Natafuta mbwa watatu wa kukodi

Natafuta mbwa watatu wa kukodi

Mkuu nianze kukupa pole kwa hasara unayoopata kila mara
Ushauri wangu kwako
Unajua usiongee na watu wa mali asili wakiwa ofisini badala yake
Mpoint yule mwenye cheo kidogo
Kaa nae pigeni story ikibidi mnunulie hata supu wakati mkibadilishana mawazo
Chomekea hiyo mada na atakusaidia kiurahisi kabisa bila tabu

Ukienda ofisini mambo ni mengi

Ni hayo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi huu ulinifanya nipekue nione kana kuna nyoka mnene huo wa foot moja, nikagundua kuwa hupimwa kwa uzito na urefu, ambapo inakadiriwa nyoka mkubwa zaidi ana 222kg na urefu wa feet 30 sawa na mita 9.1.
Pia nikaona na dau sliloweka rais Roosevelt la $1000 na mwisho kabisa $50,000

Sent using Jamii Forums mobile app

Yaani kuna watu bado wanamtafuta wa 30ft [emoji23]
Lakini dunia hii kuna majoka makubwa aisee



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ni maajabu tu ya hivi yanatokea kwenye nchi masikini kuomba hela wakati ni kazi yao
Katika miaka ya 1900 aliekuwa Rais wa USA Roosevelt alitoa dau la $1000 kwa yeyote atakaefanikisha kumkamata nyoka mkubwa wa kufikia urefu wa zaidi ya 30ft
Baadae dau lilipanda na kufika 5000 halafu 15,000 mwaka 1978
Na mnamo mwaka 1980 bila mafanikio dau likapanda mpaka $50,000
Hapo watu zaidi walichangamkia fursa na kwenda mpaka Amazon kupambana na Anacondas ili wapate huo mchongo ambapo watu wengi walipoteza maisha kwa tamaa na bila mafanikio
Sasa sisi huku badala ya idara kusaidia watu wao ndio wanatafuta madili



Sent from my iPhone using Tapatalk
Serikali zetu za kipumbavu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walami utawajua tu. Yaani mmezaliwa clinic mkakulia mtaani. Hata shamba la muhogo hujawahi kuliona. Sasa, nenda huko mikoani. Chatu anammeza ndama bila hata taabu yeyote. Wadhani anakuwa na unene gani kama sio futi 4?? Sikujaliwa kubishana na wasioamini
Ficha aibu yako dogo. We unazijua futi nne wewe?

Nikusaidie tu, mlango standard wa nyumba ni futi tatu sasa umewahi kuona nyoka mkubwa zaidi ya mlango wa nyumba?
 
Ficha aibu yako dogo. We unazijua futi nne wewe?

Nikusaidie tu, mlango standard wa nyumba ni futi tatu sasa umewahi kuona nyoka mkubwa zaidi ya mlango wa nyumba?
We ni kambaku au kambako?? Kama walijua Kambaku lazima utalijua lindama lake lilivyo. Hebu fikiri; Limemezwa na chatu, Je unene wa hilo lichatu utakuwa inchi 2 au 3?? Ungelikuwa unamshonea suruali huyo chatu kiuno ungesema ni inchi 4?? Nadhani hapa asiyejua jinsi ya kumpima unene ni weye
 
Mkuu jaribu kuwasiliana na familia ya Kingunge.
 
Ni maajabu tu ya hivi yanatokea kwenye nchi masikini kuomba hela wakati ni kazi yao
Katika miaka ya 1900 aliekuwa Rais wa USA Roosevelt alitoa dau la $1000 kwa yeyote atakaefanikisha kumkamata nyoka mkubwa wa kufikia urefu wa zaidi ya 30ft
Baadae dau lilipanda na kufika 5000 halafu 15,000 mwaka 1978
Na mnamo mwaka 1980 bila mafanikio dau likapanda mpaka $50,000
Hapo watu zaidi walichangamkia fursa na kwenda mpaka Amazon kupambana na Anacondas ili wapate huo mchongo ambapo watu wengi walipoteza maisha kwa tamaa na bila mafanikio
Sasa sisi huku badala ya idara kusaidia watu wao ndio wanatafuta madili



Sent from my iPhone using Tapatalk
AKIMUUA PIA AKACHUKUA NGOZI NI KESI YA JINAI NYARA YA SERIKALI. HII NDO TZ
 
Mtegeshee mbuzi akimmeza mmwagie Tina atakatika vipande hapo ndo mwisho wa
maisha yake
 
Ishu ni hiyo Jeuri ya kumfuata je anayo?
Kweli watu sasa weshachanganya mambo. Hivi wajua hakuna mdudu rahisi kuua ka chatu aliyemeza kitu?? Sasa kama alimeza kondoo, mbuzi, mbwa huku wewe unamuangalia tu, unategemea aondoke hapo??
Elewa; Chatu akimeza kitu, huongezeka urefu na ukubwa kila amalizapo mlo wake tumboni. Sasa kama alimeza akiwa na unene wa futi 1, mlo wa kwanza, si ajabu sasa ana unene wa futi 2.
Ushauri; Huna haja ya kutafuta mbwa wa watu kuja kuliwa/kumezwa. Kumbuka, mbwa hana ujanja mbele ya chatu, Hutoa harufu fulani inayomlewesha mbwa anajipeleka mwenyewe kumezwa. Endapo atameza kondoo au mbuzi mwingine ngoja akiisha kumuingiza mdomoni tu, hata kabla hajamalizia kummeza, wewe nenda tu na hata panga uanze kumkatakata. hataweza kukimbia wala kumtema kwani meno yake huzuia kisitoke mdomoni bali kiingie ndani. Utakuwa umemuua chatu wako. Ukifanikiwa mrejesho hapa ni muhimu na malipo kwangu nilyekufundisha mbinu hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Happy Boxing Day wana JF.

Naomba niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi wangu. Najihusisha na ufugaji huku kanda ya ziwa ila nina changamoto ya chatu katika eneo langu hali iliyosababisha mifugo 5 kuuliwa ikiwemo mbwa wangu wawili aina ya Germany Shepherd ambao walimezwa katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.

Mbuzi wangu wawili pamoja na kondoo watatu wamemezwa na chatu pia ndani ya mwaka mmoja uliopita. Sasa naona hali inazidi kuwa mbaya zaidi na ninatafuta mbwa watatu ili nione kama wataweza kupambana na chatu huyo.

Hivyo natafuta mbwa wenye nguvu watatu ambao nitawatumia ili nione kama nitafanikiwa kumuua huyu chatu.

Kama una mbwa wenye sifa hizo njoo PM tuone namna ya kufanya biashara.

Muda wa kukaa nao ni ndani ya siku 6 hadi wiki moja moja. Kama watakuwa wamemezwa basi tutarudi kwenye meza ya mazungumzo tuone tunafanya nini.

Karibu wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulifanikiwa kupata mbwa?
 
Back
Top Bottom