Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,375
- 14,870
Ngoja walaji waje
Kumbe kule Uarabuni wanakula sana hii kitu?? SikujuaUlaji mkubwa wa nyama ya kitimoto huathiri hata tabia za wanyama, mfano ukikuta madume ya simba yanaingiliana (yakifanya ushoga) basi utakuta eneo wanapoishi hao simba kuna nguruwe mwitu wengi na hao nguruwe ndiyo chakula kikuu cha hao simba.
You Google to find homosexual lions.
AiseeTembelea shamba hilo pengine wazo lako linaweza kupata mahala pakuanzia.
Hao jamaa kwa sasa zoezi lakuongeza thamani nyama kwa taarifa iliyopo imewashinda/wameacha .Kajifunze hapo kwanini walikwama.
Hadi saiv waendelea? Sijui nihamishie mrad wangu hukoNyongeza kidogo.
Mimi nipo mkoani ifakara, Morogoro. Ufugaji wa nguruwe kwa hapa ni rahisi kuliko sehemu yoyote nchini. Unapata pumba za Mpunga kwa bei ya kutupa. Maana hapa ndio wazalishaji wakubwa wa mpunga. Kg 70 ya pumba napata kwa shs 2500 hapo nishamlipa na mjazaji. Kwa nilivyo alwatan naweza kupata bure.
Mashudu ya alizeti yapo kwa wingi, Pumba za mahindi zipo kibao kwa kifupi ufugaji wa hapa ni rahisi. Ila changamoto zipo. Mimi sifanyi ufugaji wa kuzalisha, nafuga kuendeleza. Nanunua kwa kuchagua nguruwe wazuri ambao hawajadumaa.
Natengeneza chakula cha mwezi mzima kinanigharimu kama tsh 200k na kinatosha kulisha nguruwe 80-100 kwa mwezi. Ila pumba za mpunga zinazidi kwenye huo mchanganyiko.
Nachanganya pumba za mahindi, Mashudu ya alizeti, pumba za mpunga, chumvi, pig mix wakati mwingine na dagaa. Matengeneza gunia 30 zinatosha kulisha mwezi mzima. Nawalisha Ahsubuhi na jioni. Wanapewa majani kila baada ya siku tatu.
Ufugaji wangu ni kama kibubu. Nikiuza ndio nimevunja.
Kiwanda bado kipo??Mkuu uko mkoa gani?Ngurue wanatafutwa sana maana nakumbuka kipindi niko moshi,kulikua kuna wadau wanatoka Dar kutafuta ngurue,na walituambia kuna kipindi wanaenda mpaka mbulu kutafuta ngurue,mama yangu alikua mfugaji mzuri sana,na Ngurue wa 70kg alikua anamuuza 350k,hii ni kwa wastani wa 5000kwa kg.
Na pia alikua anasuply kiwanda cha soseji Arusha,na hawa wa soseji arusha walikua hawana longolongo,ukiwa na breed nzuri,na ngurue wa kiume uwe umemuasi toka akiwa na miezi mitatu,amasivyo nyama inakua na harufu ambayo madume wanakua nayo,na kwenye soseji hawataki iyo harufu.Ngurue wakifika kiwandani tuu,hela mama anawekewa CRDB Chap!
So demand ya Ngurue in kubwa sana has a Arusha,Moshi,Dar na Mwanza
Heh! Mchanga tena?
Dsm sehem gani mkuu. Ulipata mwekezaji?Kama mtahitaji eneo la kujenga hayo mabanda ,Nina eneo zuri Sana hapa dar tunaweza kuingia ubia ukajenga mabanda ya kufungia ,
Eneo Lina maji ,umeme ,na lipo jirani na main road ya morogoro road
Nafuatilia hapaDsm sehem gani mkuu. Ulipata mwekezaji?