Natafuta kwale, bata mzinga na kanga wakufuga.

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,160
1,717
Habari wadau. Niko dar mpaka tarehe 26. Kama kuna mtu anayeuza hao viumbe hapo juu kwa ajili ya kufuga naomba anicheki.
 
bluetooth 1.eti bata mzinga kuanzia mtoto hadi mkubwa (yani ready for kuliwa) anachukua muda gani?kama ukimpa matunzo stahiki

2. Naskia malezi ya bata mzinga ni ya changamoto kuzidi kuku wa kisasa, je kuna ukweli?

Thanks
 
Last edited by a moderator:
bluetooth 1.eti bata mzinga kuanzia mtoto hadi mkubwa (yani ready for kuliwa) anachukua muda gani?kama ukimpa matunzo stahiki

2. Naskia malezi ya bata mzinga ni ya changamoto kuzidi kuku wa kisasa, je kuna ukweli?

Thanks

Bata mzinga huchukua miezi sita na nusu mpaka kukomaa au kupevuka na kuanza kutaga-huo ni umri mzuri kwa matumizi ya nyama
Bata mzinga hana complications katika utunzaji wake kama watu wanavyosema

Bata mzinga hutaga mayai 100 kwa mwaka na mzunguko wake ni zaidi hata ya kuku Changamoto ya bata mzinga ni ugonjwa wa ndui (fowl pox) ..... unatakiwa kuwapa chanjo wiki ya pili tena kwa dozi kubwa .... matunzo ya bata mzinga kwa free range huwa na matokeo mazuri sana

Important fact:
dume wa bata mzinga hupoteza hamu ya jike ndani ya siku tano anapokuwa anaishi naye hivyo unabidi kuwa na madume uliyoyatenga kubadisha kwa majike ili uweze kuwa na mbegu katika yai la bata mzinga (egg fertility) .... bata mzinga anatabia ya kuwa na wivu na hasira kali sana dhidi ya mwingine

Bata mzinga anakula mazagazaga na mabaki yote ya chakula cha binadamu pia majani ni virutubisho vizuri sana

Karibu sana
 
Last edited by a moderator:
Kanga ninao wakubwa na wanataga wapo wengi ila naweza kukuuzia kumi tu

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kware tunao kama utahitaji. Piga simu 0715 284 187. Tuko Mbezi Luis. Mayai pia yapo . Bei 20,000.00 kwa "tray"
 
Back
Top Bottom