Natafuta Ng'ombe wa maziwa

Natafuta Ng'ombe wa maziwa

Piga 0755-159607, huyu yupo pale shambani Kitulo kama mwalimu,atakupa simu ya meneja au akakupa majibu yote ya maswali ya awali, meneja bado sijampata. akikuuliza nani kakupa simu, mwambie Malila.

Thanks Malila, pamoja na article na psot kuwa ya zamani umenisaidia sana, nimeongea na Mwl and he will assist me to have number ya simu ya meneja wa shamba.
 
this Is very informative.. Mm mwaka jana nlifanya research ya kutosha.. nlikwenda mafinga... ihema iringa... mpaka liti mpwawa.. nashukuru pia kwa hizi taarifa na mm ntazifanyia kazi.. thanks
 
na mimi nangoja feedback maana toka 2010 ni kitambo sana
 
Jamani, naombeni msaada wenu.
Natafuta ng'ombe wa maziwa wa kisasa, kama wale wanaopatikana Iringa (ASAS Dairy products).Nitawapata wapi huko Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha n.k.
Naomba contacts.
Nahitaji wanaotoa at least lita 20 kwa siku.
Nataka wenye mimba ya kuanzia miezi mitano hadi sita.

Nimetafuta sana bila mafanikio!

Wafugaji wengine wananiuzia ng'ombe waliochoka (ng'ombe anatoa lita 3-4 kwa siku?)
Na serikali nayo kimeo, nilishaweka oda ya ng'ombe (hybrid) huko Nanyumbu wanasema oda ya mtu inaeza kuchukua hata miaka miwili na pia unaweza kupata idadi chini ya ile uliyoomba. Nonsense!

Naomba msaada wenu.

Natanguliza shukrani.
Mkuu Majimoto

Labda hujakutana nao WAPO WAKULIMA WANAUZA NGOMBE WENYE MIMBA, Moja wao alikuwa jamaa wa ASSAS-Iringa alitoa matangazo mpaka kwenye magazeti. Pia hata watu binafsi wanazo kunajamaa ntawasiliana nae ili anipe contact then ntaziweka hapa
;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; ******** mahitaji yaNg'ombe wa maziwa ,Ushauri n.k wasiliana na veterinary products, mobile phone 0754987809
 
Good idea! hivi unaweza ukafahamu bei ya kila ng'ombe kwa kulingana na umri wake? kwa kweli ni mradi mzuri kama ukiwa na eneo kubwa kama ulivyosema.
kama mkipata hao n'ombe naomba n mimi nipewe taarifa maana nina interest ya ufugaji hasa wa ngombe na kuku.
kwa ng'ombe mwenye mimba unaweza ambiwa 1.7m au 1.5m, ka ndo uzao wake wa kwanza inaweza kuwa 1.3 nakuendelea, japo kunabaadhi wanauza bei za kawaida ila nao ndo unakuta wamesha wachanganya changanya yani mtu unakuta anamajike tuu yani popote akisikia panadume anapeleka maana ng'ombe kapata joto kitu ambacho kinaharbu mbegu na utoaji wa maziwa maana dume si wote ni mbegu ya maziwa wengine wakiona dume kubwa ndo wanasema huyo ndo wa maziwa kumbe la
 
Mkuu taasisi zote za serikali sehemu kubwa ziko hoi kihuduma.
Zinafanya kazi kwa matakwa ya watu fulani lakini sio soko (kama ilivyo kwako). Soko la ng`ombe hawa ni kubwa sana mkuu. Juzi nimevuta uzi ili nipate ng`ombe wa kituo cha watoto Yatima,nikaambiwa may na june hawapokei maombi mpaka july. Niliishiwa nguvu. June/July hii napiga kwata mpaka kwa meneja,yaani itakuwa uso kwa uso ili anisaidie japo niwe kwenye foleni ya mwaka mzima.
Ulifanikiwa mkuu?
 
Wadau naonba kujua Tanga fresh wananunua bei gani kwa lita ya maziwa toka kwa mfugaji mkoa wa pwani?
 
sina bei yao ila naona kuna baadhi ya mawakala wanakusanya maziwa japo sijajua ni wa kampuni gani, bei zao zinatofautiana mara zishuke mara zipande ila ni kati ya 1000 mpaka 1500
 
Cha G,
Kuna CEO wa kampun moja hapo dsm ana shamba la kufa kiumbe pale siha-k'njaro na ni mfugaji mkubwa wa Ng'ombe. Ana ngombe zaidi ya 2000 pale siha katka mashamba tofaut mawili. Ng'ombe 1 anatoa lita 30 mpaka 52. Anasema ukitaka maziwa meng lisha ng'ombe wako pumba,wape maji ya kutosha, na pia ili maziwa yawe bora lishe lazima izingatie ratio. jamaa amefungua kiwanda cha kupack, fresh na yogurt juz tu! Nipm nikupe email yake akupe njia/ushaur.
Mkuu habari ,,naomba email ya huyu jamaa.
 
Nashukuru sana.
Nimeongea naye jana saa 12 jioni, ng'ombe wapo (Freishian).
Wenye mimba ya miezi 3-4 laki 7 lkn mpaka uweke oda.
Wanakuza mitamba mfano wakipandisha 30, 20 wanaweka kwa ajili ya kuzalisha zaidi, 10 nd'o wanauza.
Katika uzao wa 1-3 wantoa lita 20-40 (avarage 30) kwa siku - lkn katk maeneo ya baridi 4-15 degree Celcius eg. Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha n.k
Kwa maeneo ya joto inabidi uwajengee banda chini ya mti kwa ajiri ya upepo na ubaridi ili ku-cool environment, japo pia production ya maziwa siyo sawa na maeneo ya baridi, ukiwachunga katika maeneo ya joto production inazidi kuwa ndogo.

Akanishauri maeneo ya joto nichukue chotara (hybrid) na akanipatia contacts za Manager wa Sao Hill; nilipowasiliana naye akasema ng'ombe kwa sasa wapo wachache sana,labda hadi mwakani. Nilipomwambia nikiweka order ya ng'ome 20 nitapata? Akastuka kushangaa kuwa si rahisi kabisa!!
Naona itabidi niwachukue tu hao wa Kitulo kuanzia September/October, October/November na November/December. Nitatumia wataalamu kunijengea mabanda na kunishauri nyasi za kupanda na utunzaji wake; baadaye nitaanza kuwapandisha ili kuzalisha chotara.

Hata kama nisipofanikiwa kununua mwaka huu, I wish I start this project not before June, 2012.

Lkn hii nchi yetu vipi?
KILIMO KWANZA NI SUSTAINABLE KWELI? Kama mtu mmoja tu akihitaji ng'ombe 20 toka shamba la Serikali, Serikali inakuwa haina uwezo tutafika kweli?
Mkuu ulifanikiwa ,kama hutojali naomba utupe mrejesho.
 
Back
Top Bottom