Natafuta Mganga wa Kienyeji Aliye Mkweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta Mganga wa Kienyeji Aliye Mkweli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Feb 16, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Natafuta mganga wa kienyeji aliye mkweli.
  Kwanza sijui kwa kumpata, na wala sijui sifa za mganga wa ukweli, ila wale waendao kwa waganga naomba mnisaidie kwa hili.
  Shida zangu hasa ni:-
  • kuliteka jimbo la uchaguzi wa kijiji nilichotoka ili nikautwae ubunge wa jimbo hilo.
  • kumtimua bosi wangu hapa idarani maana amekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya wafanyakazi wote, anamtumikia zaidi muhindi na anasahau hata kukutetea haki zetu za msingi.
  • awe mshauri wangu wa mambo yajayo na kunisomea alama za nyakati.
  Niko tayari kumpa kiasi kinono yeyote atakaye nisaidia kumpata mganga mwenye sifa hizi.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Well, check na Sheikh Yahya!
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Feb 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Umekosa kazi za kufanya?
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 640
  Trophy Points: 280
  Sumbalawinyo wewe ni mwenyeji wa Sumbawanga? Maana sikuelewi hapa.. Fanya kazi kwa bidii, achana na walaghai
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,940
  Trophy Points: 280
  kwenye maisha
  mganga ni wewe mwenyewe...
  just follows your instincts....
   
 6. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,816
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  pita morogoro road, pale jangwani kuna kibao cha mganga kutoka naijeria, fuata mshale, natumai utafika unakokusudia...kila la kheri na nguvu za giza...lakini kama wewe ni ccm, mtafute mbunge wako na umuulize yeye alifanyaje?
   
 7. F

  Future Bishop Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sumbalawinyo shida ulizoeleza hapa hazitatuliwi kwa kwenda kwa mganga wa kienyeji, angalia ushauri wangu nilioweka katika rangi ya bluu

  Shida zangu hasa ni:-
  • kuliteka jimbo la uchaguzi wa kijiji nilichotoka ili nikautwae ubunge wa jimbo hilo. Mimi sio mwanasiasa lakini naamini kama umekuwa karibu na wananchi wako yaani wanakufahamu vizuri na ukawa na sera nzuri zenye ushawishi na ukagombea kupitia chama kinachokubalika eneo hilo utashinda badala ya kumuamini mganga wa kienyeji kuwa anaweza kukufanya ushinde.
  • kumtimua bosi wangu hapa idarani maana amekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya wafanyakazi wote, anamtumikia zaidi muhindi na anasahau hata kukutetea haki zetu za msingi. Sioni kama njia ya kumtimua bosi itakuwa ni suruhisho la changamoto mnazozipata kazini, huyo bosi anaweza akaondoka akaja mwingine ambaye atakauwa mbaya zaidi. Ni vizuri kuangalia system na mwongozo mzima wa ofisi yenu inawezekana ndio wenye shida. By the way huyo boss ndo wa mwisho na hakuna mtu mwingine juu yake? Usipoteze muda wako, nafsi yako na roho yako kuwaendea waganga wa kienyeji
  • awe mshauri wangu wa mambo yajayo na kunisomea alama za nyakati. Ndugu yangu naomba nikukumbushe maandiko yanasema "AMELAANIWA MTU AMTEGEMEAYE MWANADAMU NA KUMFANYA KUWA KINGA YAKE". Achana na jambo hili njoo kwa YESU utapata raha nafsini mwako na atakupa hakika ya maisha yajayo.
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Kwishnei! Hata uwenyekiti wa mtaa hupati ww.
  Why did I repply this thread? AaGgggrrrrr! Great thinker inataka kuwa kijiwe cha kahawa na bao.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hakuna mgamga wa kienyeji ambaye ni wa kweli.Kwa mtaji huo hushindi ng'o huo ubunge unaoutaka.
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,158
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  .... [​IMG][​IMG]......!!
   
 11. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ni kweli waganga wa kienyeji wote ni waongo na ni watumishi wa shetani. Mwenye kuwategemea anajitafutia mwisho mbaya wa kutapeliwa na kisha kwenda jehanamu.
   
 12. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,931
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  hivi kuna mganga asiyetaka ubunge? sasa kwanini mganga akusaidie wewe kuwa mbunge kwnaini asijisaidie mwenyewe? au ndio mambo ya mganga hajigangi? na kama hajigangi kwanini asienda kwa mganga mwenzake kama yeye ana amini mambo ya uganga haweze kuwa mbunge au tajiri?

  natoka nje kidogo nina swali,kwa kiswahili sanifu kazi ya mganga ni nini? naona kama mleta hoja anatafuta mchawi? au nimekosea wakuu? naona watu siku hizi wanachannganya kati ya mganga na mchawi naomba tofauti ziwekwe mwenye kujua kwa undani?
   
 13. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  kwa kuwangoza wasiyo wachawi huwezi kutumia uganga
  sema tu ukweli kuwa una lengo la kujifunza uchawi
  hizo zingine ni porojo tu, utashauriwaje na kuongozwa na
  nguvu za kishirikina, harafu uwe kiongozi wa jimbo?
   
 14. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,581
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  ........Yesu pekee ndio mganga aliye wa kweli.
   
 15. d

  debora Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  najua huo ni utani lakini serious we christians we believe in bible na bibilia inasema amelaamiwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake kumbe moyoni mwake amemwasi Bwana Yesu. Do bear in your mind kwamba there is no free lunch, shetani hakupi kitu bure bwana utalipa tu whether you like or not. so its your choice kuwa na furaha ya kitambo au kuwa na uzima wa milele.
  mbarikiwe
   
 16. babalao

  babalao Forum Spammer

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 427
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama ukitaka kujua waganga wa kienyeji ni waongo jaribu akupe dawa ya biashara kwani majibu yake ni ya moja kwa moja wengi hawawezi kufanikisha hutoa visingizio oh ulikosea nasharti. Naona wote ni waongo usipoteze muda wako bure.
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  hahaha hehehe leo nimecheka mie sikutegemea kauli hiyo ingetoka kwako wewe sumbalawinyo in my love i will neva neva trust nguvu za giza ,nayaweza mambo yeye katika yeye anitiae nguvu,hivo na wewe mtumaini mungu atakushindia ,waganga wenyewe michosho tupu
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  ...mimi nakushauri kwa nia njema tu, chukua likizo kazini halafu tafuta recreational activities haraka iwezekanavyo, hata kama itakuwa ni kibustani cha mboga mboga.

  Ni dalili za depression hizo, au kwa lugha nyepesi wanaita 'msongo wa mawazo' ndio yanakuandama kiasi kukupelekea kuanza kupoteza self-esteem, au kwa kiswahili chepesi; "uwezo wa kujiamini" .
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Very gud advice mbu
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  NA HAWEZI KUMFANYIA HII KAZI......
  Huyu ndugu anatafuta short cut kuelekea kuwadanganya wananchi wa kijiji chake... na akiupata huo ubunge hatawafanyia chochote wapiga kura bali kujinufaisha yeye mwenyewe.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...