Natafuta wimbo wa Bungeni Kariakoo

valour

Senior Member
Aug 3, 2010
168
71
Wana JF,

Asubuhi hii wakati nakuja ofisini, nimesikia wimbo mpya kwenye radio clouds, unaoitwa Bungeni Kariakoo, ukimnukuu Spika Makinda akimwagiza Mh. Wenge kufuta kauli yake akiwa anakataa, wabunge wa CCM kumwambia atoke na Mh. Zitto kumtetea kuwa asitoke ndipo zogo likaanza. Na hivi karibuni kauli ya Mh. Kafulila kusema kuwa serikali ni legelege na kuamriwa afute kauli naye kukataa na zogo likaanza tena. Kwa kweli mwimbo unafundisha sana na pengine wabunge wakiusikia watajirekebisha na kuachana na ushabiki usio na tija.

Atakayeusikia aniambie unapatikana wapi. Shukrani!
 
aiseee huyu jamaa noma nimem sikia clouds leo naomba ukipata tugaiane jamani yaani tungepata kama hawa watatu yaani hii ilitakiwa iitwe
mmmh sisemi
 
Unapatikana apo hapo Clouds. Nami niko njiani kuelekea Clouds kujipatia copy zangu (LAKINI WANITHIBITIHIE KUWA MWENYE NAKALA HALALI YA WIMBO AMESHIRIKISHWA KATIKA DILI)
 
Pia wandugu naomba mwenye wimbo wa Roma inaitwa Mathematics auweke hapa plz nautafuta vibaya mno
 
Sizinga nausubiri kwa hamu. Hata chai sinywi hadi niupate. Natanguliza shukrani za dhati japo mie siye niliyeuomba kiherehere changu tu hiki

haya ndugu nimesha-upload, gonga hiyo link sikiliza, ukiweza download
 
Nitauingiza kwenye list ya nyimbo zangu kwenye kampeni nitakapoenda Jimboni na nyingine nyingi....vipaji hivi! Ujumbe umefikishwa vizuri
 
Nitauingiza kwenye list ya nyimbo zangu kwenye kampeni nitakapoenda Jimboni na nyingine nyingi....vipaji hivi! Ujumbe umefikishwa vizuri
sikufichi mr ben natami nikuone ukiwa bungeni !ingawa sijawahi kukuona ,ila unaonyesha wewe ni tingatinga !
 
Huu wimbo unacheza vizuri kwa VLC...so listen it, nimeupload thru eastafrcantube

Bungeni Kariakoo!!

isee asante sana, huu wimbo umeniacha hoi sana, kweli bungeni kama vile Kariakoo kila mtu anawasha MIC yake... bunge linaitaji kuendeshwa na mtu independent ambaye haelemei upande wowote, sijui kama inawezekana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom