Naomba kuuliza kitu kuhusu hii minada ya hapa Dar es salaam?

Tanki

JF-Expert Member
Apr 7, 2013
491
189
Ok, ni hivi wakuu, Kuna hii minada huwa inafanyika kwenye eneo husika Kwa siku maalum. Kwa mfano najua Kwa huku Dar es salaam Kila Ijumaa mnada huwa upo Kitunda, Jumanne huwa upo Kivule sokoni, Jumatatu ni Tabata Kinyerezi, Na Kuna siku huwa upo Tabata segerea Kwa mbele kule sijui ni Tabata bima pale ( sijui ).

Swali langu: Je, from no where tu naweza kwenda kuweka biashara yangu kwenye eneo na siku husika?.
Kuna taratibu za kujiunga Ili niwepo kwenye Kila mnada?. Taratibu zikoje, na kama Kuna gharama zikoje?.

Nipo Dar es salaam Tabata Kinyerezi.
 
Hakuna utaratibu wowote ,fika unapoona kuna uwazi wa wewe kuweka chako ,ongea na hao majirani wa sehemu husika,wakikuambia fresh ,Basi tandaza biashara,Ila jioni ukimaliza ,watakufuata na wewe uchangie Pato la nchi,sio Ela nyingi inategemea na sehemu husika,wanapita kwa kila mtu kukusanya ushuru
 
Kuna utaratibu wa kufuata.
Huwezi tu kuvamia eneo kwa kuwa lipo wazi(hasa ukiwahi).
Maeneo yapo, meza zipo na vyote vinalipiwa gharama kidogo tu pamoja na ushuru wa serikali.
Cha kufanya kama unahitaji kufanya biashara onana na wenye matoroli ya kubebea mizigo kwenye mnada husika, wao wanajua leo mtu fulani anaembebea mzigo wake haji watakuonesha eneo lake au kukuunganisha nae ili akuachie kwa siku husika n.k.
 
Back
Top Bottom