Sasa haikonzani vipi wakati maana uliyoitoa inaonyesha hivyo.Hapana haikinzani bali sasa hizo ni aina za uchawi... Kumbuka hata kama ni nguvu hasi kiroho lakini bado haimzuii mtu kujifunza na kuelimika
Huko juu kama ulikuwa makini nilisisitiza juu ya maana na nikakupa maana ya maana na vijenzi vyake,lengo tusije kushughulika tena na maana ya Uchawi baada ya wewe kutoa maana ya tamko hilo. Lakini naona hali inakuwa kinyume. Sababu maana yako naona inaruhusu yaingie yasiyotakiwa kuingia na kuzuia yanayo takiwa kuingia.
Maana ulipose ni hasi...Maana yake vyote vinaangukia humo,ukivitoa baadhi ujue maana yako ina mushkeli.
Kwanini mtu ujifunze jambo ambalo hubadilisha uhalisia na kulifanya jambo baya kuonekana zuri na kufarakanisha watu ? Vipi uelimike kwalo ? Labda ujifunze ili uweze kuliepuka na si kulitendea kazi,ndiyo maana wale Malaika Harut na Marut,walikuwa wana watahahdarisha watu pale wanapo wafundisha Uchawi huo kwamba tunawafundisha lakini hii ni FITNA.
Sasa vipi ujifunze Uchawi kisha uelimike ?