Nataka kuacha kazi

Nataka kuacha kazi

House of Commons

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2013
Posts
2,189
Reaction score
2,206
Wasalam wapendwa

Si kwamba nimechanganyikiwa, hapana. Naona kama nachelewa kutimiza malengo yangu na kazi niliyo nayo ni ya kuajiriwa na ofisi zake ni vijijini. Kwa miaka 10 nimekekuwa nikisafiri kutoka ninakoishi (naishi moja ya jiji hapa nchini) kwenda ofisini. Zifuatazo ni hasara na changamoto ninazoziona kwenye ajira hii

1 Nina shughuli zangu mbadala (miradi) huko jijini, kila wiki 1 au 2 lazima nione maendeleo yake, hii hunigharimu sana kifedha kiasi cha Tshs 80,000 hadi 100,000 kwa mwezi.

2 kipato changu kinachotokana na ajira si kikubwa sana ukilinganisha na shughuli binafsi nilizonazo

3. Shugughuli za ofisi zina nature ya kumlazimisha mwajiriwa kufanya kazi mchana, usiku hadi weekend (sometimes) bila overtime au incentives in turn

4 Sipendi kuhamishia familia huko kazini kwangu maana nitaongeza gharama za maisha na kupoteza dira na malengo yangu

5 Sioni kama ajira rasmi itanipa kipato thabiti kabla ya umri wangu wa uzeeni

6 Nataka kutumia Elimu yangu ya " shahada ya udhamili ya usimamizi wa miradi" kuendeleza miradi yangu binafsi

7 Naona kama utumwa fulani kuwa mwajiriwa, hii inanifanya au niwe mtoro kazini au ku Underform kazini kwangu

Kwa sasa bado naendelea, ila miradi yangu itakapokuwa na thamani ya 300mil nita resign with good will, na hili nitalifanya ndani ya miezi 18 ijayo kuanzia leo.

Just to share with you friends, you can advise otherwise, maana haya maisha nayo hubadirika, nipe uzoefu na mawazo yako tafadhari...
 
kama umeona miradi yako ipo imara, na inakuingizia kipato kizuri unaweza kufanya maamuz yoyote yenye manufaa kwa upande wako
 
kama kwenye miradi yako binafsi unapata faida zaid ya.ulikoajiriwa ni bora ujiajiri kwani kujiajiri ndo mpango mzima...ngoja nishee kauzoefu..nilipomaliza chuo just bachelor nilijaribu kutafuta kaz...wakat huo nilikua na biashara zangu tu ila nlitaka kufanya kaz nikiamini baada ya muda nitaacha na kuongeza.mtaji wangu...niliishia kupata kaz za.muda yaan part.time kusimamia miradi kwa miez 3 mpaka wiki kadhaa na kipato kikiwa elfu 20 kwa mpaka 25 kwa siku...hapo nilikua nafanya kaz bila muda maalum mpaka masaa 13 unafanya kaz...duuu nilivumilia nikiamini nakuza mtaji..kumbe ilikua utumwa tu hiyo hela nliyokua napata kwa siku ni zaid ya mara tano ya faida ninayopata kwenye biashara zangu nikaamua kujiajiri moja kwa moja na kuelekeza nguvu zangu kwenye kujiajiri na sasa maisha yangu yapo safi napiga hela vizuri tena kwa uhuru mkubwa kuliko ningeajiriwa hata mtu akiniambia kuna kazi mahali ya mil kwa mwez sifanyii...

Nakushauri ndugu yangu kaka yangu ni heri ujiajiri maana huwez kuyafikia malengo yako kwa kutegemea mshahara tu otherwise uwe unalipwa dola 1500 kwenda juu na marupurupu hapo unaweza kutoka maana unaweza kupata mtaji kwa haraka otherwise quit the job and continue with ur own bussness!
 
