Habari zenu wakubwa, mimi ni mwenyeji wa Arusha, ila nina trip nyingi sana za Dar Es Salaam, nimefikiria si mbaya kama nitakuwa na kaenea na kujenga kajinyumba kangu kadogo kakufikia Dar Es Salaam, sasa basi niko na msako wa Eneo Dar kati ya maeneo yafuatayo: Tabata - Kimanga au Kinyerezi, Mbezi ya Tegeta, African yote, Tegeta Yote, Bunju .....
Nina ka budget kangu kadogo tu, between 4m - 5m. Ahsanteni.
Huwezi amini wabongo saizi wanaijua ardhi kuliko hata waarusha tena. Kwa bei hiyo maeneo hayo uliyotaja itakuwia ngumu, hebu uongeze kuanzia million 7 na kuendelea ndiyo angalau unaweza kupata kwa kubahatisha maeneo hayo.
Kuna viwanja vya bei hyo maeneo ya Vikunai. Karibu na kota za NSSF mtoni kijichi
Naomba maelezo zaidi,nami nimekuwa interested..Kuna viwanja vya bei hyo maeneo ya Vikunai. Karibu na kota za NSSF mtoni kijichi
Wazee Nashukuruni sana, nimepata Tabata Kinyerezi for 5m, hapajajengwa sana ila sio issue patajengeka tu, namaliza biashara kesho narudi kwetu Arusha KUJIPANGA, like linaendelea wazee.
Mambo vp ?
Nina kiwanja segerea mzimuni nakiuza 6.5million bei ya biashara. umeme upo karibu na majirani wa ukweli.
Mzimuni kwa 6.5 mbona bei sana?
Lile si bonde ndugu yangu?