natafuta mke wa kuoa

mkulimamwema

Senior Member
Apr 14, 2011
153
18
Walimwengu mimi ni mwanaume mwenye miaka 26 na tangu kubalehe sijafanya mapenzi nipo chuo kikuu,niliwahi kupenda wasichana wawili wote waliniumiza(sikufanya ngono nao kwani nilimwahidi MUNGU mpaka nioe) sasa umefikia wakati siwezi kuvumilia tena na ningekuwa safi kiuchumi ningeoa mwaka huu,na kuvunja ahadi niliyomwahidi muumba nafsi inaniuma zaidi mchumba niliyenaye anataka nifanye naye mapenzi,yeye bado miaka 4 amalize chuo au nitafute mwingine maana naona ananichelewesha
 
Acha uongo na kupendezesha story, kama ulimwamini mungu mwombe yeye atakuonesha mbona sasa unataka kumtosa Mungu? Wewe yote hayo kama umefanya sawa Mungu kakusaidia sasa cha kuja mataifani kutafuta ushauri? Umemsahau aliyekuwezesha kote huko?
Nimekujibu hivyo kwa sababu nimejua story tu hiyo unataka kuwarusha roho mademu zetu humu kuwa wewe badooooo.
 
hongera kwa kujitunza,maana ni wanaume wachache wenye kujitunza,jee mwenzako na yeye hajawahi?maana kama hujawahi,unakuwa huna haraka ya kuvunja amri.na kama mwenzako anataka mvunje amri na wewe hutaki,bora alivyokuwa mkweli kwako,kuliko angekuendea kinyume na akampa mwengine tunda.jee unampenda?na kama unataka mwengine,usifanye haraka ya kutafuta mwengine,uoe chapchap kwa ajili ya tendo la ndoa,ndoa ina mambo mengi, ambayo ukiingia ndio unaujua uchungu wake na utamu wake.
 
Aisee! Unafaa kuwa mfano wa kuigwa!

26yrs bdo hujavunja amri ya Mungu? Kama ni kweli 'HONGERA'
 
Hii thread inafanya nini hapa??? Peleka uongo wako Love connection muwe mna mazoea ya kusoma sio kukurupuka tu na kuanzisha mithread yenu msituharibie MMU yetu
 
Walimwengu mimi ni mwanaume mwenye miaka 26 na tangu kubalehe sijafanya mapenzi nipo chuo kikuu,niliwahi kupenda wasichana wawili wote waliniumiza(sikufanya ngono nao kwani nilimwahidi MUNGU mpaka nioe) sasa umefikia wakati siwezi kuvumilia tena na ningekuwa safi kiuchumi ningeoa mwaka huu,na kuvunja ahadi niliyomwahidi muumba nafsi inaniuma zaidi mchumba niliyenaye anataka nifanye naye mapenzi,yeye bado miaka 4 amalize chuo au nitafute mwingine maana naona ananichelewesha

Upo sayari gani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom