Nimerejea
Bado tunapishana hapo kwenye dini na ukweli... Labda utumie neno 'dini yangu' hapo naweza kukuelewa, lakini shida itakuja moja pale utakapodhani ya kuwa dini yako ndio imani ya 'kweli' na ndio sahihi
Katika usanifu wa lugha na kumjua mtu,kuna kauli mtu akiitumia hufidisha maana nyingine na huweza baadhi ya muda ukaondosha tamko kabisa,na ukajua hapa anakusudia nini au linakusudiwa nini,mfano "naenda kuoga maji" hii kauli si fasaha sababu ulitakiwa uondoshe tamko "maji" sababu kawaida mtu akienda kuoga ujue kabisa anaenda kuoga maji. Mimi ninapo ongelea dini ujue ni dini yangu mimi.
Hiyi unayo isema shida si shida endapo ukiwa mkweli na una hoja na ubainifu,sijui huwa mnaogopa wapi ? Au labda hamjui nguvu ya ukweli ilivyo. Mimi kwa jinsi nilivyo naweza kujadiliana na yeyote maadamu nina hoja na ubainifu.
Tukirudi kwako kama ulivyo bainisha huko nyuma ya kuwa uliweka vigezo vyako vya kuona jambo fulani ni sawa,sasa tukienda mbali tunatakiwa tuhakiki tunayo yaamini au kuyaegemea maadamu mizani ipo. Sasa mnapoleta kisingizio hiki mnaonekana hamuwezi kukosoa kile ambacho mtu yuko dhidi yako,na hili linaonyesha udhaifu wa unacho ona unakijua.
Imani ni jambo la kiroho zaidi na ni jambo la kuaminishwa zaidi kuliko kuhoji na kupata ithibati.. Lakini dunia haina imani moja wala dini moja na karibia kila mmoja anadhani kuwa dini na imani yake ndio sahihi kuliko za wengine
Hii siyo kweli,huwezi kuitenganisha imani na matendo imani na uhalisia. Huu mtazamo si wa kweli na unaonyesha ya kuwa kuna mambo huyajui mengi kuhusu imani. Mathalani mimi katika imani yetu,tumetunukiwa elimu ya uhakiki wa habari hasa za mtume na nyingine kwa ujumla,elimu hii kiistilahi inaitwa "Mustwalahul Hadithi", ukitaka kujua kuna miujiza katika elimu basi ni elimu hii. Elimu hii kuhoji na utafiti ndiyo msingi mama wa elimu hii. Lakini kadhalika Mola wetu anatutaka tuhoji mno na kifikiria mno. Sasa unaposema imani ni jambo la kuaminishwa hakuna kuhoji hakuna ithibati wewe unakuwa Muongo,labda uainishe mathalani Imani fulani wao hufata mambo kichwa mchunga,lakini si imani zote hasa imani yangu.
Sahihi kabisa kuna imani nyingi na dini nyingi kadhalika,lakini akili ya kawaida tu inakataa ya kuwa imani zote hizo na dini zote hizo kwamba ziko sahihi zote. Haya ni matumizi mabaya ya akili na ni kujidanganya kuliko pea zaidi.
Mathalani mimi nina uwezo wa kutoka mbele na kujifaragua juu ya imani yangu ndiyo ya kweli zaidi kuliko nyingine na huu ndiyo ukweli na ushahidi upo na uko wazi. Sasa hamtakiwi kuogopa kuonyesha ukweli wa imani zenu,la sivyo mtakuwa mnaishi maisha yenu yote katika uongo na upotofu na huu ni uzembe.
Ni wachache wenye mtazamo mpana zaidi kuliko huo, na hawa wachache ndio wana harmonize dunia na kuleta amani la sivyo pangekuwa hapatoshi
Huu ni uongo ambao mpaka unakufa huwezi kuthibitisha ukweli wa kauli hii. Huwezi kuwa na mtazamo pana zaidi nje ya imani sahihi,huko ni kujidanganya. Hili halipo.Unao wasema wewe ni wajinga ambao wanaona maisha ni hapa na hakuna cha ziada na ndio hao hao hawajui kwanini wanaishi.
