Natafuta vijana wa kufyatua matofali

Natafuta vijana wa kufyatua matofali

Ndugu zangu sio masikini
Aisee alokupa wewe ndo kawanyima hao unaowaita maskini. hata kama una kipato kikubwa jifunje kumheshimu kila mmoja kwa nafasi yake. ndugu zako yawezekana sio masikini kiuchumi ila ni maskini kwa nguvu wangekuwa sio maskini wa nguvu basi ungewapa hao hayo matofali wakayafyatua.
 
Kama kichwa Cha habari kinavyosema hapo juu natafuta vijana watatu nitaowaajiri waje wafyatue matofali malipo ni 5000 Kwa siku kula juu Yao Kwa waliotayari waje pm mda huu Kwa mnaohitaji nimeamua kutoa ajira Kwa vijana wenzangu Ili tuweze kusonga mbele
Hivi unazijua tofali wewe? yaani 5000 kwa siku bora nikaibe kuliko kuteswa hivyo
 
images (9).jpeg
 
Watu wananiambiaga nachagua kazi lakini binafsi huwa naangalia malipo na risk ztokanazo na kazi yenyewe, kazi kama hii ni UJINGA kuifanya,kijana mwenzangu hata kama una shida ya ajira usijishushe kiasi hicho, ..sasa hapo ukila unabaki na nini? na kumbuka mtu anaefyatua tofali hali kawaida anakula haswaa ,hapo jioni bado,.. baada ya hapo unabaki na nini?
 
Mjombaa izi kazi ngumu uwa zina permanent price usiwafanye watu wajinga, kufaytua tofali na kuzipanga kuna bei zake, nafikiri kila tofali mia ndo elf tano iyo ni ktk mashine ile ya umeme, kuhusu zile za kushindilia inazidi
 
Hata mim nafahamu hivyo kwamba kufyatua tofauli kwa Gharama ya mfuko mmoja, Mfano huku kwetu mfuko mmoja wa saruji ni 4000- 5000 kutokana na maelewano. Kwahyo raia wakikupigia mifuko 20 ya wanaondoka kama na 80k mpaka 100k.
Hii angalau ina ubinadamu ndani yake.
 
Jana kuna kazi ilitangazwa humu kwa malipo ya 2k per day, huyu alitoa ofa ya kula bure mara 3 kwa siku.

Hiyo 5k ba kula juu ya kibarua 😪


Tuoneeni huruma majobless
 
Back
Top Bottom