Natafuta wa kumrithisha mikoba, kilinge

Natafuta wa kumrithisha mikoba, kilinge

Ndugu wana JF huu si utani..! Niko serious..
Najiona kabisa nazeeka sasa na nguvu zinanipungua, hivyo nimekuwa na limited movements japo mahitaji bado yako juu
Nimeamua kutangaza kufafuta mrithi wa kazi zangu.
  • Mkoba mkuu mmoja
  • Mkoba wa kati
  • Mkoba mdogo
Hii mikoba yote iko Mkoa wa Pwani kilingeni Msata
Kilinge kila kila kitu cha uganga, ugaguzi, ulozi, ushirikina na kuwanga.. Kina vifaa vyote muhimu vya kale na vya kisasa kwa shughuli zote hizo..!

Ukubwa wa eneo ni miguu 50 kwa 40. Najiandaa kurudi kumtumikia mola wangu..infact nitakuwa na kituo changu cha huduma za kiroho zisizochangamana tena na shirki.

Niliwahi kuwagusia kuhusu hiki kituo kitakachojulikana kama MULT FAITH RESEARCH SOCIETY. Naona muda wa kuwa umekaribia kabisa!
Nitakuja kutoa aina ya mrithi nimtakaye!

Asanteni.
Mkuu ni kweli
 
Pale kaini na Abel walipotoa sadaka ya malimbuko na Kaini kutoa hafifu..Abel sadaka yake ikapokelewa na Kaini haikupokelewa...
Sasa kaka hapa Uchawi ujaingiaje ? Labda kama unaendelea kuelezea ili nione unapo igusia hoja ya msingi.

Au unataka kuniambia watoto hawa wa Adamu ndiyo walileta uchawi au ?

Kaka swali langu naona bado hujanijibu.
 
Ndugu wana JF huu si utani..! Niko serious..
Najiona kabisa nazeeka sasa na nguvu zinanipungua, hivyo nimekuwa na limited movements japo mahitaji bado yako juu
Nimeamua kutangaza kufafuta mrithi wa kazi zangu.
  • Mkoba mkuu mmoja
  • Mkoba wa kati
  • Mkoba mdogo
Hii mikoba yote iko Mkoa wa Pwani kilingeni Msata
Kilinge kila kila kitu cha uganga, ugaguzi, ulozi, ushirikina na kuwanga.. Kina vifaa vyote muhimu vya kale na vya kisasa kwa shughuli zote hizo..!

Ukubwa wa eneo ni miguu 50 kwa 40. Najiandaa kurudi kumtumikia mola wangu..infact nitakuwa na kituo changu cha huduma za kiroho zisizochangamana tena na shirki.

Niliwahi kuwagusia kuhusu hiki kituo kitakachojulikana kama MULT FAITH RESEARCH SOCIETY. Naona muda wa kuwa umekaribia kabisa!
Nitakuja kutoa aina ya mrithi nimtakaye!

Asanteni.
Hicho kilinge mkuu kwa vile umeona kwa Mungu ndiyo salama yako nakushauri umwite Askofu aje akipige moto na kuteketeza kila kitu kabisa!
 
Nimekujibu mara 3 lakini naona hujaridhirika na majibu yangu
Nilikujibu chanzo ama asili ya uchawi
Maswali yako yaliyofuata yalikuwa yanafananafanana hebu cheki muongozo uliotufikisha hapa
Hebu nisome kwa ufafanuzi zaidi
Kwenye maandiko ya Kikristo tunaambiwa Mungu ndie mganga wetu mkuu.. Mganga anagagua lakini pia hashindwi kufanya uchawi(kwa tafsiri yoyote ile)
Kwenye mapigo saba yale ya Misri Farao alileta waganga wa kupambana na madhila ya yale mapigo... Waganga wale walitaka kushindana na walawi wa Mungu lakini wakashindwa mfano walipoleta nyoka, Mungu kupitia walawi wake akaleta nyoka wenye nguvu zaidi na kuwala wale nyoka wa wachawi wa Farao
Uchawi ni pamoja na uwezo wa kutenda miujiza.. Uumbaji wa dunia kwa kutamka tu na ikawa ni mojawapo ya uchawi... Kama tunaamini kwamba vyote vinatoka kwa Mungu basi hata uchawi unatoka kwake
Uchawi wa cain unaanzia pale kwenye kutoa malimbuko ...roho ya kwanini! Inakuja hatua ya pili kijicho, wivu na husuda.. Halafu anakuja na uamuzi wa kumuua nduguye
Uchawi huanzia kwenye wazo na daima haliwi zuri
Je unanipata?
 
