Natafuta Mbuzi bora wa Nyama Madume aina ya Savanna na Boar hapa Tanzania

Goat pox sio mapafu mkuu ni ndui ya mbuzi,lakini kuna chanjo za mapafu na ndui unachanja tu kuwakinga.
 
Goat pox sio mapafu mkuu ni ndui ya mbuzi,lakini kuna chanjo za mapafu na ndui unachanja tu kuwakinga.
Nashukuru sana kunisahihisha ila nimezungumzia kwamba nilipatwa na hiyo shida ya GOAT POX, na nikazungumzia kuwa kinga Mbuzi na mapafu, na kuna mahala nimezungumzia chanjo ya CCPP kwaajili hiyo. Kikubwa mimi sikuchanja GOAT POX wala sikuweka Mbuzi quarantine pindi nilipo waleta Mbuzi wapya, kiboko nilicho kipata hakina mfano wake kwakweli, Mungu anajua kwakweli.
Mbuzi wanakufa mpaka unachanganyikiwa.
 
Kwa pwani tufuge aina gani?

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa pwani tufuge aina gani?

#MaendeleoHayanaChama
Inategema na wewe hitaji lako ni mradi wa aina gani,1 wa nyama? kama ni ndio basi anaza na Galla/isiolo ukichanganya na hawa wetu wa kawaida. 2 ni wa maziwa? kwanza nankushauri uangalie soko likoje halafu utembelee wafugaji kwanza na mashamba ya serekali Tarili Mpwapwa na Tanga wao wanao wanao wa cross kwaajili ya ukanda wa Pwani.
0715391788/0784391788. Taliri Tanga hao watakupa mwongozo mzuri wa Mbuzi wanaozalisha na upandaji wa majani ya ulisha Mbuzi ktk shamba lako.
0718312084/0674625420. Taliri Mpwapwa hao pia watakusaidia kuhusu mbegu bora za Mbuzi walio cross na hizo za kisasa watakao kufaa kwa ukanda wa Pwani.
 
Asante sana kwa taarifa hizi muhimu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Asante sana kwa taarifa hizi muhimu.

#MaendeleoHayanaChama
Karibu sana niwaombeeni nyote muwe na baraka za Mungu ktk lile mliwazalo kuanzisha miradi yenu, Mungu Baba awape Nguvu,hekima,busara,nia iliyo njema na mafanikio ktk mashamabayenu mliyoyaanzisha na mtakayo yaanzisha , kikubwa uvumilivu,chanjo na usafi wa mabanda, mbarikiwe sana.
 
Kumbe tuna research centers kama hizi bongo, lakini seems watu hawazitumii inavyotakiwa kujiletea maendeleo
 
Kumbe tuna research centers kama hizi bongo, lakini seems watu hawazitumii inavyotakiwa kujiletea maendeleo
Knowledge is power.

Wao pia hawahangaiki kujitangaza kwa kuwa wanajua watalipwa wafanye kazi au wasifanye. Ikiwa wanafanya utafiti na kuzalisha mbegu bora na soko lipo kwanini wanashindwa kuzalisha. Nadhani ile move ya Magufuli kuwataka watoe gawio serikali kuu ingefaa iendelee
 
Maelezo kamili juu ya upatikanaji wa mbuzi aina ya boer
👇
Sasa yale maswali yote juu ya Mbuzi Boer niwaombeni sana sana ndugu mumfwatilie huyo kaka kwenye kurasa zake mbali mbali kuanzia Facebook, Instagram, YouTube kwajina la Shambani farm mtafaidika sana kwa jinsi ya ufugaji bora na kujua zaidi Mbuzi ni nini. kwangu mimi ni zaidi ya mwalimu,kiongozi na mhamasishaji mahususi juu ya ufugaji wa Mbuzi Tz.
 
Kwa wale walio kuwa wanatafuta. Mbuzi bora wa kufuga kuna ranch moja huko kimanzichana wanauza mbuzi aina ya Galla wenye mimba kwa bei ya shilingi laki 2 na nsu ila mpaka uchukue mbuzi zaidi ya 10.

Kama kubwa mtu anahitaji nadhani tuungane twende kuchukua. Binafsi nina weza kuchukua kuanzia hiyo idadi lakini baada ya kujiridhisha kuwa wako vizuri.

Lingine kuna mtu nimempa Kazi kunitafutia mbuzi wanao zaa mapacha huko Kagera nae kapata hivyo pia kama kutakuwa na watu wako interested tunaweza kwenda kuchuku. Huko bei ni rafiki kwani unaweza kupata kuanzia 40k - 100k. Huku nitakqenda kuchukua mbuzi Kati ya 30 hadi 50. Tukiwa watu wawili watu tunaweza kushare usafiri
 
Kimanzi chana ni Mavuno Farm ni kweli anauza Galla walio pandwa na Boer tayari, 0713282715 nilishawahi weka number yao hapa wasilianeni nao wana Mbuzi viwango kweli.
Kuhusu kagera ni kweli utapata Mbuzi wazuri wanao zaa mapacha mpaka 3 hao wanaitwa Mubende, ila ningeomba nikushauri kitu ktk hao Mbuzi jitahidi sana wakutafutie amabe alisha zaa mara moja au amchukuwe ambae ana watoto wake pacha kabisa ndio inakuwa vyema na ujitahidi sana kuangalia umri maana ukimchukuwa amabae amaesha zaa sana huwa anakuja kuzaa watoto wadhaifu na wanakufa mara wazaliwapo wanakaa muda mchache.
Mubende ni Mbuzi wazuri na wastahilivu sana, nakupongeza sana kwa hilo la kuamua kuwekeza mtumainie Mungu na utafikia malengo yako ubarikiwe sana.
 
Kumbuka channjo na quarantine ni muhhimu sana ndugu hasa utakapo chukuwa Mbuzi wa sehemu tofauti tofauti, kila siku naomba sana Mungu yaliyo nikuta yasimkute wala kumpata mfugaji mwenzangu yeyeyote ktk ufugaji wake, nawaombeeni kheri nyote ktk ufugaji na wote mnao anza kufugaji wenu.
 
Nashukuru sana kwa kutukumbusha. Yaani Kati ya kitu nilicho toka nacho kwenye huu uzi ni hicho cha chanjo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…