Ndugu zangu naomba msaada wa gharama za tofali endapo nitatengeneza mwenyewe

StanyHD

Member
Mar 31, 2018
25
12
Ndugu zangu naomba msaada wa gharama za tofali za block endapo nitatengeneza mwenyewe na sio kununua. Juz nilienda kijijini kwetu ambako nataka nianzishe mradi wa kufuga nguluwe, hivyo nikaenda kuuliza bei ya tofali za block kwa ajiri ya ujenzi wa mabanda na nyumba ndogo ya wafanya kazi,cha kushangaza bei ya kule n tsh 2500 kwa tofali moja bei ambayo kwangu niliona n kubwa mno na kuamua kutengeneza hizo tofali ili nipunguze gharama ukizingatia nahitaji nyingi tu.

Kwa anayejua naomba kujua bei ya mashine ya kutengeneneza zile tofali, ile ya mkono tu sio ya umeme, pia nahitaji kujua mfuko mmoja wa cement unatoa tofali ngapi,na gharama zingine zote zinazohusisha kazi hiyo. Natanguliza shukrani
 
Mfuko unatoa matofali imara kuanzia 45 yasizidi 60 kwa mfuko wa sementi m'moja.

Tafuta fundi, bargain nae bei ya tofali moja piga jumla ya idadi ya tofali unahitaji utapata idadi kamili.
 
Mfuko unatoa matofali imara kuanzia 45 yasizidi 60 kwa mfuko wa sementi m'moja.

Tafuta fundi, bargain nae bei ya tofali moja piga jumla ya idadi ya tofali unahitaji utapata idadi kamili.
Nimependa wazo lako
 
Back
Top Bottom