Natafuta Mbuzi bora wa Nyama Madume aina ya Savanna na Boar hapa Tanzania

Nipe mawasiliano na kama unawajua fika basi nielekeze ni wilaya gani na sehemu gani ili nitume watu wangu wa karibu walioko Mbeya wakathibitishe
Mkuu ulipata? mimi nafugia Kerege bagamoyo ila mradi bado ndio umeanza nina mbuzi wa nyama mbegu kubwa aina ya GALLA/ISOLO na BOAR nategemea kuzalisha kwanza ndio nianze kuuza
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu, naomba niwape ufafanuzi kuhusiana na Mbegu ya Mbuzi mlizo ziseama, kusema ukweli kabisa kuna watu wanao hao Boer na Savanna hapa Tz ila naomba niwape anagalizo kama kwesi unahitaji kuwekeza ktk hizo mbegu ningeliwashauri kwanza mfanye kutembelea kwanza wafugaji wa hizo mbegu halfu ndio uamue kufuga.
Nazungumza hivyo kutokana na uzoefu wangu ktk ufugaji wa mbuzi na nipo ktk mtandao wa wafugaji Mbuzi Tz, kwa hizo mbegu ningeshauri uwasiliane na Mbogo Ranches ndio pekee weney uhakika wa hizo mbegu. Shamba lao lipo Mdaula hapo, na ukiingia Instagram utawakuta utaona kila aina ya Mbegu walizo nazo na utawasiliana nao hao.
Kuhusu ugaji wa Mbuzi wa Nyama nitawashauri uanze na Galla/Isiolo wana faa sana kwa Nyama na soko letu la kawaida. mliopo Ngara fugeni Mubende ukiwa cross na Galla/Isiolo mtapata matokeo mazuri sana.
Mlioko kigoma Fuga Buha nao niwazuri sana kwa ukuwaji na kuzaa vyema wote hao huzaa mapacha mpaka 3.
Ukihitaji ufafanuzi zaidi utauliza.
 
Magharibi ipi mi ndo nimemaliza mabanda Ngara. Wilaya ya Longido nimewaona mbuzi wazuri weupe breed ya Kenya nimesahau jina, ni Wakubwa kama hizo breed ulizotaja ila hawana complications, ni kama local breed. Sasa kuwafikisha magharibi ndo sijui.
Hao mbuzi asili yao ni Kenya eneo la Isiolo, hao wanaitwa Siolo, wanazaa mapacha mara nyingi na wanakua kwa haraka.
Ni mbuzi wa nyama na maziwa.
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu, naomba niwape ufafanuzi kuhusiana na Mbegu ya Mbuzi mlizo ziseama, kusema ukweli kabisa kuna watu wanao hao Boer na Savanna hapa Tz ila naomba niwape anagalizo kama kwesi unahitaji kuwekeza ktk hizo mbegu ningeliwashauri kwanza mfanye kutembelea kwanza wafugaji wa hizo mbegu halfu ndio uamue kufuga.
Nazungumza hivyo kutokana na uzoefu wangu ktk ufugaji wa mbuzi na nipo ktk mtandao wa wafugaji Mbuzi Tz, kwa hizo mbegu ningeshauri uwasiliane na Mbogo Ranches ndio pekee weney uhakika wa hizo mbegu. Shamba lao lipo Mdaula hapo, na ukiingia Instagram utawakuta utaona kila aina ya Mbegu walizo nazo na utawasiliana nao hao.
Kuhusu ugaji wa Mbuzi wa Nyama nitawashauri uanze na Galla/Isiolo wana faa sana kwa Nyama na soko letu la kawaida. mliopo Ngara fugeni Mubende ukiwa cross na Galla/Isiolo mtapata matokeo mazuri sana.
Mlioko kigoma Fuga Buha nao niwazuri sana kwa ukuwaji na kuzaa vyema wote hao huzaa mapacha mpaka 3.
Ukihitaji ufafanuzi zaidi utauliza.
Isiolo ninao japo ni mfugaji mpya
 
Hao mbuzi asili yao ni Kenya eneo la Isiolo, hao wanaitwa Siolo, wanazaa mapacha mara nyingi na wanakua kwa haraka.
Ni mbuzi wa nyama na maziwa.
Nikweli unacho kisema lakini hao wanao zaa mapacha ni wali Cross walipo kuja kenya, asili kabisa ya hawa Isiolo ni kuzaa mmoja, na nakubaliana na wewe kabisa waliingizwa Kenya kwanza kabisa ktk kaunti ya Isiolo.
Ni kweli ukuwaji wao ni wa haraka na wana jaza nyama vyema ktk miili yao.
Na niwavumilivu sana ktk hali ya hewa hasa hiki kipindi cha ukame,
Na niwavumilivu sana kwa magonjwa ila wakipata ile homa ya mapafu hawapindui.
Nina ushaidi ktk shamba langu nilipatwa na mkasa wa GOAT POX ugonjwa huu uliua Mbuzi wengi sana shambani kwangu lakini jamii ya ISIOLO/GALLA hawakudhurika na huo ugonjwa.
Nilikuwa na Mbuzi 168 nimebakiwa na Mbuzi 15 kwa sasa,
Chanjo na tiba ni vitu muhimu sana ktk ufugaji wa Mbuzi, na quarantine pindi unapo ingiza mfugo mpya ktk zizi lako.
 
Asante sana Ndugu yangu kwa kunishauri vizuri. Nitatafuta mawasiliano yao ila sema Taasisi zetu huku Tanzania zimelala.
Yaani hata hawajitangazi sijui wanataka nini.

Hawa ndugu zetu waganda wametupiga bao. Mfuatilie huyu jamaa Hamiisi Semanda kwenye youtube utapata kitu.
Yep, yule mganda anatoa elimu nzuri sana na inaonekana mbuzi wanaweza kukupa kipato kikubwa sana ukifanya inavyotakiwa, na kuna mwingine wa Ghana lakini yeye ni samaki, seems hivi vitu mtu ukiamua kujiajiri na ukawa serious unaweza kuwa better kuliko kuajiriwa na mtu,napenda kuangalia hawa watu kwenye youtube, Africa kuna namna nyingi sana ya kutokuwa maskini, ningekuwa siko busy na mambo yangu ningefanya hayo mambo na nina uhakika nisingepiga pesa ya kutosha tuu
 
Kwa kweli ufugaji wa Mbuzi ni mzuri sana kikubwa ni kupata vijana waangalifu na wenye kuupenda ufugaji, maana changamoto inayotukabili ni kuwa bado tupo kwenye ajira za watu sasa vijana ndio huwa wanatuangusha sana.
Ingia mwenyewe polepole kama unaogopa kuacha ajira yako, kwa mishahara ya watu wengi wa bongo naona kama ukiwa serious na hivi vitu unaweza kutengeneza kuliko ajira za kuajiriwa
 
Nawasaalimuni nyote kwa jina la Mungu, naomba niseme kitu hapa Mimi binafsi nimeshaingia na kufanya ufugaji kwa muda mrefu sasa na nimeshaona faida yake, changamoto zake,na utendaji wake wa kina, nachopenda kusisitiza ni nidhamu inahitajika sana pindi unapoianza hii kazi ya ufugaji, maana miiko mikubwa sana ya fuguaji ni Ulinzi, Usafi, Tiba stahiki, Kuwa na mbegu bora, Eneo na vifaa stahiki kwaajili ya mifugo yako.
Mara nyingi sana napenda kuwa shauri watu pindi unapo taka kuanza ufugaji ujipe muda wa kufanya utafiti wa kutosha na ukiweza kutembelea wafugaji walio tangulia inakusaidia kujua nini mawazo yako ya lipoko na utapata walao lakuongezea ktk wazo lako la ufugaji.
Kabla sijapata shida ya kuuguliwa na mifugo nakumbuka nilialika baadhi ya wana jukwaa humu kwaajili ya kuja kujifunza na kubadilishana mawazo ktk ufugaji na kuweza kupeana njia mbali mbali juu ya ufugaji. Tukishirikiana na kupendana kuvumiliana na kugawana kile tulicho nacho naamini tutafika malengo yetu kwa jina la Mungu. Mbarikiwe nyote.
 
Hawa ni baadhi ya mifugo niliyo kuwa nayo.

20210306_143953.jpg

20201205_151138.jpg

20210306_143956.jpg
 
Back
Top Bottom