Natafuta mke

makaveli10

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
28,131
81,003
NATAFUTA MKE (MWANAMKE WA KUOA)

Assalaam aleykum warahmatulahi ndugu zangu

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza natafuta mke wa kuoa.

Mtu atajiuliza why, nitafute mtandaoni ?
Binafsi naamini waliokuwepo mtandaoni ni sawa na waliokuwepo mtaani, kuna watu safi, kuna watu waovu vike vile, kama ambavyo mtaani wapo, lakini mtandao unanikutanisha na watu ambao katika maisha yangu ya kila siku si rahisi kukutana nao.

Kwanini nataka kuoa
Kwanza ni sababu dini yangu imenitaka mimi nioe, ndoa ni utulivu wa nafsi, ndoa ni nusu ya dini, ndoa ni stara.
Binafsi naona ibada ya swala bila ya kuwa na ndoa nakuwa katika kucheza pata potea, na hili ndio linalonisukuma hasa hasa kutaka kuoa, ili nipate kufanya ibada vema, ibada zenye uzito mkubwa ndani yake..
Pili kuna maisha fulani natamani kuishi ila haya pasina mke bora(mcha mungu) sioni kama nitaweza kuishi walau robo yake.

Mwanamke wa aina gani ?
Kama naoa sababu dini, basi sina budi kuoa mwanamke ambae dini yangu imenifundisha(imenielekeza) kuoa.
Rasulillah s.a.w ametufundisha mwanamke anaolewa kwa mambo manne(4) i.e dini yake, nasaba yake, uzuri wake na mali yake, hivi ndio vigezo, katika hivi kila mtu atachagua kwa kigezo ama vigezo katika hivi vi4
binafsi nikiambiwa nichague kigezo kimoja tu, basi nitaoa mwanamke kwa dini(uchamungu) natafuta mwanamke tuishi hali ya kuwa duniani tunapita, tuishi kwa ajili ya kesho yetu, na inshaallah mola wetu akituridhia atutie katika pepo yake, nae akawe huraini wangu peponi.

Kwa mimi

DINI - awe na elimu kubwa ama ndogo ya dini sijali, muhimu awe tayari kuishi kwa ajili ya kesho yetu

NASABA - kwa mtandaoni hiki kigezo nakosa hata cha kuzungumzia, ni kigezo muhimu saana, wazee wetu wa zamani hata kama dini walikuwa hawajui saana, ila walifaulu kwa kigezo cha nasaba, maana ukoo mwingine mtihani mtupu, unaweza ukauingia ukoo una maswahibu yake sio mchezo, walikuwa sahihi kuoeleana, makaveli mwanangu anataka kuoa naenda kumposea kwa mzee njukuru sababu naujua ukoo vizuri, wakati mwingine binti anakuwa namuona malezi ya bwana njukuru nayajua, yeye bwana njukuru ananijua vema, hii ndoa ikawa rahisi, lakini siku hizi tunaokotana okotana, na maisha yetu ya kimjini ndio mtihani. Allah anifanyie wepesi katika hili, yeye ndio mjuzi zaidi anayajua yale yaliyodhahiri kwangu na yasiyokuwa dhahiri.

UZURI - Uzuri wa mtu uko machoni kwa mtu, kwangu mwanamke akiwa mweupe, pua ndefu kidogo, kasura kazuri zuri kidogo(sura za kitusi) mrefu, umbo lolote kama, akiwa na vinyama nyama inapendeza zaidi.. Lakini akikosa kigezo chocjote hapa asijali, kwangu muhimu ni huo utayari wa kuishi kwa ajili ya kesho yetu, anaweza akawa na kigezo kimoja, au hana kabisa asijali.

MALI - kwangu awe nacho awe hana, hiki kigezo sikizingatii.

N.B sijata umri hapo, sababu mtume hakutaja umri, alioa wakubwa kwake na wadogo pia. Kama atakuwa 30+ mpaka kwenye 40+ hivi itapendeza zaidi, ila hata km itakuwa chini ya hapo kweye 25+ si mbaya pia, awe mjane sijui nini, muhimu ni utayari wake kuishi maisha yanayompendeza mola wetu.

Mimi nani
Mimi ni kijana tu wa kiislaam, mweupe kiasi, mrefu, sina elimu kubwa saana ya dini, na pia nina elimu kiasi kwa elimu ya duniani, mwisho form 6, chuo nikasoma mwaka mmoja tu (....) maisha yangu ni ya kawaida tu, alhamdulillah , vijana wa siku hizi wanasema nabangaiza.

Kipi nisichopenda. 1. Kuacha kufanya ibada, 2. Usaliti. Hivi ndio vitu viwili vinaweza vikavunja na ndoa yenyewe, mengine tutavumiliana vumiliana, binadamu sie, si wakamilifu. Moja ya sifa kuu ya ndoa ni kucover(kustiriana) pale kwenye mapungufu ya mwenzangu nimstiri nae kwenye mapungufu yangu anistiri.

Ujana nimeufanya saana lakini nimekuwa nikiishi nakufikiria kesho yangu, najitahidi kufanya ibada kuna wakat najisahau, lakini kuna aina fulani ya maisha nayatamani na naamini pasina ndoa ngumu kuyaishi kwa kweli. Kiukweli kabisa maisha ya dunia ni mpito tu. Kesho yetu ni ndefu mnoo, maisha yake hayana mwisho, ikiwa nitamuelekea mola wangu hali kanikasirikia basi mimi ni mpotevu, na ikiwa nitamuendea hali hajanikasirikia basi nimefaulu, natamani niwe miongoni mwa wailofaulu.

Mtume Muhammad s.a.w
"Dunia ni starehe, na starehe iliyo bora zaidi ni kumpata mke mwema." Sambaza ujumbe huu kadri utakavyoweza uwafikie watu wengi wengi.


Allah atufanyie wepesi katika mazito yetu, atujaalie mema duniani na kesho akhera, atuepushe na moto, atuepushe na adhabu zake kali, atupunguzie uchungu wa umauti, atujaalie mwisho mwema, ajaalie makaburi yetu yawe viwanja katika viwanja vya peponi.

Wala tusiwe miongoni mwa waliopotea. Ya rabbi bila huruma yako sisi tumeangamia, bila ya uongozi(nusra) wako sisi ni wapotevu.

Nina mengi ya kuandika muda tatizo.

Wabillahi tawfiqi.

____________________

UPDATE(March 02)

Niseme alhamdulillah, ama hakika sifa zote njema anastahiki mola wa viumbe woote.

Kwakuwa jambo nilileta humj si vibaya pia kuleta mrejesho humu, kuna ndugu/washikaji kadhaa walikuwa wanaulizia mrejesho akiwemo bwana Darmian na wengine wengi.

Wazee ndugu yenu nimefanikiwa, japo kazi haikuwa rahisi saana, maana waliojitokeza ni wengi kuliko nilivyokuwa natarajia, mie nilidhani ni suala jepesi tu la kuandika hapa JF atokee mtu nione siku zisogee.. Ila walitokea wengi mnoo, wanawake saafi kabisa wenye uhitaji wa ndoa wapo wengi. Nasikitika uwezo wangu mdogo siwezi kuoa walau wawili, kwa ghafla.

Lau kama ningekuwa na uwezo ningeoa hata wa3, sababu katika kuwapunguza punguza walibaki wachache ambao naona wanafaa kabisa, ila ilinilazimu niwaache tu, sababu niliyoelekeza hapo chini.

Nimefanikiwa kwa huyu mmoja, na mahari nimefanikiwa kupeleka MAHARI, harusi ilibidi iwe mapema kama nilivyotamani, ila kutokana na mchumba mwenyewe bado yupo darasani likizo yake ni mwezi April (ndogo) na ile kubwa ni September, nilipanga iwe April, hilo ndio lengo langu, lakini MAMA MZAZI (yangu) ameniomba nisogeze mbele sina budi kufanya mwezi huo kutokana na ratiba ya mwenzangu.