Hakuna watu wanao jua umuhimu wa amani kama watu wa dini hasa dini yangu,sababu wanaiangalia amani katika uhalisia wake.
Mimi nakupa kazi ndogo ili nikuonyeshe udhaifu wa hiki ukichokiandika,nitajie watu wawili tu wenye mtazamo huo mpana (unao dai) kisha tuwajadili japo kwa uchache wenye kukidhi haja.
Watu wa dini ndiyo wanasimamia amani ipasavyo sababu wanajua vijenzi na misingi yake.
Tumeshuhudia mauaji ya kutisha kwa ajili ya dini na imani
Tumeshuhudia ukatili wa kutisha kwa ajili tu eti kulinda dini, kulinda imani
Tumeshuhudia mifarakano na migongano kila kona ya dunia kuhusu dini na imani pia
Suala hilo linazungumziwa katika hali mbili,moja sahihi na nyingine si sahihi kwa msingi wa ufitini na ujinga. Tumeshuhudia fitina nyingi za nchi za magharibi katika umwagaji wa damu kwa ajili ya maslahi ya kidunia na haya ndiyo mauaji mengi na yana shamiri sana,lakini kwa wahusika kuficha ukweli na kuitangaza batili. Lakini wasahau ya kuwa "Japokuwa wao wanapanga na Mola naye ana panga na Allah ndiye mjuzi wa kupanga mambo". Hakika hali wa shani laiti ulimwengu ungefata dini hasa ya Uislamu,ulimwengu ungekuwa sehemu salama sana.
Ama nukta ya pili,katika usahihi kwenye dini kuna ibada inayo itwa Jihadi hii ni ibada na nguzo na msharti yake,na haipiganwi tu kiholela holela bali mpaka mashart na nguzo zidirikiwe. Sasa unachokiona katika mapigano yanayo husisha imani fulani mengi huwa hayaja kidhi vigez vya imani husika.
Sasa tujadili katika uhalisia nitajie mapigano au umwagaji damu ambao hauna mkono wa wafitini nawazungumzia nch za magharibi kisha mimi nakutajia vita ambavyo havina mkono wa wamagharibi,hizi akili tulipewa bure tuzitumie na tuseme haki popote tulipo.
Kaka hakuna kitu kizuri kama elimu,ili uamini ya kuwa elimu ni kitu kizuri,mpaka mjinga huwa unapenda aitwe msomi na mjuzi wa mambo wakati hana anacho miliki katika elimu husika.
Uchawi pamoja na ubaya wake wote unaosingiziwa haujaua mamilioni kama dini
Haujafitinisha mamilioni kama dini
Haujafanya ukatili wa kutisha sana kuliko dini
Kuna uchafu na ubaya wa kutisha ndani ya dini kuliko kwenye ushirikina ndio maana unapoongelea 'ukweli' wa dini napata ukakasi fulani
Ni kosa kubwa sana hasa kiakili kulinganisha mambo mawili ambayo kwa dhati yake kabisa hayafanani.
Ubaya wa uchawi si tu kufarakanisha watu,au kuua watu bali ni kutafuta msaada nje ya yule anayestahiki kuombwa msaada yaani Allah mtukufu,kwahiyo idadi hapa haina nguvu mzee bali athari. Mambo hayapimwi kwa wingi isipokuwa machache sana na ukifatilia sana uchache umesifiwa mno.
Kaka vipimo vyako dhaifu mno na havikupeleki katika kupatia ndiyo maana nakutaka ujenge hoja kwa mapito yako na mimi nijenge hoja kwa mapito yako. Mathalani kosa kubwa ambalo uko nalo ni kuwa msingi wa upimaji wa usahihi kwa mtazamo wako wewe ni wewe mwenyewe,sasa nitakuuliza wewe ni mwanadamu dhaifu mno,kuanzaia mwili,milango ya fahamu mpaka akili. Ndiyo maana si ajabu ukaona Ushirikina ni sawa huku historia ya ushirikina hijui. Hili tatizo kubwa mno.
Nakuja kuendelea hapa nilipo ishia...m