya uvunaji sambamba na mazao ya Asali na Nta ambayo yamezoeleka zaidi.

Sumu ya Nyuki huvunwa kwa wiki moja mara mbili yaani unapovuna mzinga moja siku moja hunauacha mpaka siku ya nne unarudia tena kuuvuna. Mfano ukivuna leo (Jumapili), unauacha mpaka Jumatano kisha Alhamisi unarudia kuvuna, wakati Asali huvunwa kwa mwaka mara mbili tu.

Sasa ili kuivuna sumu mfugaji hulazimika kuwa na mashine maalumu kwa ajili hiyo ambayo sehemu ya kifaa chake kiitwacho Plate hutegeshwa katika mlango wa mzinga au juu yake baada ya kuondoa mfuniko wa mzinga kuwashawishi nyuki kutoka kushambulia wakiamini ni adui hivyo kuacha sumu hiyo ambayo baadaye hukusanywa kwa utaratibu maalum na kuhifadhiwa tayari kwa kuuzwa.
Katika mzinga mmoja mfugaji anaweza kuvuna kiasi cha 0.20 hadi 0.85 ya gramu mmoja lakini ikitegemea ukubwa wa kundi la nyuki waliomo ndani yake na namna ya uvunaji.

Wakati Asali huuzwa kwa kipimo cha kilo moja (sawa na gramu 1,000), sumu huuzwa kwa kipimo cha gramu mmoja kwa zaidi ya bei ya asali.

Sumu ya Nyuki ni nini?
Sumu ya nyuki ni kemikali asili au tindikali isiyo na rangi, ambayo hutengenezwa na kuhifadhiwa ndani ya mwili wa nyuki na wao huitumia kwa kujilinda na maadui wao kwa kuwashambulia pale wanapohisi kuvamiwa.

Sumu hii hutolewa na nyuki kwa njia ya mwiba wake (Stingers) uliopo nyuma ya mwili wake wakati wanaposhambulia maadui baada ya kuvamiwa. Sumu hii inapoingia kwenye mwili wa adui husababisha maumivu makali kutokana na vichochezi ilivyonavyo
ambavyo ni Phospholipase A2, Enzyme na Allergen kuu ambayo husababisha huathiri kwa kushambulia seli za adui.

Hata hivyo kulingana na tafiti mbalimbali kiasi cha vichochezi vilivyomo ndani ya sumu licha ya kuwa na athari inayosababisha maumivu hasa kwa binadamu anapoumwa na nyuki, ilibainika vimekuwa mali ya faida kwa binadamu hivyo kuifanya sumu ya nyuki kuwa bidhaa muhimu kwa matumizi ya kibinadamu. Umuhimu huu pia umechochea kuongezeka kwa matumizi yake na hivyo
kuwalazimu watalaamu kubuni teknolojia ya kuvuna sumu hiyo.

Uvunaji wa Sumu hufanyikaje?:
Ili kuvuna sumu ni lazima mfugaji awe na mizinga ya nyuki yenye makundi makubwa na waliyokaa ama kuishi ndani yake muda mrefu walau isiwe chini ya miezi mitatu, awe na mashine ya kuvunia, chupa ya kutunzia pamoja na jokofu kwa ajili ya kuhifadhi sumu hiyo kabla ya kuiuza au kuipeleka sokoni. Sumu hii pamoja na kwamba hutolewa ikiwa kimiminika (Liquid) lakini inapovunwa huwa hutoka ikiwa unga (Powder) ambao unapaswa kutunzwa kwa makini kwa kuukinga na joto kali, mwanga wa jua na maji, hivyo sumu hii hutunzwa kwenye chupa maalumu isiyoruhusu mwanga wa jua na huihifadhi kwenye jokofu kwa muda ambao kusafirishwa au kupelekwa sokoni. Ikitunzwa vyema kwa kuzingatia utaratibu hukaa muda mrefu hata zaidi ya mwaka.

Sifa za Sumu ya Nyuki:
Mfugaji anapoivuna sumu hii anapaswa kuhakikisha inakuwa safi na alazima ajiepushe na kuichanganya na kitu chochote na ili kuweza kuiuza ni lazima iwe na rangi nyeupe au brownish. Sumu ikiwa na rangi nyeusi wala majimaji huwa imeharibika hivyo kupoteza sifa sokoni.

Matumizi ya Sumu ya Nyuki:
Hutumika katika tiba ya kuzuia magonjwa na maumivu (API Therapy), ingawa hivi karibuni imepata umaarufu zaidi, tiba ya sumu ya nyuki imekuwa ikitumika katika mazoea ya dawa za jadi kwa miaka mingi. Kwa sasa sumu hii hutayarishwa sindano za kinga za mwili kwa magonjwa ambazo zimekuwa zikisimamiwa na wataalamu wa huduma za afya na pia zimekuwa ikiongezwa katika utayarishaji wa bidhaa kama vile Moisturizers, Lotions na Lozenges ikiwa sehemu ya virutubisho na viboreshaji.

Unaweza kusoma moja ya makala zangu zingine hapa jamiiforums kama; Fahamu mbinu ya kugawa makundi ya nyuki uliyonayo kujaza mizinga mipya isiyo na nyuki

Utegaji Nyuki waingie kwenye mzinga

Wewe ni Guru
Nimekubali mkuu
Asante kwa maarifa haya
Kama unafanya hii shughuli pia utajua gharama zake, hebu tuchakachulie kwenye gharama za ufugaji na uendeshaji..
 
Wewe ni Guru
Nimekubali mkuu
Asante kwa maarifa haya
Kama unafanya hii shughuli pia utajua gharama zake, hebu tuchakachulie kwenye gharama za ufugaji na uendeshaji..
Hili swali wengi huuliza, siwezi kukupa jibu la moja kwa moja sababu kuna mahitaji itakubidi uyajue katika eneo lako yana gharama gani ndiyo yakupe gharama halisi. Mfano;
1. Utafugia mstuni au shambani, sasa kama ni msitu au shamba utanunua kiasi gani au utahitaji kibali.

2. Aina ya mizinga ambayo utafugia itakugharimu kiasi gani kwa kila mmoja. Maana mbao zinatofautiana bei eneo hadi eneo.
Unaweza kuanza na mizinga mingapi ili ujue gharama ya mizinga husika.

Binafsi huwa nawashauri kwanza kuanza na kujifunza, ili wafanye ufugaji anaojua ajue aina za mizinga na kutengeneza pia au kuwatega nyuki waingie.

Sasa ili ujue unaweza kuwekeza Kwa kiasi gani fanya hivi:
1. Bei ya eneo unalotaka kufugia.
2. Mizinga Sh 170,000 X 50=
3. Ujenzi wa kibanda (unaweza kuiweka katika miti)
4. Vifaa kama;
Bee suite 2X 150,000
Smoker Sh 50,000
Chujii Sh 60,000
Brash ya Nyuki Sh 20,000
Batasi Sh 20,000
Gambuti Sh 20,000

Kwa kifupi siwezi kuiweka gharama halisi hapa zikamfaa kila mmoja lakini nimekupa picha ndogo ikusaidie kuelewa. Na gharama zinapanda zaidi kulingana na mamna unavyotaka kuwekeza au kuanza mradi.

Gharama za uendeshaji itategemea umbali wa eneo la mradi na Aina ya ukaguzi unayofanya na kama ni wewe au utamuweka mtalaamu akufanyie.

Ila ukitupa kazi ya kukuchambulia na gharama zako binafsi na eneo unalotaka tunaweza kukuandalia kwa uzuri zaidi ikiwa ni pamoja na kukushauri mbinu za kuanza nazo kulingana na mtaji ulio nao.
 
Nimeulizwa sana swali hili DM, sasa naweka video hiiitasaidia kujibu wengi. Tunapovuna sumu tunahakikisha mwiba wake hautoki kama ambavyo akiuma binadamu mwiba unatoka na kubakia hivyo huingiza hewa ndani ya tumbo na baadaye Nyuki hufariki.

Lakini Plate ya mashine hii, inakioo bacho Nyuki akiuma mwiba hautoboi hivyo humwaga sumu ambayo hugandishwa na umeme na kuitoa kwa kukwangua kama inavyonekena hapa kwenye video, ikitoka ikiwa unga.
 
Mkuu fred leo nimenufaika sana na nyuzi zako zenye elimu kuhusiana mzee nyuki, swali kwako kuhusu uvunaji wa hiyo sumu je mashine na vifaa vya kuhifadhia hiyo sumu vinapatikana wapi? Na kwa bei gani.
 
Up
Mkuu fred leo nimenufaika sana na nyuzi zako zenye elimu kuhusiana mzee nyuki, swali kwako kuhusu uvunaji wa hiyo sumu je mashine na vifaa vya kuhifadhia hiyo sumu vinapatikana wapi? na kwa bei gani.
Upatikanaji upo mara mbili, zipo mashine za Ulaya ambazo unaweza kununua online na zile zinazotengenezwa hapa kwetu.

Nitaangalia contay zao wauzaji wa hapa naweza kusaidia.
 
Kwa muda mrefu nilikuwa nikishauriwa kuanzisha darasa la uvunaji sumu ya nyuki, sasa nawataarifu rasmi tunaanzisha darasa hili kuanzia mwezi Machi 2022 kwa wafugaji Nyuki wenye uhitaji na watakaopenda kujifunza.
 
Mkuu mimi nina maswali yafuatayo

1. Bei ya hiyo sumu ni kiasi gani?

2. Unahitaji kuvuna kwnye mizinga mingapi ila kufikisha kilo moja?

3. Ukivuna sumu, bado nyuki wanatengeneza asali kama kawaida au ndio imetoka?

4. Sumu ya nyuki ikiingia mwilini kwa wingi inaua, vipi unasema watu wanachomwa sindano ya sumu hiyo?

5. Soko liko wapi?

Naomba unijibu hayo kwanza
 
Asante kwa maswali Aziza, naomba kujibu;

1. Kuhusu Bei; Sumu ya Nyuki inauzwa kwa gram, hivyo mpaka sasa 1gram ni Tsh 20,000/ hadi Tsh 35,000/ kwa soko letu la ndani.

2. Mzinga mingapi inakupa kilo moja; Kilo moja ni Sawa na gram 1,000 kiasi hiki ni kikubwa sana. Kwa kawaida Mzinga mmoja wenye Nyuki wengi au kundi kubwa lililostawi vyema likivunwa mara moja linapaswa kukupa 0.80gram hivyo ili ufikishe gram 1 tu unahitaji kuwa na mizinga 6-7 hivi.
Hivyo basi ukiwa na mizinga 100 ukavuna mara 2 Kwa wiki utaoata wastani wa gram 20 hivyo wiki 4 (mwezi) utakuwa na gram 80 au zaidi.
Mizinga 100 inaweza kukupa gram 80 Kwa mwezi hesabu ni 80X20,000=1,600,000/

Angalizo haya ni makadilio yanaweza kuwa Chini ya hapo au zaidi Kwa vile itategemea ubora wa makundi yako ya Nyuki na mahalo unapofugia.

3. Ukivuna sumu unaweza kuvuna asali? Ndiyo inawezekana lakini unapaswa kuvuna Kwa kuzingati utalaamu na kipimo cha muda wa kuvuna (hapa lazima ufundishwe) kisha utavuna na asali.
Ukivuna holela utaoata sumu bila asali.

4. Sumu ya Nyuki ikiingia mwili kiasi kingi inaweza kusababisha kifo. Watalaam wanasema zaigi mil 900 Kwa mtu mwenye uzito wa kg 32 anaweza kufariki, Chini ya hapo atapata taabu Sana. Sasa mil 900 ni Sawa na sumu ya Nyuki 1500-1900.
5. Soko liko wapi? Kuna masoko aina mbili lipo soko la ndani ambalo nimekutania bei na soko la nje ambalo pia linapatikana bila Shaka.
 
boss haya madini unayotoa ni ya hatari, hii ndiyo raha ya kutoa mada ukiwa na uzoefu wa field. Boss naomba kuuliza maswali kadhaa..
Hivi langstroth na top bar beehives ni ipi unashauri mtu kutumia kwa commercial bee keeping? mzinga mmoja unaweza pata pollen kiasi gani uki trap kwa mwezi mzima? ekari moja inachukua mizinga mingapi kwa modern apiary ambayo unaweka kwenye vibanda?,
 
Asante kwa maswali haya ambayo nimeyatenga kama ifuatavyo:
1. Mizinga aina ya Langstroth na Top bar ni ipi unashauri mtu kutumia kwa commercial bee keeping?

JIBU: tumia Langstroth, lakini hakikisha ukiwa na Kikinga Malkia (Queen Excluder) na siyo wavu ule wa madirisha kama wanavyoweka wengine. Faida ya Kikinga Malkia ninkuoa mavuno zaidi.

2. Mzinga mmoja unaweza pata Pollen kiasi gani uki trap kwa mwezi mzima?

JIBU: Hakuna jibu la moja kwa moja unaweza kulipata kwa anayefuga na kuwatambua nyuki, mengine yanayosemwa makisio tu, sababu upatilanaji wake inategemea uwezo (Nyuki) kuzalisha/ kukusanya chakula ndani ya Mzinga wao. Kumbuka uzalishaji wao hata Kwa asali hutegemea ukubwa wa kundi Lao, Uchapakazi wao na upatikanaji wa malisho (maua ambayo huwapa Pollen). Vivyo hivyo katika uzalishaji asali.
3. Ekari moja inachukua mizinga mingapi kwa modern apiary ambayo unaweka kwenye vibanda?,

JIBU: Ekari moja ukitaka unaweza kujenga Kibanda hata cha mizinga 100+ lakini, lazima uzingatie uwepo wa malisho kwenye eneo hilo Hadi eneo jirani na Ekari moja yako.
Ukifanya uhakiki na kubaini malisho yapo ya kutosha unaweza kuweka hata zaidi ya mizinga hiyo.

Hata hivyo IPO kanuni ya kitalaamu ambayo inabainisha kukiwa na miembe mingapi au miti na maua kulingana na uwezo wake wa uzalishaji Pollen unaweza kukuongiza kuwekanidadi ya Mzinga.
Niwe radhi hapa siwezi udadavua kwa kina sababu ni somo pana ambalo litatubidi kuangalia aina za miti au maua na uwezo wake wa kuzalisha pollen hivyo kukupa mwongozo ya idadi ya mizinga inayofaa kufungwa.
 
kaka I salute you, usichoke kutupa madini uliyonayo. nitakutafuta baada ya muda kwa kuwa hii kitu niliianza miaka 5 iliyopita ila nilikuwa bado najifunza.. sasa nafikiria kupiga modern apiculture.
 
Mkuu fred leo nimenufaika sana na nyuzi zako zenye elimu kuhusiana mzee nyuki, swali kwako kuhusu uvunaji wa hiyo sumu je mashine na vifaa vya kuhifadhia hiyo sumu vinapatikana wapi? Na kwa bei gani.
Wapigie Tanzania International Bee 0744344488
 
Mkuu kati ya royal jelly na hiyo sumu ni koi rahisi kuvuna kama utakuwa na mizinga zaidi ya 500?
 
Back
Top Bottom