ndio mkuu na umesikika watanzania wamekusikia na wamekuelewa .
Mimi ninachoweza kusema ni kua Hakuna docomenti ya kiingereza,kiswahili ,kijerumani,kichina,kijapani ama lugha yoyote tofauti na polish inayowezwa sainiwa na mahakama nchini hapa.
wala hakuna mwanasheria hapa anaye process dokomenti za lugha za kimataifa yani kiingereza ,kifaransa na kispanish na zinginezo tofauti na polish.
Ukiona watu wanaoparamia lugha za watu ni sisi tu waafrika ndio utakuta tunatoka kifua mbele na lugha za watu kwa bahati mbaya sana hawa watu WEUPE wanapenda vyao.
Mkamap,
Naona hapo juu hauko sahihi. Kwasasa Poland iko EU, wana wajibu wa kutafsiri documents zote muhimu kwenye lugha mbalimbali za EU.
Ndio maana hata hizi nchi zingine kwasasa zinatafsiri documents mbalimbali kupeleka kwenye
lugha za wananchama wapya wa EU.
Kuna Wapolish wengi sana sasa wamepata kazi za maana kwenye eno hilo la lugha ili kutimiza masharti ya EU.
Kwa mawazo yako hata Bush akija Poland,basi makualiano wanasaini kwa kipolish?