Labda kuna kitu hamjui vema, kuteketeza tunguli kwa moto ni tofauti kabisa na kuteketeza kilinge.. Kuchoma moto kilinge sio mwisho wake..kuna mengi ya kufanya..Moto ni hatua ya mwisho
 
Ndugu wana JF huu si utani..! Niko serious..
Najiona kabisa nazeeka sasa na nguvu zinanipungua, hivyo nimekuwa na limited movements japo mahitaji bado yako juu
Nimeamua kutangaza kufafuta mrithi wa kazi zangu.
  • Mkoba mkuu mmoja
  • Mkoba wa kati
  • Mkoba mdogo
Hii mikoba yote iko Mkoa wa Pwani kilingeni Msata
Kilinge kila kila kitu cha uganga, ugaguzi, ulozi, ushirikina na kuwanga.. Kina vifaa vyote muhimu vya kale na vya kisasa kwa shughuli zote hizo..!

Ukubwa wa eneo ni miguu 50 kwa 40. Najiandaa kurudi kumtumikia mola wangu..infact nitakuwa na kituo changu cha huduma za kiroho zisizochangamana tena na shirki.

Niliwahi kuwagusia kuhusu hiki kituo kitakachojulikana kama MULT FAITH RESEARCH SOCIETY. Naona muda wa kuwa umekaribia kabisa!
Nitakuja kutoa aina ya mrithi nimtakaye!

Asanteni.
Tatizo huo ULOZI,UCHAWI NA SHIRK tu!
 
Nitakuwa na uwezo wa kuwa kama popo bawa?ku ride ndinga kali?kama sivyo kaa nayo
 
Nimekujibu mara 3 lakini naona hujaridhirika na majibu yangu
Nilikujibu chanzo ama asili ya uchawi
Maswali yako yaliyofuata yalikuwa yanafananafanana hebu cheki muongozo uliotufikisha hapa
Hebu nisome kwa ufafanuzi zaidi
Kwenye maandiko ya Kikristo tunaambiwa Mungu ndie mganga wetu mkuu.. Mganga anagagua lakini pia hashindwi kufanya uchawi(kwa tafsiri yoyote ile)
Kwenye mapigo saba yale ya Misri Farao alileta waganga wa kupambana na madhila ya yale mapigo... Waganga wale walitaka kushindana na walawi wa Mungu lakini wakashindwa mfano walipoleta nyoka, Mungu kupitia walawi wake akaleta nyoka wenye nguvu zaidi na kuwala wale nyoka wa wachawi wa Farao
Uchawi ni pamoja na uwezo wa kutenda miujiza.. Uumbaji wa dunia kwa kutamka tu na ikawa ni mojawapo ya uchawi... Kama tunaamini kwamba vyote vinatoka kwa Mungu basi hata uchawi unatoka kwake
Uchawi wa cain unaanzia pale kwenye kutoa malimbuko ...roho ya kwanini! Inakuja hatua ya pili kijicho, wivu na husuda.. Halafu anakuja na uamuzi wa kumuua nduguye
Uchawi huanzia kwenye wazo na daima haliwi zuri
Je unanipata?
Kaka swali langu hujajibu mpaka muda huu,nilichokiona kwako maana ya uchawi hujui (hapa utanikosoa kwa kunipa maana ya uchawi,lakini mpaka muda huu hujajipa maana ya uchawi).

Nilikuuliza maswali mawili au matatu,la kwanza ni nini hasa uchawi na umeanza lini na nani wa kwanza. Ukasema tangu kuumbwa kwa ulimwengu,mwisho tukaja kubaliana ya kuwa vyote vinatoka kwa Mola,lakini ajabu umerudia tena suala ambalo laiti kama ungekuwa makini usingelisema tena sababu nimeligusia,ndiyo uchawi nao unatoka kwa Mola muumba.

Ajabu nyingine tena unaelezea tukio la watoto wa Adamu kama uchawi lakini haikutosha ukasema tena kitendo cha Mola kuumba dunia nao ni uchawi,hili ni tatizo la kiufundi la kutojua hasa uchawi ni nini. Mola ametakasika na hilo,ndiyo maana kuna miujiza na mazingaombwe.

Wivu,kijicho na mfano wa hayo si katika uchawi bali ni katika uovu na tabia mbaya.
 
Kaka ngoja nikusaidie katika maana ya Uchawi(Sihri) kisha unipe jibu la lini ulimwenguni Uchawi ulidhihiri.

Na nukuu :

"Amesema:“Neno “Uchawi”, kwakiarabu “As Sihr”,
maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na shetani nakwa msaada wake(shetani)”, na
akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo
mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia
watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.”

Ama Sahaba Ibni Abbas(Radhiya Llaahu
‘anhu) amesema : ”Uchawi ni kuidhirisha
batili katika sura ya haki.”
Hayo ni katika kamusi zalugha.

Amma katika kamusi ya dini,maana ya
neno Uchawi (AsSihr), kama
alivyo fasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhruddin Al Razi kuwa; ”Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na
ndani yake mnahadaa (khidaa).”

Tuendelee na mjadala kutokea hapo....
 
Unajua Jurjani Tunapishana kwenye uelewa mimi na wewe kwakuwa msingi wa mijadala yako unajikita zaidi kwenye kile imani yako ilivyokufunza na mara nyingi hupendi kuliona jambo nje ya hapo ama hutaki kukubaliana na mawazo huru nje ya imani
LAKINI bado si tatizo sana... Kila kitu kina asili mbili mbili na uchawi pia unazo hizo asili
Hizi nilizotaja ukaziita tabia mbaya ndio misingi ya mtu kuwazia kudhuru wengine kwa uchawi nk... Nimeishi kwenye kaliba ya uchawi kwa miaka 20 na ushee... Ni wachache mno mno mno wanaotafuta 'uchawi wa manufaa' ...! Na wote walioumizwa na uchawi asili ni hizo ulizoita tabia mbaya
 
Kaka swali langu hujajibu mpaka muda huu,nilichokiona kwako maana ya uchawi hujui (hapa utanikosoa kwa kunipa maana ya uchawi,lakini mpaka muda huu hujajipa maana ya uchawi).

Nilikuuliza maswali mawili au matatu,la kwanza ni nini hasa uchawi na umeanza lini na nani wa kwanza. Ukasema tangu kuumbwa kwa ulimwengu,mwisho tukaja kubaliana ya kuwa vyote vinatoka kwa Mola,lakini ajabu umerudia tena suala ambalo laiti kama ungekuwa makini usingelisema tena sababu nimeligusia,ndiyo uchawi nao unatoka kwa Mola muumba.

Ajabu nyingine tena unaelezea tukio la watoto wa Adamu kama uchawi lakini haikutosha ukasema tena kitendo cha Mola kuumba dunia nao ni uchawi,hili ni tatizo la kiufundi la kutojua hasa uchawi ni nini. Mola ametakasika na hilo,ndiyo maana kuna miujiza na mazingaombwe.

Wivu,kijicho na mfano wa hayo si katika uchawi bali ni katika uovu na tabia mbaya.
Nimekujibu kwa ufupi hapo chini , nimechanganya kwa pamoja post zako mbili, hebu nisome kisha tuendeleee
 
Labda kuna kitu hamjui vema, kuteketeza tunguli kwa moto ni tofauti kabisa na kuteketeza kilinge.. Kuchoma moto kilinge sio mwisho wake..kuna mengi ya kufanya..Moto ni hatua ya mwisho
Kwani mkuu wewe kinachokutoa huko ni nini? Kama umeona ni ushetani kwa nini unataka wenzio waendeleze shetani? Mshana Jr bwana, anauzia wenzake msala!!
 
ni vema mhitaji akautendea haki udadisi wake.. Akiona kuna faida atabaki...au kinyume chake..kwakuwa si wote ni waamini
 
Unajua @Jurjani Tunapishana kwenye uelewa mimi na wewe kwakuwa msingi wa mijadala yako unajikita zaidi kwenye kile imani yako ilivyokufunza na mara nyingi hupendi kuliona jambo nje ya hapo ama hutaki
Tunaishi kuutafuta ukweli kama ulivyo na si kama watu wanavyo ona au kuhisi.

Kawaida huwezi kulijua jambo kama lilivyo,bila kupita katika ile misingi kumi aidha kuijua au kutoijua. Historia imeshaandikwa na kalamu zimeshanyanyuka na wino umekauka,tunachotakiwa sisi kurejea na kuyapima mambo katika uhalisia wake.

Laiti kama watu wangeaza kujua maana ya maneno au vitendo kwanza hakika upotofu juu ya mambo ungepungua kwa kiasi kikubwa sana. Mathalani watu tungejua historia ya Uchawi na nini uchawi hakuna mtu angedai ya kuwa kuna uchawi wenye manufaa. Uchawi unatokana na majini yaani mashetani ya kijini sababu kuna majini wema. Hawa ndiyo walikuwa wanawafundisha wanadamu jambo hili,nabii Nuhu ameletwa duniani Uchawi upo,na alikuja baada ya kudhihiri Ushirikina,ushirikina ambao sababi yao ilikuwa ni majini kuwashawishi wanadamu wachonge masanamu ya waja wema ambao walifariki kitambo kirefu huko nyuma,kisha Mashetani hao hao wakawa wanawashawishi wanadamu wawaabudu masanamu hayo. Baadae kitovu cha uchawi kikawa ni mji wa Baabil (Babylon) huko Iraq,hii ilikuja katika kizazi cha nne cha nabii Nuhu baada ya lile gharika katika utawala wa Nimrod mwana wa Kan'aan mwana wa Kush mwana wa Saam mwana wa Nuh (Noah). Baada ya hapo ukaja ule uchawi sasa ambao walikuja nao wale Malaika Harut na Marut,wanazuoni wanasema uchawi huu ni tofauti na ule ulio kuwa unafundishwa na Mashetani wa kijini,huu ni ule uchawi ambao unafarakanisha mume na mke. Sasa tukishajua historia inatupelekea kung'amua jambo na kulipima kwa usahihi,sababu marejeo tunakuwa nayo tayari.

Tuendelee...
 
LAKINI bado si tatizo sana... Kila kitu kina asili mbili mbili na uchawi pia unazo hizo asili
Hizi nilizotaja ukaziita tabia mbaya ndio misingi ya
Hii si sahihi. Mimi naona tungeanza kwanza kujikita katika kudurusu maana ya Uchawi kisha tukakubaliana kutokea hapo,yaani tuwe na marejeo tuweze kuhukumu,wewe utoe maana yako ya Uchawi na wewe usome maana niliyo iweka hapa juu ya Uchawi kisha tuendelee.

Hizo sababu sasa haziitwi uchawi ila hupelekea mtu katika kufanya uchawi. Sasa swali uchawi ni nini hasa ?
 
Mimi nafaa kuwa mrithi! Shida yangu kubwa Mi Mlevi! Ukinipa KILINGE ipo siku ntawaroga SERENGETI na TBL ije kuwa majuto

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Pepsi tu chali
 
Hii si sahihi. Mimi naona tungeanza kwanza kujikita katika kudurusu maana ya Uchawi kisha tukakubaliana kutokea hapo,yaani tuwe na marejeo tuweze kuhukumu,wewe utoe maana yako ya Uchawi na wewe usome maana niliyo iweka hapa juu ya Uchawi kisha tuendelee.

Hizo sababu sasa haziitwi uchawi ila hupelekea mtu katika kufanya uchawi. Sasa swali uchawi ni nini hasa ?
Ok lakini nataka tuwe na tafsiri moja huru kwa wote bila kuegama viasili vya kiimani na dini za kuletewa zilizokuwa na malengo yake
 
Back
Top Bottom