• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Natafuta softcopy ya kitabu cha 'shamba la wanyama'

Gmpa

Gmpa

Senior Member
Joined
Aug 1, 2016
Messages
135
Points
225
Gmpa

Gmpa

Senior Member
Joined Aug 1, 2016
135 225
Wana jamvi naombeni mwenye soft copy ya kitabu cha shamba la wanyama (ANIMAL FARM) anisaidie au anielekeze namna yakukipata.
 
ndio walewale

ndio walewale

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
1,592
Points
2,000
ndio walewale

ndio walewale

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
1,592 2,000
Ninacho mkuu, fanya utaratibu nikutumie kwa wasap maana mimi si mtaalam sana kiasi cha kuweza ku upload humu.

Kama hautojali karibu PM unipe namba unayoweza kukipokea kupitia wasap
 
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Messages
3,921
Points
2,000
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2013
3,921 2,000
Ninacho mkuu, fanya utaratibu nikutumie kwa wasap maana mimi si mtaalam sana kiasi cha kuweza ku upload humu.

Kama hautojali karibu PM unipe namba unayoweza kukipokea kupitia wasap
Naomba Mkuu.0762997095
 
ndio walewale

ndio walewale

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
1,592
Points
2,000
ndio walewale

ndio walewale

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
1,592 2,000
Pakua kutoka hapo mkuu.
 
Attachments:

Gmpa

Gmpa

Senior Member
Joined
Aug 1, 2016
Messages
135
Points
225
Gmpa

Gmpa

Senior Member
Joined Aug 1, 2016
135 225
SHAMBA LA WANYAMA
Mwandishi wa kitabu maarufu, ‘SHAMBA LA WANYAMA’,George Orwell,jina lake halisi ni Eric Blair.

Alizaliwa India mwaka 1903, ambako babaye alifanya kazi kama Ofisa wa serikali huko Bengal.Akiwa mtoto,Eric Blair alipelekwa Uingereza, akasoma shule binafsi ya Eton, ambayo ilikuwa bora sana zama hizo.

Wazazi wake walikuwa makabwela.Hivyo, Blair akaishi katika madhila ya ufukara;maisha ambayo yalimfanya kudharauliwa na jamii ya Kiingereza yenye ukwasi.

Mwaka 1922, akajiunga na jeshi la polisi Burma, siku hizi nchi hii huitwa Myanmar.

Burma, ilitawaliwa na Uingereza kwa mkono wa chuma,kinyume na matakwa ya raia.Siku hizi Uingereza inaimba wimbo wa ‘Demokrasia’ kumbe kawimbo ‘demokrasia’ katamu,lakini waimbaji wake hunuka mithili ya kwapa la Ibilisi! Unafiki tu!!

Eric, alipopata likizo akarejea Uingereza ambako alikaa muda wa likizo ukapita-hakurejea Burma.Alijisikia vibaya sana kutumika katika jeshi la Kiingereza kuwakandamiza raia wa nchi hiyo na matakwa yao.

Naaam, ilikuwa mwaka 1927.Eric Blair aliishi London,na wakati mwingine mjini Paris,Ufaransa ambako aliishi katika lindi la ufukara wa kupindukia.

Aliishi sanjari na watoto wa mitaani, ‘chokoraa’ na wasio na ajira waliolala vibarazani katika mitaa ya kitajiri.Na wakati mwingine aliishi na wasio na ajira, na waliolipwa kiduchu mithili ya ujira wa mtwangaji.

Wakati mwingine, akaosha vyombo hotelini ili kujipatia mlo wa usiku hususan huko mjini Paris,Ufaransa.

Ni hapa, Eric Blair alipoanza kuandika kuhusu maisha yake ya kijungujiko.Kitabu chake cha awali kilichapwa kwa jina la GEORGE ORWELL,kwa sababu alisema alionea aibu jina lake halisi,Eric Blair! Ufukara!

Amewahi kuwa mwalimu, akaacha.Alifanya kazi dula la vitabu.Mwaka 1936 alimuoa Eileen Hertfordshire, wakaanzisha duka dogo la reja-reja.

Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Hispania, alikwenda huko ili kupata cha kuandika kuhusu vita; akajikuta katika mapigano makali.Alijikuta akipigana bega kwa began a Republican-akajeruhiwa vibaya, akatimkia Ufaransa na mkewe ambaye waliandamana naye.

Mwaka 1938 George Orwell alikuwa mgonjwa sana, hata vita vya Pili vya Dunia vilipozuka(1939-44) alitamani kujiunga jeshini,lakini hakufanya hivyo.

Alifanya kazi kama Mwandishi wa habari.Mkewe alifariki ghafla mwaka 1944;wakati mwandishi huyu mahiri alipokuwa yungali mwenye afya mbovu.Wakati huo, alitumia muda mwingi katika korido za hospitalini ili kutafuta tiba.

Mwaka 1949,Orwell alimuoa Sonia Brownwell.Walipanga kwenda Switzerland, lakini Orwell akafariki dunia mwaka 1950.

Vitabu vingi vya mwandishi huyu mahiri duniani vinahusu madhila yaliyompata katika taabu,dhiki,kudharauliwa sababu za ufukara.

Baadhi ya vitabu vyake ni Burmese Days, Down and Out in Paris and Londonvilivyohusu maisha ya ufukara katika miji mikuu ya Ulaya.

Homage to Catalonia, kinahusu vita Hispania, A Clergyman’s Daughter ni uzoefu wake katika kazi ya ualimu.

Aliandika Keep the Aspidistra Flying kama uzoefu wake katika duka la vitabu.The Road to Wigan Pier ni stori zake kuhusu maisha ya wasio na ajira Kaskazini mwa England, eneo la viwanda vikubwa.

Hata hivyo,George Orwell ni maarufu sana duniani kwa vitabu vyake viwili alivyoandika mwishoni mwa uhai wake.

“1984” ni kitabu cha kuogofya kuhusu maisha ya usoni(Future),wakati fikra za watu na maisha yao yatakapotawaliwa na serikali. Kwamba mwaka huo 1984 watu wasingeamua hatma ya maisha yao wenyewe-Udikteta.

‘ANIMAL FARM’ ni riwaya kali ya kejeli(satire) kuhusu wanyama-watu,akizungumza dhima ya Mapinduzi yaliyoshindwa ya Joseph Stalin huko Urusi.Si Urusi tu,kitabu hiki Animal Farm huonesha yanayojiri hata sasa hapa Tanzania.

Ujumbe mahsusi ni kwamba,tama ya madaraka ya viongozi huwaingiza walalahoi katika matumaini makubwa,kisha hugeuka watumwa wa kupindukia-hata humwaga damu yao ya thamani.

Baadhi ya “wanyama” katika riwaya hii kali huwakilisha watu muhimu sana katika taifa(Public Figures) na ambao hupendwa sana na mashabiki wao utadhani miungu-sacred cows ,kuwagusa inakuwa laana na kifo!

Ni maisha halisi ya wanyama hawa hata hapa unapopenda sana wewe bila akili tunduizi(critical mind).Nguruwe wajanja,wasomi waliojitia ku-“organize” wanyama wenzao ili kuondokana na utumwa ulioendeshwa na BINADAMU-Madhila ya utumwa na ukandamizaji hata leo tunao hapa hapa kijiweni petu-kila mtu na kijiwe chake.

Wanyama walikusudia kufanya MAPINDUZI uili kujenga JAMII YENYE USAWA! Jamii yenye usawa katika dunia hii hii eeh??

Taifa jipya la Wanyama walilokusudia baada ya mapinduzi ni lenye haki tupu,kweli,ubora na usawa, ambalo lingeleta Maisha Bora kwa Kila (Mtanzania)! Hapana, maisha bora katika shamba la wanyama-ANIMA FARM.

Kufuatia mawazo haya ya kimapinduzi, zilitungwa sheria, ama AMRI SABA(The seven commandments) ili kuwalinda wanyama.

