Natafuta Wachezaji Kuja Kucheza Europe

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,138
3,208
Natafuta wachezaji kutoka afrika hasa watanzania kuja kujaribu soka hapa.

Uwezekano wa kupata timu ni mkubwa kama yeye ni mchezaji maana atajaribiwa ktk timu nyingi na za daraja tofauti.

Asiwe na umri unaozidi miaka 23.

Awe na uwezo wa kujigharamia Ticket

Maradhi na chakula akiwa hapa yatafanywa na kampuni.
Mwariko atatumiwa na kampuni wa kuja kujaribu soka hapa

Kwa vile tz haiifahamiki kisoka tutahitaji wachezaji wa mwanzo wawe wanasakata kabumbu kisawasawa ili wapeperushe jina .
pia unaweza tembelea ktk web yetu .
www.nowakconsulting.pl

Nitwangie sms +48697461457 andika jina lako na klabu unayocheza mimi nitakutwangia simu moja kwa moja.
Ama nitwangie Email mkamap@yahoo.com ama uni PM ukibainisha namba yako ya simu.

ustaraabu Nimatumaini yangu hatuta ABUSE mawasiiano .Na ni mategeo yangu ujumbe tutawafikishia wahusika .
Otherwise ON PEACE !!!! C U then.
 
Mwanatanu hiyo namba ni ya Poland! Sweden huanza na +46...
Hii ni news nzuri sana,Shukurani kubwa kama utaweza kusaidia vijana wetu...Hongera SanaHio lugha ya kipolish na bongo wapi na wapi?Web site----Polish
Simu-----Sweden....mhmhmhmh!!!!!!!!!
 
Mkamap,
Mkuu wewe mkali nimekuvulia kofia. Kitu kimoja tu usije jaribu kuwa agent ukawafunga watu kamba. Kuwa na uhakika na kile unachosema kwani wapo wanaowatumia ndugu zetu kama watumwa Ulaya kuuza vinyago barabarani baada ya kuchukuliwa kama wachezaji.
Nakuomba tu wasiliana na Balozi wetu ili upate msaada zaidi.
 
Jamani wachezaji wetu wa tz hasa youngs wanaohitajika...sidhani kama wanapita pita humu....naomba wadau wa print na wasogeze karibu nao.....ili wajiandae kujitafutia zali hilo huwezi jua..........vijana tunao wengi sana sana ...ingawa napata wasiwasi na nauli.....return ticket itasumbua sana......
 
Mkamap,
Mkuu wewe mkali nimekuvulia kofia. Kitu kimoja tu usije jaribu kuwa agent ukawafunga watu kamba. Kuwa na uhakika na kile unachosema kwani wapo wanaowatumia ndugu zetu kama watumwa Ulaya kuuza vinyago barabarani baada ya kuchukuliwa kama wachezaji.
Nakuomba tu wasiliana na Balozi wetu ili upate msaada zaidi.

Kuondoa maswali na shaka tafuta viongozi wa kabumbuTanzania ambao watakutafutia watanzania wanaofaa ambao hawawezi kuona hili Tangazo.Kusema upigiwe simu na kuandika barua pepe mwitikio unaweza kuwa hafifu kwa maana ya kwamba mtu halisi hujulikani,Na pia hilo la kwenda Ulaya unaweza kupata hata mabomu maana wengi wataona wameukata.
 
Nashukuru kwa maelezo yako.
Hizo process nimezipitia nimepiga simu kwa wenyekiti wa vilabu kadhaa ,lakini naona wanajikongoja sana sijui tatizo nini?

kuhusu simu mimi nahitaji namba zao za simu mimi ndio nitawapigia.

Hakuna wakuuza vinyago maana mimi pia ni mdau ktk kampuni hii ni mimi ndio nimewashawishi tuchukue Tanzania kampuni kwa ujumla ilitaka Kameruni ama Nigeria.

Nauli hatuwezi kwa sababu zifuatazo.
1.Hatujaingia nao mikataba tukiwapa nauli wakajiripua kwingine sisi hasara tupu.
2.kuna minigeria/kameruni/senegal ambao wao kwanza wanajulikana pili kwa gharama yoyote wao wako radhi kusafiri kuja.

Sasa basi wabongo nasisi tuchakarike waje si tusubiri kutafuniwa sisi tumeze tu .
Naomba wafikishieni habari hii mwenye uwezo huo asanteni.
 
Mkamap,
Mkuu wewe mkali nimekuvulia kofia. Kitu kimoja tu usije jaribu kuwa agent ukawafunga watu kamba. Kuwa na uhakika na kile unachosema kwani wapo wanaowatumia ndugu zetu kama watumwa Ulaya kuuza vinyago barabarani baada ya kuchukuliwa kama wachezaji.
Nakuomba tu wasiliana na Balozi wetu ili upate msaada zaidi.

Mkuu mkandala
siwezi funga kamba mtu
Hapa ulaya sio kama bongo hakuna longolongo
kampuni imesajiriwa na akitaka tutamtumia agreements huko huko inamaana tukimuuzisha vinyago atupeleke polisi.

Tatizo ambalo wengi linawakuta ni kua wakishafika ulaya wanapagawa hawafiki ktk destinations zao badala yake wanajiripua ndio wanajikuta wanauza machungwa ktk hilo hatutahusika na ndio maana kwa vile saizi kuna kitu kinaitwa SHENGEN hatutoi Nauli.
 
