BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 2,705
- 6,503
Kwa mzazi ambaye kichwa kina chaji hawezi ruhusu huu uhuni, hii inawezekana kwa wazazi wapumbavu pekee, ambao kiwango cha kuwaza ni zero.
Mtoto kasoma miaka 7 sasa kamaliza shule, huyu hapumziki, anaunganishwa aanze kitu kinaitwa Pre-form one, atapigishwa Pre-form one hadi December then January aanze shule.
Na wazazi wengi tulivyo wapumbavu tunaona ndio njia sasa ya kumfanya mtoto aje kuwa kama Elon Musk wa Tesla au Mark Zuckerberg wa Facebook na Whatsapp. Yaani njia ya kumfanya mtoto aweze hata kuvumbua chombo cha kwanza cha Tanzania kwenda Mwezini ni kumpelekea Pre- form one.
Watoto hawana muda wa kupumzisha akili, na hii njia za Pre-form one ni njia za Wazazi kukwepa majukumu, Wazazi wa Kiafrika hawataki kukaa na watoto wao hata kuwafundisha elimu ya Duniani, kumfundisha maisha.
Wahindi sio wajinga kwenda na Watoto wao wa miaka 6 Dukani au Offisini kwao.
Ila sisi Wabongo tunaofanya Biashara eti hatutaki kwenda na Watoto wetu kwenye maeneo ya Biashara angalau waangalie kile tunachofanya, tunadanganywa na wahuni kwamba watoto wanapaswa kwenda Pre-form one kujifunza.
Ni vitu gani wanajifunza huko Pre-form one ambavyo hawatajifunza Sekondari?