Nataka kufuga kuku wa kisasa sehemu ambayo hamna umeme nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kufuga kuku wa kisasa sehemu ambayo hamna umeme nifanyeje?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by guta2010, Jun 6, 2011.

 1. g

  guta2010 Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshema wana JF,nataka kufuga kuku wa kisasa lakini sehemu nayotaka kwenda kufugia umeme haujafika bado naombeni njia nyengine ya kusolve tatizo la umeme.
   
 2. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Aidha nunua jenereta ama wekeza kwenye solar panels, tatizo ninaloliona ni kwa kutumia generator profit margin ni ndogo ama pengine utapata hasara kabisa kutokana na gharama za diesel/petroli
  Kama mradi wako ni mkubwa nahisi Solar panels inaweza kukupatia faida ila sio ya harakaharaka pengine baada ya miaka 2 ama zaidi.
   
 3. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  ASANTE NDUGU GUTA.Mimi nilikuwa mfugaji wa kuku wa mayai na nyama.Unaweza kufuga bila umeme na mambo yakaenda kama kawaida.Zingatia nitakavyo kuelekeza.Kwanza unapopa vifaranga uviangalie kama vimejikunyata ndo unawasha chemri.Mara nyingi inakuwa wakati wa asubuhi.Ikishafika mchana unazima taa unaacha wapate mwanga wa jua kwa joto likizid ni hatari.Pia kama joto ni dogo unaweza kuwasha jiko la mkaa na ukaliweka kwenye kona unayofugia mpaka uone vifaranga vimechangamka.Kwa kuku wa mayai hakikisha wanalala na taa mpaka wafikishe miezi miwili kwa usalama zaidi.Lakini wakishachangamka ndani ya mwezi mmoja uwe unawazimia taa mchana na usiku unawasha mpaka miezi miwili itimie.Kama una maulizo tuwasiliane ili nikutumie maelezo yanayoelekeza ufugaji bora wa kuku aina zote.KWA SASA NIPO DAR KWA MWANA JF MWENZETU KUNA BIASHARA TUNAFANYA HIVYO KAMA UNAWEZA KUONA NI VIZURI NIKAKUPA MAELEZO KWA KINA.USIOGOPE KUULIZA USIPOELEWA.
  Asante.
   
 4. g

  guta2010 Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Tizo asante sana ata sisi tupo Dar,tunataka kufuga kuku so tunaweza kukuonaje tupate hizo detail info.
   
Loading...