Jamani kwa wale wenye ndugu wanao sakata kabumbu chance hiyo si mmeiona?kwa hiyo kazi kwenu jaribuni kuitumia ipasavyo kazi kwenu........
 
Hii itakuwa agency uchwara, kwanini if you really mean business msiwalipie watu nauli?Ninavyojua mimi serious agents wao ndio wanasafiri wenyewe nchi mbalimbali kufanya scouting au wanakuwa na representatives, mpaka mtu akubaiwe kupanda ndege anakuwa uwezo wake ushajulikana. Sitashangaa kama mtu atajikokota na kinauli chake halafu akifika huko kama hafikii kiwango mkatelekeza akaanza kulala mitaani na kula majalalani. If you are serious with this bro, tuwekee copy ya mkataba wako hapa tuupitie ili hao trialists wajue what to expect, usije ukawa umetumwa na watu wenye mashamba yao wanaotafuta cheap labour hapa.
 
Mkamap,

Kama alivyogusia KKN, pengine ingekuwa idea mzuri kama wewe na partner(s) wako mngefunga safari Bongo kwenda kuwasiliana ana kwa ana na vyombo (timu) vya soccer, pamoja na wachezaji.

Kuonyesha u-seriousness wa nia yenu, mngetakiwa muandae kitu kama seminars kwa wachezaji na wakufunzi wa soka bongo. Ni kwenye seminars hizo ndio mngepata nafasi ya ku-pitch ideas zenu. Naamini tactic hii ingesaidia ku-establish credibility na hence chance ya ku-recruit talented players.

Plus, kwa kufunga safari kwenda bongo, mnapata nafasi ya kuchagua wenyewe the really talented players na sio wababaishaji.
 
Balali hakukosea watanzania wavivu wakufikiri.
 
Nakuelewa mkuu na natambua unalosema

Hayo mambo ya seminar ni jukumu la TFF na sio kwamba kampuni inawategemea wachezaji kutoka TZ ila nilionelea nichukua watanzania wezangu Maana wamekua wakihaha na timu ya taifa kutafuta timu.

All in all NABII HAKUBALIKI KWAO nikijaza wanaigeria ,wakongo na wakenya lazima watanzania wazangu mnaohoji leo mtageuka nakusema watanzania tunabaniana.
 
Mimi wasi wasi ni kuwapata hao vijana wenye umri mdogo hivyo....na pia wao kupata nauli za returns kwenda huko ulaya ambapo ni kama 1.2m au zaidi...wajua kwa maisha yetu uswazi sio kidogo hizo ati....oohh....mi nashauri kama ukija na uka attach na TFF wakatangaza media zote..ukaomba makocha wakusaidie kutafuta na kuchuja vijana....then ukiwapata una wapa form wanajaza particulars zao zote......wanajiandaa kutafuta nauli na passport .......wanakuja kujaribu ila vinginevyoo holaaaaaaa.............
 
All in all NABII HAKUBALIKI KWAO nikijaza wanaigeria ,wakongo na wakenya lazima watanzania wazangu mnaohoji leo mtageuka nakusema watanzania tunabaniana.

LoL.... Sasa si ndio utakuwa mchango wako wa kuinua soka la nyumbani. Wala usijali na maneno ya kukatishana tamaa mzee, binafsi naamini nia yako ni mzuri kabisa. Kwa sababu, unaweza kutengeneza hela mzuri tu kwa kuwakusanya Nigerians and Co, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba kwa kuwapa nafasi wachezaji wa Kibongo, sio tu utatengeneza hela, bali pia utajivunia wanapofanikiwa.

Ni kweli suala la seminars ni wajibu wa TFF. Lakini kwa sababu nia yako ni zaidi ya kutengeneza hela, haitaumiza kama ukienda extra miles katika kutoa mchango wa kuwainua wachezaji wetu. Kwa mtazamo wangu, pengine bado unaweza kushirikiana na TFF kufanya hizo seminars. In the end, unajua kuwa pindi wachezaji watapofanikiwa, na wewe utafanikiwa katika kila hali. Ni malengo ya muda mrefu tu.
 
.

ndio mkuu mimi nimekuelewa.
tatizo letu sisi wabongo kila mmoja amegeuka kua mwanasiasa mimi nimeomba contact za wachezaji lakini mtu anajitahidi kuligeuza kua siasa.

Naomba simu
1.Mrisho Ngassa
2.uhuru suleiman
Mwenye nazo anipatie
 
Vipi umewasilina na TFF ?
Nafikiri wanaweza kukusaidia
 
Hapa ndiyo wachezaji wasiotaka kuingia katika mtandao na forums kama hii ya jamii wanapokosa opportunity kama hizi. Bahati mbaya ninaowajua ni aged na hawana uwezo wa kusakata kabumbu huko. Shida ya vijana wetu wakishachezea Yanga na Simba tu basi wanadhani mpira unaishia hapo hawafanyi jitihada za makusudi kujiendeleza zaidi katika soka. We waangalie tu utashangaa, maana hata kama alikuwa anasoma shule ujue hapo ndiyo mwisho. Sijui tumelogwa?
 
Balali hakukosea watanzania wavivu wakufikiri.

Ni kweli kabisa na wewe ni mmoja wa mifano hai, ni wazi umekurupuka kuweka hili tangazo hapa, hukufikiri. Kuna issues nyingi ambazo ungeweza kuzifine tune kabla ya kuanza kuutangazia ulimwengu kile unachotaka kufanya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom