Don Clericuzio
JF-Expert Member
- Dec 8, 2017
- 16,930
- 40,585
Umuhimu wa services kama hizo kuwa hapo hapo inapunguza migongano kwa wana kamati kutaka kuleta watu wao ili wapige 10%, pia mfano vinywaji vikiisha store iko around mnaongea vinaongezeka.
Kumbi nyingi zinajitahidi sana kwenye vyakula na mapambo siku hizi kwa sababu za kiushindani, hivyo usiwe na wasiwasi kuhusu hilo swala.
Advise zaidi: kumbi zote utakazoenda kuvisit nenda na mtarajiwa wako ili mfanye chaguo pamoja.
Kwa location ya wageni kutokea Upanga na Tabata, nadhani Sinza inaweza kuwa Centre nzuri, kuna kumbi kama Deluxe (iko Kijiweni), kuna ukumbi uko opposite na Big Bonn (Sinza Mori), pia kuna ukumbi uko barabara ya kutokea Sinza Makaburini kuelekea Kobil (Sam Nujoma), siukumbuki jina vizuri ni kitu kama Elegance or so. Hakikisha unatembelea hizo kumbi, moja kati ya hizo kwa budget yenu itakufaa.