Deeboyfrexh
JF-Expert Member
- Apr 3, 2015
- 3,240
- 5,248
Mambo sio rahisi namna hii kwenye nchi ambayo Waziri anaweza akaamka na kujitungia Tozo za ajabu ajabu kwa kuziita za kizalendo!Habari wana JF!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Natafuta mtu wa kuja kuwekeza Milioni 2.5 tu katika biashara ya kusaga na kukoboa mahindi pamoja na kuuza viroba vya sembe na dona, Viroba vitakuwa kwa mfumo wa 25kg, 10kg, 5kg. Kila kitu kipo cha kuweza kusagisha na kukoboa mahindi na kuufunga katika viroba. Ufuatao ni mtiririko wa manunuzi, mauzo na mgao wa pesa kwa muwekezaji na mmiliki wa mashine;
Manunuzi:
Tani 2(kg 2,000) za mahindi kwa wiki
Bei ya kg moja ni Tshs 500
Bei ya kg 2,000 ni Tshs 500×2,000= Tshs 1,000,000/=
Uzalishaji:
Kwa Tani mbili zinatoa,
Wastani wa viroba vya 25kg= 56
Magunia 6 ya Pumba
Mauzo:
Viroba 56
Kila kiroba kwa sasa ni Tshs 19,000/=
56 X 19,000/=1,064,000/=
Magunia 6 pumba@15,000=90,000/=
Jumla kwa Tani mbili ni 1,064,000+90,000=1,154,000
Usagishaji:
Kusagisha kwa siku wastani Tshs 20,000/=
Kwa wiki 120,000/=
Kwa mwezi 480,000/=
Faida:
Unga kwa Tani mbili kwa wiki ni Tshs. 154,000/=
Kwa mwezi ni Tshs. 616,000/=
Usagishaji kwa mwezi ni Tshs.480,000
Jumla faida wastani ni 1,096,000/=
Matumizi:
Umeme+Ushuru kwa mwezi ni Tshs. 50,000/=
Mfanyakazi fundi kwa wiki ni Tshs. 50,000/=
Kwa mwezi ni Tshs. 200,000
Mfanyakazi wa kupepeta wiki ni Tshs. 21,000/=
Kwa mwezi ni Tshs. 84,000/=
Fremu kwa mwezi Tshs. 200,000/=
Jumla Tshs. 534,000/=
Faida Halisi (Net Profit ):
Tshs. 1,096,000-Tshs.534,000 = Tshs. 562,000/=
Mgao:
Mgao kwa investor Tshs. 250,000/=@mwezi
Kwa miezi 15 ni Tshs. 3,750,000/=
Net Profit yake:
Tshs. 3,750,000- Tshs. 2,500,000= Tshs. 1,250,000/=
Mgao kwa mmiliki wa mashine kwa mwezi ni Tshs. 312,000/=
Note:
Huo ni mgao wa mtaji wa Tani mbili ambao ni Tshs. Milioni moja. Milioni 1.5 inayobakia itatumika kuhamishia mashine kuipeleka barabarani-kwenye soko zaidi (Nyerere road-Barabara ya Gongo la Mboto hadi Chanika)na ayo ni mahesabu pindi ilipokua majohe (Gongo la Mboto kwa ndani) ambapo haya ni makadirio ya chini ya mauzo kuliko uko inapopelekwa/itapopelekwa (hivyo tegemea kua kwa ongezeko la mgao wa faida kwa muwekezaji kwa kila mwezi). Lengo ni wote wafaidike-Muwekezaji na Mmiliki.
Pia kutakua na kuingia mkataba wa kimaandishi wa miezi 15 na kushuhudiwa na mashahidi wa pande zote mbili.
Namkaribisha Muwekezaji
Kwa nchi ambazo government policies ziko imara ningekubaliana na hii assesment!