Nitafurahi sana utakapo-implement project yako.
Nashukuru sana.
Nimeongea naye jana saa 12 jioni, ng'ombe wapo (Freishian).
Wenye mimba ya miezi 3-4 laki 7 lkn mpaka uweke oda.
Wanakuza mitamba mfano wakipandisha 30, 20 wanaweka kwa ajili ya kuzalisha zaidi, 10 nd'o wanauza.
Katika uzao wa 1-3 wantoa lita 20-40 (avarage 30) kwa siku - lkn katk maeneo ya baridi 4-15 degree Celcius eg. Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha n.k
Kwa maeneo ya joto inabidi uwajengee banda chini ya mti kwa ajiri ya upepo na ubaridi ili ku-cool environment, japo pia production ya maziwa siyo sawa na maeneo ya baridi, ukiwachunga katika maeneo ya joto production inazidi kuwa ndogo.
Akanishauri maeneo ya joto nichukue chotara (hybrid) na akanipatia contacts za Manager wa Sao Hill; nilipowasiliana naye akasema ng'ombe kwa sasa wapo wachache sana,labda hadi mwakani. Nilipomwambia nikiweka order ya ng'ome 20 nitapata? Akastuka kushangaa kuwa si rahisi kabisa!!
Naona itabidi niwachukue tu hao wa Kitulo kuanzia September/October, October/November na November/December. Nitatumia wataalamu kunijengea mabanda na kunishauri nyasi za kupanda na utunzaji wake; baadaye nitaanza kuwapandisha ili kuzalisha chotara.
Hata kama nisipofanikiwa kununua mwaka huu, I wish I start this project not before June, 2012.
Lkn hii nchi yetu vipi?
KILIMO KWANZA NI SUSTAINABLE KWELI? Kama mtu mmoja tu akihitaji ng'ombe 20 toka shamba la Serikali, Serikali inakuwa haina uwezo tutafika kweli?