Amri zote saba zilibeba maudhui na muktadha ya USAWA- “ALL ANIMALS ARE EQUAL”.Naam, usawa,usawia.

Nadhani msomaji umepata kusikia au kuona, ama vyote viwili-kuona na kusikia baadhi ya wanyama ambao ni ‘Public Figures’ katika Tanzania hii hii wanapotokwa mapovu mdomoni kuhubiri juu ya Tanzania yenye usawa,wakati ukweli halisi ni ubeberu na udikteta uliokamaa kuzidi wa mkoloni katili!

Nianze kukutajia AMRI SABA za wanyama wa George Orwell.Shamba la wanyama la Uingereza!

1.Kila aendaye kwa miguu miwili(binadamu) ni adui wa wanyama.

2.Kila aendaye kwa miguu minne au mbawa ni rafiki

3.Ni marufuku mnyama kuvaa nguo!

4.Ni marufuku wanyama kulala kitandani

5.Hakuna mnyama kufakamia kilaji(pombe,masanga,ulabu n.k)

6.Marufuku mnyama kuua mnyama mwenzake

7.WANYAMA WOTE WAKO SAWA

Amri hizi zote zilitundikwa ukutani,ili wanyama wote katika shamba hili la wanyama waishi na kuzifuata, na wanyama wote walisomewa kwa sauti ili wazisikie.

Kusudi ni kila mnyama kuondokana na utumwa,udikteta,ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka katika jamii ya wanyama-haki stahiki.

Ni ufisadi wa kutisha kwa wanyama hao wa George Orwell ulioendeshwa na binadamu.

Binadamu(binadamu mniwie radhi kusema haya) alikula bila kuzalisha chochote!(MAN IS ONLY CREATURE THAT CONSUMES WITHOUT PRODUCING)!

Binadamu HAMKAMULIWI MAZIWA,wala hamtagi mayai;ninyi ni dhaifu kupindukia hata hamwezi kukokota jembe linalokokotwa na wanyama kazi(plough).

Binadamu wala hamwezi hata kufukuza kasungura,mpaka msaidiwe na mbwa!

Mbwa akifukuza sungura,hutokwa jasho jingi na povu mdomoni; lakini mara anapokamata ‘Apwoyo’ sungura, binadamu humpora kasha huchukua minofu na kumtupia mbwa mifupa na matumbo! Mbwa hula makombo,pamoja na kulinda mali ya binadamu utadhani yake, wakati wa hatari, wa baridi,mvua-jua lake mvua yake!!

Eti huyu binadamu ndiye “Lord of all animals”, KATILI,mbinafsi ndiye anayeamrisha wanyama wote kufanya kazi na kumpa yeye chakula,kiburi na utajiri,anasa!

“Hata kinyesi cha wanyama ni mbolea.Kazi ya binadamu ni kulewa pombe na machangudoa,kulewa sifa na mafanikio hewa.”

Hizi kauli za wanyama zilitia simanzi.

Kwamba, ingawa wanyama ni chanzo cha mapato na kiburi cha mwanadamu katili, bado wanyama hawamiliki chochote wanachozalisha kasoro ngozi zao tu!

Ng’ombe hawamiliki hata galoni moja ya maziwa,miongoni mwa mabilioni ya papipa ya maziwa yanayokamuliwa kila mwaka na kuuzwa ama kunywewa kila siku!Kuku hawakuwa na haki hata ya kula yai moja.

Vyote,binadamu akafakamia.Kuku akila yai hata moja alilotaga, ni kosa. Mwisho wa siku hakuna mnyama anayenusurika kwa makali ya jisu! Kuchinjwa!!

Hata mbwa aliyejitia ‘rafiki’ wa binadamu,pindi anapozeeka na kuishiwa meno mdomoni, anaposhindwa kubwekea adui kwa maradhi na kuachwa nje kila siku, hufungwa kamba nene shingoni na kutupwa katika shimo refu, asiweze kuokoka!

Wenye masikio na wasikie.

Naam, kwa kifupi, sera za shamba la wanyama zilikuwa na mashiko,ili kuuelekeza umma wa SHAMBA LA WANYAMA kufanya mapinduzi=mabadiliko.

Maslahi ya wanyama hayakuwepo isipokuwa dhuluma,kudharauliwa,utumwa na unyang’au wa binadamu.

Binadamu walijiona “Aloof” walijiona wako juu kuliko wanyama,walijiona “Better than Animals”.

UNAFIKI WA KUTISHA

Hata hivyo,licha ya sera za wanyama kuitikisa nchi,mapinduzi yalipokuja(mabadiliko) viongozi wa shamba la wanyama wakayateka nyara.Wakabadili amri muhimu za usawa,amri zikaanza kusomeka hivi:

“ALL ANIMALS ARE EQUAL, BUT SOME ANIMALS ARE MORE EQUAL THAN OTHERS!”

Kwamba, ingawa wanyama wote ni sawa, baadhi yao(viongozi wateule wa mungu) walikuwa na usawa zaidi kuliko wenzao!

Nguruwe walipofanikiwa kuongoza mapinduzi ya kumtimua binadamu kwa mapinduzi makali, walianza kulewa pombe, afadhali ulevi wa pombe kuliko kulewa madaraka!

WALIVAA SUTI za binadamu!Mnyama kuvaa suti ya binadamu mkia nje!!Kanuni za usawa zikatupwa chini,wanyama wakakosa haki na usawa waliotegemea wakati wakifanya uasi dhidi ya mwanadamu.

Ndoto ya ukombozi ikaanza kupotea,demokrasia ikatupwa shimoni, wanyama wakaanza kusema, “Heri utumwa wa kwanza kuliko wa sasa!”Wenye masikio na wasikie.

Nguruwe, walioongoza mapinduzi,wakidai usawa na demokrasia,wakaanza kukataa kuulizwa ‘Mapato na Matumizi’ ya Shamba la Wanyama! Kuhoji hesebu za shamba la wanyama ikawa kujitafutia kifo ama kuchapwa mijeledi!

Ukihoji kwanini hata uchaguzi wa viongozi ndani ya shamba la wanyama, hakuna? Unaambiwa msaliti! Umetumwa na binadamu kuvuruga shamba la wanyama!

Unatimliwa kinyama,unavuliwa hata ngozi yako uliyopewa na Mungu! Unachapwa bakora!Wenye masikio na wasikie.

Uhaini! Eti kuhoji hesabu za shamba la wanyama ni uhaini,usaliti! Ufisadi? Hamtaki kuulizwa Mapato na Matumizi ya SHAMBA LA WANYAMA?

Nguruwe, hamtaki uchaguzi huru wa uhuru na haki? Hamtaki kuulizwa mhula wenu wa uongozi utakoma lini? Mnaanza kusingizia wanyama wenzenu kusaliti SHAMBA LA WANYAMA? Mizengwe,kuvuliwa ngozi yako uliyopewa na Mungu-This is abuse of political power.

For this reason animals have even less freedom than before. Wenye masikio na wasikie kilio cha shamba la wanyama!
 
Hammy Js

Hammy Js

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2017
Messages
3,023
Points
2,000
Hammy Js

Hammy Js

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2017
3,023 2,000
Na Mimi natafuta kitabu cha Hekaya za Abunuwasi, nasikia ni kizuri sana kinaburudisha
 
ndio walewale

ndio walewale

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
1,592
Points
2,000
ndio walewale

ndio walewale

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
1,592 2,000
Nimeupenda sana huo uchambuzi. Hongera sana mkuu kwa kushea nasi
 
James Comey

James Comey

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2017
Messages
5,069
Points
2,000
James Comey

James Comey

JF-Expert Member
Joined May 14, 2017
5,069 2,000
Kuna kimoja kinaitwa pedagogy of oppressed kama unacho tuwekee hapa mkuu
 
Alphaking2023

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
2,096
Points
2,000
Alphaking2023

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
2,096 2,000

Mbona kama Hilo shamba la wanyama linahusu chama flani cha siasa hapa nchini
 
Forum statistics

Threads 1,406,602
Members 532,389
Posts 34,520,755
Top