Salute!..thanks for recognition, noted...
 
kama umeona miradi yako ipo imara, na inakuingizia kipato kizuri unaweza kufanya maamuz yoyote yenye manufaa kwa upande wako

Yes, lakini kuna mahali naona ni bora tu nifanye hivo, time value nayo ni factor..
 
jiamini ndugu, maisha bila kuajiliwa yanawezekana,niko kwenye njia hiyo pia, nimewekeza milioni nane kwenye vimiradi vidogo vidogo,lengo likiwa ni kuzalisha 25milioni ambazo ntaaziingiza kwenye project kubwa zaidi, nikifanikiwa naresign,
 
Yes, lakini kuna mahali naona ni bora tu nifanye hivo, time value nayo ni factor..

Ni jambo jema sana kuamua kujiajiri.
Ushauri wangu ni huu, angalia miradi yako unayoitegemea kama imejengwa ktk misingi imara ya kuhimili ushindani wa mitaji ya wengine,kuna miradi mingine inaingiza fedha za chap chap lakini ikipita misuko suko kidogo tu, mradi chali.

Uoga ni dhambi, choma meli tukutane ng`ambo ya ziwa.
 
Hakika mkuu, let us strugle
jiamini ndugu, maisha bila kuajiliwa yanawezekana,niko kwenye njia hiyo pia, nimewekeza milioni nane kwenye vimiradi vidogo vidogo,lengo likiwa ni kuzalisha 25milioni ambazo ntaaziingiza kwenye project kubwa zaidi, nikifanikiwa naresign,
 
Umenitia moyo sana, nitathubutu, si kwa kujarib lakini kudhamilia na kusonga mbele

Ni jambo jema sana kuamua kujiajiri.
Ushauri wangu ni huu, angalia miradi yako unayoitegemea kama imejengwa ktk misingi imara ya kuhimili ushindani wa mitaji ya wengine,kuna miradi mingine inaingiza fedha za chap chap lakini ikipita misuko suko kidogo tu, mradi chali.

Uoga ni dhambi, choma meli tukutane ng`ambo ya ziwa.
 
inawezekana mkuu maisha bila kuajiriwa.kuajiriwa ni utumwa na uoga wa maisha unakuta mtu kaajiriwa kipato ni kidogo lakin bado anaendelea kuitumikia hiyo ajira ni uoga tu.choma moto meli mkuu weng tupo nyuma yako kukufuata ngoja tujipange mkuu.
 
cc_wall09084_1024.jpg
 
Kuna wakati unafika inakubidi ufanye maamuzi magumu, tunapoishi hapa duniani tunatakiwa tuwe na focus...Mimi mdada niliamua kufanya maamuzi magumu na kuamua kuacha kazi yangu ya ualimu wa Sekondari niliyoajiriwa na serikali huko vijijini mkoani Tanga kwani kipato nlichokuwa nakipata, ukiunganisha na mazingira na uwezekano wa kuendelea kifikra na kimaisha kiujumla ilinifanya nitake opportunity cost mara tu baada ya kupata kazi hapa Dar kwenye Kampuni binafsi ingawaje mshahara sio mkubwa na wala sio mdogo ila naamini ni mwanzo wa kupata kazi nzuri zaidi..Nia na madhumuni ni kupata chance ya kupata pesa nyingi nije kuwa mjasiliamali kubwa hapa mjini na kupanuka kimawazo....Maisha ni malengo usipokuwa na malengo huwezi kuendelea kamwe....Kwa iyo mimi nakushauri shauriana na Halmashauri yako ya kichwa na kumshirikisha Mungu then come up with the right decision, usiwe muoga hakuna kitu kigumu kama una nia na malengo...KILA LA HERI.
 
Unafikiria mtaji wa mil 300? Niliacha kazi kwa mtaji wa laki 7 tena hii ni pension yangu kwa miezi saba nlofanya. Nlihustle kukuza mtaji wangu. Na sasa mambo fresh. Hakuna kitu kizuri kwangu kama kuwa na uhuru na amani katika kufanya mambo yako.
Kazi nlokuwa nafanya ni torture na kufanya kazi had jmosi ndo ilikuwa msala.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Back
Top Bottom