Natafuta watu binafsi, creators au timu zenye Original Content (OG) zinazohusu maisha halisi ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vijana waliotoka vyuoni.
Maudhui ninayohitaji ni pamoja na:
Burudani na maisha ya kila siku ya wanafunzi
Elimu na maendeleo binafsi
Mahusiano na changamoto za vijana
Biashara na ujasiriamali wa wanafunzi
Ushauri wa kazi, ajira na maandalizi ya maisha baada ya chuo
Hadithi za mafanikio na changamoto
Simulizi za kuhamasisha na kuelimisha
Campus interviews na mijadala ya vijana
Vipindi vya maoni, fikra na uzoefu wa maisha
Masharti:
✓ Content iwe original na isiwe imekopiwa kutoka kwa creator mwingine.
✓ Muuzaji awe na haki ya kuuza au kushirikisha content hiyo.
✓ Video au maudhui yawe na ubora mzuri.
✓ Wenye uwezo wa kuzalisha content mara kwa mara watapewa kipaumbele.
Niko tayari:
Kununua content moja moja.
Kufanya ushirikiano wa muda mrefu
Kushirikiana na creators kutoka vyuo mbalimbali nchini.