Natafuta Mashine ya Interlocking Bricks (Tofali Za Kufungamana)

Natafuta Mashine ya Interlocking Bricks (Tofali Za Kufungamana)

Gien Banks

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
336
Reaction score
891
Shallom / A.Salaam Aleykum

Husika na Kichwa Cha Habari Hapo Juu.

Nimekua interested na teknolojia ya ujenzi wa kitumia interlocking bricks kwani seems ina faida nyingi kuliko tofali za kawaida

1. Huokoa gharama za ujenzi i.e. Cement / Mchanga / Finishing.

2. Sehem yenye kupata material za ujenzi unaweza fyatua tofali mwenyewe ukauza kwa wengine au hata kutumia mwenyewe..nk

3. Fitting of Wires and Plumbing ni Rahisi. Na hata plastering si lazima kwenye kuta za nyumba.

Naombeni kujuzwa pa kuzipata hizi mashine...na bei zake. Wengi wao wanaouza mitandaoni janja janja nyingi + hawako straight.

Ushauri / Maoni / Maelekezo Ni Mbolea Sana Kwenye Hii Topic. Karibuni Tujadili Wakuu.

Natanguliza Shukrani Nyingi Kwenu.

Thanks
 
Anzia SIDO unaweza kupata muongozo.

Licha ya Mashine Tu (Ushauri Pia ni Mbolea)
Kuna Hydraform Interlocking Bricks na Interlocking Bricks (unaweza google chap chap kuona utofauti, zote zina almost faida sawa sawa if not completely the same but different material and shape)

1. Differences (Zitahitaji Vibao Vya Mbao au Bila Vibao Vya Mbao)

2. Prices za mashine ( Kuna Tofauti Tofauti + Ubora Kwa Waliotangulia Kuzitumia)

3. Sido na Watengenezaji Wengine (Tofauti Zao)

4. Ratio Za Matofali (Mixing Materials + Cement Ratio). Interlocking nyingi zinatumia udongo, je nikitumia mchanga na cement kama tofali za kawaida ila kwa muundo wa interlocking nitatoboa ?? If not Why ??

5. Kwann Matofali Mengine Baada ya Muda Yanamomonyoka ?? Je ni poor ratio / mixing / ubora wa Mashine ?? Cz Kuna Bricks zenye Blind Holes na kuna zenye Through Holes, Zipi ni Bora ?? This therefore defines the machine specifications.

Yani Full Details Na Ndio Maana Hii Mada Nimeileta Hapa Kwa Wajuzi, SIDO nitakwenda ila tuanze hapa kwanza ili nikienda kule niwe na maswali na uelewa flani concrete na Kabla Sijaanza pia Kuzitafuta Uraiani Huko.

Si Wajua JF is some sort of a Hustle Guide

Karibuni.
 
Licha ya Mashine Tu (Ushauri Pia ni Mbolea)
Kuna Hydraform Interlocking Bricks na Interlocking Bricks (unaweza google chap chap kuona utofauti, zote zina almost faida sawa sawa if not completely the same but different material and shape)...
Haya wacheki wabrazil Hawa wanazitengeneza hizi machine ila bei zao zimechangamka
View attachment Catalogo Verde 2020.pdf
 
Ok. Hapo bongo vp ?? Any connects ??
Hapa bongo labda ucheki na mechanical workshop kubwakubwa wanaweza kukutengenezea kitu quality, ninayo machine mmoja nilitengeneza hapa nchini kiukweli quality yake haikunivutia pamoja na kuwa nilimpa design
 
Duuh ila end products vp ?? Tofali ulipata yenyewe ?? Na we pia umejenga kwa interlocking bricks ?? Nakuskiza Chief.
 
Duuh ila end products vp ?? Tofali ulipata yenyewe ?? Na we pia umejenga kwa interlocking bricks ?? Nakuskiza Chief.
Ili upate product nzuri basi Kuna mambo kadhaa hakikisha unayafuata

1. Uchaguzi wa udogo
2. Machine
  • Manual or Automatic interlocking bricks Machine
  • Soil crusher machine
  • Soil sieving machine or sieving
  • Concrete Mixer
3. Laboratory Kit
  • Laboratory kit hapa nazungumzia zile chekeche kama zile wamama zamani walikuwa wanachekechea unga kwajili ya kutambua soil content
  • Beaker or Mizani zile ndogo napendekeza digital

Uchaguzi wa udogo
Udogo unatakiwa uwe na content ya soil around 60% to 70 % ili iweze kubond vizuri na cement na pili iwe rahisi kutoa tofali kwenye mold baada ya compression

Mixing ratio
Udongo 8 to cement Moja
Wakati wa kumix material yako maji yanatakiwa ni kidogo sana yaani iweze kutengeneza kitu kama tonge like kama la ugali

Mengine wataongezea wengine. Naandika nikiwa sijatulia
 
Shallom / A.Salaam Aleykum

Husika na Kichwa Cha Habari Hapo Juu...
Mkuu, hizi machine zipo. Zilikuwa zinauzwa na Agency ya serikali (NHBRA) iliyokuwa chini ya wizara ya Ardhi, ila Agency sasa imebadilishwa jina. Ofisi zao ziko Mwenge (Karibu na Hospital ya Lugalo/mlalakuwa).
Nahofia hata hapa unaweza kukutana nao..!
Mbwange, kwa kusema "unaweza" unakuwa sahihi sana. Maelezo niliyompatia ni ya hakika kabisa.
 
Kaka nakuomba uki settle urudi please. Ur content is highly appreciated. Many Thanks.
 
Mkuu, hizi machine zipo. Zilikuwa zinauzwa na Agency ya serikali (NHBRA) iliyokuwa chini ya wizara ya Ardhi, ila Agency sasa imebadilishwa jina. Ofisi zao ziko Mwenge (Karibu na Hospital ya Lugalo/mlalakuwa).

Mbwange, kwa kusema "unaweza" unakuwa sahihi sana. Maelezo niliyompatia ni ya hakika kabisa.

Bei za mashine zinakwendaje ??
 
Naombeni kujuzwa pa kuzipata hizi mashine...na bei zake. Wengi wao wanaouza mitandaoni janja janja nyingi + hawako straight.
Nahofia hata hapa unaweza kukutana nao..!
Jaribu pale BICO, UDSM. Kama hawana au hawazitengenezi, basi uhakika ni kuwa wanajua mahali zinapopatikana
 
Back
Top Bottom