Natafuta mavazi ya kuvuna(kurina) asali

de brazza25

Member
Apr 22, 2017
48
34
Habari wanajamvi,

Naomba niende moja kwa moja kwenye swali langu, hivi ninawezaje kupata mavazi ya kuvuna asali?

Wakuu habari zenu wote. Ndg zangu naombeni msaada wa kunijulisha wapi naweza pata kununua mavazi ya kulinia asali.
 
habari wanajamvi. naomba niende moja kwa moja kwenye swali langu ivi ninawezaje kupata mavazi ya kuvuna asali
iloh tu wakuu
Mwone Mwl.RCT akuagizie hizi protective gear au kama unaweza fanya manunuzi mwenyewe fanya.
s-l500.jpg

Link
 
Niliwahi vuna asali kienyeji Kwa kuvaa gunia, asali tamu ila wale wadudu wabaya sana. Sikutoka salama.
 
Wakuu habari zenu wote. Ndg zangu naombeni msaada wa kunijulisha wapi naweza pata kununua mavazi ya kulinia asali.
 
mara nyingi maliasili wanakuwa na vifaa kama hivyo,jaribu kufika ofisi ya karibu ya maliasili iliyo jirani nawe
 
Home kwetu kuna nyuki wengi sana sana tatizo tulilo nalo ni uhaba wa mavazi. Huwa naumia kuona walinaji wa nyuki huko home wanatumia moto na dawa ya rungu na kuangamiza nyuki wengi sana. Nataka tem hii mara niendapo nibebe mavazi hayo kwa ajili yangu na hao wenzangu.
 
Aisee dawa ya rungu ni sumu mzee, kemikali yoyote inayoua viumbe hai haifai kuchanganywa na chakula, madhara yake yanaweza yasionekane sasa hivi ila wanaweza kuja kupata cancer ama kujifungua watoto wa ajabu, kawape elimu hii mkuu
 
Nashukuru sana mkuu. Ntajitahidi sana kwenda kutoa elimu. Ujue pia kwa kutumia dawa ya kuua wadudu au moto wanaangamiza raslimali na utajili wa nchi yetu. Ni sawa na mtu anaeua tembo wetu huko mbugani.
 
Ndio, pamoja na hilo..msisitizo wako unapaswa kuwa kwenye afya zao kwanza ndio watakupa attention, maana sijui kama watu wa vijijini watakuelewa kirahisi kuhusu kuhifadhi wadudu ama wanyama pori
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom