Natafuta mtoto wa kulipia Ada form one kijijini

Hao wamekariri. Shule za kata wanalipia hasa zile za boarding pesa ni kuanzia laki na 20 na kuendelea. Hata hizi za day gharama ni nyingi sema haziitwi ada
Shule za boarding za serikali ada ni elfu 70 tu. Kama umelipishwa laki na 20 au laki mbili, basi utambue fika hizo hela za ziada ni kwa ajili tu ya michango ya mahafari, na takataka nyingine.
 
Mimi sijakuzuia kusaidia hao watoto wenye uhitaji mkuu. Nakutakia kila la heri. Wasiwasi wangu uko tu kwenye hiyo njia uliyo ichagua. Ya kutaka kupigiwa simu na Watanzania maskini kuanzia saa nne usiku!

Hivi sidhani kama umeweka na ukomo wa kupigiwa! Maana haijulikani ni kuanzia saa nne usiku mpaka saa ngapi! Na hujatuambia kwa siku utapokea simu za watu wangapi! Utaongea nao kwa muda gani, nk.
Hadi muda huu Nina sms 100
 
Advance ndo balaa michango mingi unakuta mwalimu anataka wanafunzi watoe elfu kumi kila mmoja ili afundishe somo husika
Juzi juzi kuna dogo wa Kibaha sec advance tulilipia. Ndo nikawa nashangaa labda kata hawalipii

Wabongo bana
 
Sijabisha na wala sijakataa kuhusu ada na michango yake so sioni mantiki ya quote yako
Shule za boarding za serikali ada ni elfu 70 tu. Kama umelipishwa laki na 20 au laki mbili, basi utambue fika hizo hela za ziada ni kwa ajili tu ya michango ya mahafari, na takataka nyingine.
 
Kuna Dada Amekimbiwa Na Mpenzi Wake Wakati Mjamzito Anaish Na Mama Yake Tu, Amejifungua Wiki Sasa Kwa Op Yupo Hospital Moja Huku Kusin Ya Kanisa, Hana Pesa Kabisa Ya Malipo Ameshikiliwa Yeye Na Mwanae, Kama Unaweza Kumsaidia Niambie Nimpe Mawasiliano Yako.
 
Back
Top Bottom