sijajua imani yako, binafsi nilishawahi kupitia kipindi cha stress iliyoelekea depression kabisa. dawa pekee niliyoipata ni "YESU". katika kitabu cha Isaya wakati Yesu anatabiriwa kuzaliwa, aliitwa Mfalme wa Amani, Mungu mwenye Nguvu etc. depression kiini chake ni kukosa furaha na amani. jambo hili huwezi kulipata nje ya Yesu. na sio tu kwenda kanisani, ni Yesu kuingilia kati, Roho Mtakatifu akiingia kwako utapata amani ambayo haujawahi kuipata na furaha muda wote na depression huwa inafutika kabisa hadi unaisahau. nilikuwa na vidonda moyoni vingi sana, lakini hii pekee ndio iliniokoa. hadi sura ilikuwa imebadilika lakini Yesu anaweza yote.
siongei ili kutangaza dini, au lolote, ndio maana nimekwambia hata ukiwa kanisani, kama in reality Yesu hayupo moyoni na haujajazwa Roho Mtakatifu, hautakuja kupata amani, lakini pindi Roho Mtakatifu akiingia kwako, automatically kuna utulivu, amani na furaha isiyoelezeka inatua moyoni mwako. Mungu akusaidie katika Jina la Yesu Kristo.