Shukrani kwa wote, wale walioleta mzaha na pia walioniamin na kunipa moyo.

Pia wale warembo walionifata, imeshindikana waniwie radhi, hali ipo km nilivyoeleza, inshaallah panapo uhai naweza ongeza nitawafikiria km bado mtakuwa hamjapata stara.

Nawaombea ALLAH awafanyie wepesi nanyi mpate waume wa kufanya stara kwenu, mpate waume bora, waume wa ndoto zetu, na allah awajaalie vizazi vyenye manufaa na nyinyi duniani na kesho akhera.

30th MAY, 2021

Siku zinasogea, mambo yanakwenda. JF imenipa washikaji, imenipa ndugu, na sasa inaeoekea kunipa mke.

Ndugu zanguni tarehe 10/October naenda kuchukua jiko huko mjini Nzega.

Kuna watu walinipa moyo kuna watu walidhani nataka nile mabinti za watu kimasihara. Katika mara chache maishani mwangu nilizokuwa serious, hapa nilikuwa serious.

Mambo ni mengi ya kuzungumza, lakini kikubwa ni kuarifiana kuwa jambo letu linaelekea vema, kuna watu walinipa moyo na kunitakia mema katika hili hivyo ndugu zanguni dua zenu hazikubaki chini.

Maya Angelou Darmian RReigns financial services Mshana Jr Obe Rebeca 83 Goguryeo Its Pancho MzeeMpya 2sexy ledada Mwifwa Ushimen Castr Dinazarde QUIGLEY Bitoz THOMASS SANKARA @byembo jimama26 funzadume FORTALEZA Mussolin5 mtu chake mbalizi1 Dinazarde
Alexander The Great grand millenial

Si rahisi kuwakumbuka woote kwa haraka haraka, hawa ni kwa uchache kuna wale waliodhani nataka kuwala watu kimasihara(walishindwa kuniamini), wale wazee wa kejeli, kuna walionisapoti(kuniamini) kwa kunipa moyo. Bila kusahau ndugu zangu toka taifa la MAKAPUKU kule, wale wa jukwaa letu la michezo haswa FOOTBALL , na wale wazee wenzangu wa zamani toka jukwaa letu pendwa (JLW) kabisa lile la WATU TULIOKULA CHUMVI NYINGI
 
The bigger explaination, the bigger the Lies...
Tumetofautiana akili, kufikiri, maono n.k, so siwezi kukulamu kuhisi hivyo unavyohisi, huenda ndio akili yako ilipoishia..
Siwezi kukulazimisha uamini usichokiamink mzee
Haya ni maisha yangu binafsi, lau kama ungekuwa unamjua makaveli mwenyewe ungesadiki pasina chembe ya mashaka

Lakini pia unaweza kuwa sawa katika slogan hiyo, lakini tambua huwezi kuwa sawa nyakati zoote, maisha hayana formula kama kwenye physics na math's mzee..


Lakini yoote 9, 10 wewe sio muolewaji sheikh..(mnong'onezo)
 
Kwa mara ya kwanza leo ndio nimekutana na Id ambayo si mpya tunapishsnaga nayo majukwaani.
Bila shaka washakuja pm. ukizingatia huna vigezo vingi.
PM hapana hajaja mtu labda ni sababu ya namba ya simu niliyoweka, toka JF kuna kama wawili wa3 hivi, japo katika woote mpaka sasa sijafanikiwa kupata..

Inshaallah nikifanikiwa kupata nitaleta mrejesho.

Sijaja na account fake sababu
1. Sina na sijawahi kuwaza kuwa na akaunt fake
2. Pili nataka waweze hata kufukua makaburi, wanione Makaveli halisi japo kwa uchache kabla hata sijaamua kuigeuzia mgongo dunia. Niko real katika hili, sijaona haja ya kubumba bumba mambo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom