Natafuta jimbo la kugombea mwaka huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta jimbo la kugombea mwaka huu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bandorajr, May 24, 2010.

 1. B

  Bandorajr Member

  #1
  May 24, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninaitwa Bandora ni kijana niliye tayari kwa kulitumikia taifa langu....Baada ya kutafakari kwa mda mrefu juu ya namna ya kulitumikia taifa hili nikaona njia iliyo rahisi na wazi ni kupitia nafasi ya Ubunge.
  Sababu kuu ni:
  ...Kwanza ninasifa zinazo takiwa kuwa mbunge.
  ...pili ni naamini ili kuwa mbuge huhitaji mtaji maana mbunge anachaguliwa na wananchi.
  ...Tatu ninaamini mwaka huu ni mwaka wa vijana kushika hatamu.
  ....Nne na mwisho mimi siyo fisadi wala sina historia hiyo na sitegemei kuwa fisadi.

  Majimbo:
  Majimbo ninayo hitaji na ninayoona ninaweza kushinda bila kutumia fedha zozete ni:-

  1.BUSANDA
  2.ARUSHA MJINI
  3.BUKOMBE
  4.GEITA MJINI
  5.KINONDONI
  6.SENGEREMA

  Ninacho hitaji:
  Kwanza ninaomba wana jm mnisaidie kuchagua jimbo kati ya hayo niliyo yaorozesha hapo juu.
  Pili ninaomba mnisaidie kuchagua chama ambacho mnadhani ninaweza kushinda kwa urahisi na bila matatizo .
  Mwisho
  Nimatumaini yangu kuwa mmtanipa maoni na ushauri ambao utapelekea mimi kuwa mbunge mwaka huu...

   
 2. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwanza eleza unataka ubunge ili ukawafanyie nini watanzania??
   
 3. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ulijiandaa kweli hadi sasahivi haujapata mwelekeo wa wapi ukagombee, strategy gani umeplan,
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  May 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Mkuu hapa hamna anaye kujua kwa hiyo hakuna ambae ata kuambia wapi una kubalika zaidi. Nadhani mwenye jibu zuri la wapi una kubalika ni wewe mwenyewe. Mkuu processs ya kugombea ubunge haianzi mwaka wa uchaguzi ina anza kabla. Kama una nia ya kweli nakushauri ujiandae kwa mwaka 2015.

  Pia ubunge una hitaji mtaji mkuu asikuambie mtu. Una hitaji political and economic capital. Kusema haina gharama yoyote ni makosa makubwa sana na hichi pamoja na kuto kujua jimbo gani una weza kushinda mpaka muda huu inaonyesha hauja fanya research kabisa.

  Mwishoni niseme nime sikitika kusoma kwamba unaomba ushauri wa chama gani ugombee kita kacho kuwa rahisi zaidi kushinda nacho. That is wrong. Ingi kwenye chama kwa sababu una mapenzi nacho na una kubaliana na itikadi zake. Niamini ukienda kwenye chama ilimradi tu kushinda una weza ukawa na mafanikio mwanzo uka pata ubunge lakini mbeleni mambo yaka kushinda. Na kwa bahati mbaya umeonyesha kwamba you want to win at any cost even if it would mean selling your soul to the devil.
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  May 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Huyo jamaa ni sawa na kuku aliyekatika kichwa... Hajui asemacho, wala atakalo!
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Umechelewa kwa hivi sasa itabidi ujiunge na moja kati ya vyama hivi Viwili CCM AU Chadema Kisha kujiunga na hicho chama kwa Ushauri wangu itabidi kwanza uwe Mwanachama Muaminifu Mzungumzaji Mzuri katika chama, na ujiandae kwa kugombea Ubunge sio kwa mwaka huu ungoje mpaka Mwaka 2015 ili wapate Wananchi kukujuwa vizuri kisha pia utueleze umesoma mpaka Darasa la ngapi?ulisha wahi kuwa Kiongozi kataka sehemu yoyote iwe ya kazini, au Shuleni? itabidi utowe ufafanuzi zaidi ili Watu wapate kukujuwa maana unataka kuingia Mambo ya Siasa na Siasa ni ngumu itabidi utakabiliwa na mambo magumu kuhusu Siasa na itabidi ukabiliane nayo kwa hali na Mali. na ikifika Wakati wa Uchaguzi itabidi ukagombea Sehemu ulikozaliwa ndio waweza kupata Ubunge Kiurahisi kwa sababu Sehemu ulipozaliwa wewe ndipo Wananchi wengi wanaokujuwa unaweza kupata kura nyingi katika Uchaguzi wa Ubunge unaotaka Huo ndio Ushauri wangu mimi mnasemaje wana JF Wenzangu?
   
 8. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Nimesikitika kubaini kuwa Majimbo ya Mkoa wa Mara hayamo katika chaguo lako. Lakini nakushauri uongeze jimbo mojawawapo la Mkoa wa Mara hasa Tarime au Rorya au Musoma Mjini. Kule nina uhakika utachukua kiulaini hasa kupitia CCJ.
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Kaka hadi muda huu huna uhakika hata jimbo gani unakubalika na kwa chama gani? mchakato kama huu ulitakiwa uufanye miezi 9 iliyopita, sidhani kama una nia kweli ya kuwa kiongozi wa watu - nina mashaka.

  kwa muda uliobaki fikiria kuomba nafasi na kiongozi wa mtaa, then after 5 years utajipima na ujue umesimama kivipi?
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kaka Bandora hongera kwa uamuzi wako kama sifa unazo na unajiamini fanya hima ..Unagombea kwa Ticket ya chama gani?
  Nadhani Majimbo yanayokufaa ni Bukombe,Busanda na Sengerema hayo mengine sidhani ..
   
 11. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135  Kaka tafuta kazi nyingine ufanye, hufai na hatuhitaji viongozi wa aina yako, uwe fisadi ama si fisadi, hatutaki ujasiliamali kwenye siasa zetu.... Period!

  Kwa taarifa yako, wabunge tunaowahitaji ni wale wanayoyajua kwa undani matatizo ya wananchi anaotaka kuwawakirisha na anayetarajia kuyatatua.. tunachotaka kutoka kwake katika kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi ni kutuelezea ni namna gani atayatatua in a simple and practical way, kama mpaka sasa haujaamua utagombea jimbo gani na unataka miezi mitano ijayo tukupe ridhaa yetu.. ili kusudi iweje??? Ukanunua li-Vx ututimulie vumbe au ukaanze kusinzia na kupiga makofi mjengoni???
   
 12. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Yaani unataka kugombea ubunge na unataka sisi tukuchagulie jimbo [you must be joking] mimi nilidhani wale ambao watakaokupigia kura na kukuwezesha kushinda ndiyo wakuamua wewe ugombee jimbo lipi. Ushauri wa bure, tembelea hizo sehemu ulizozianisha kwamba unaweza kushinda halafu kutana na wapiga kura [ambao ndiyo waamuzi wa mwisho] halafu uamue jimbo la kugombea.
   
 13. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,717
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160


  Kagombee kwenu mkuu...najua utasema sheria inakuruhusu...ni kweli..lakini si ni kweli pia kuwa wema huanzia nyumbani????

  huhitaji chama mkuu...kagombee kama mgombea huru laa kama itashindikana...chaguo la chama unalo mwenyewe...tazama dhamira yako inakuongoza wapi na chama kipi kitakusaidia kutimiza hiyo dhamira!!!!
   
 14. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Uchaguzi unafanyika sio zaidi miezi MITANO ijayo, wewe Bwana Bandora mpaka sasa hujajua jimbo la kugombea wala hujui ugombee kupitia chama gani!!!!!!!. Wewe Hufai sio tu kugombea ubunge hata kuwa mbunge wa bunge letu. Wewe unafaa sana kuwa Mwana JF Mchekeshaji
   
 15. babalao

  babalao Forum Spammer

  #15
  May 25, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu unaonekana hujajiandaa. Kuna msemo wa kisiasa unaosema kwamba kanzu ya ijumaa inafuliwa alhamisi hivyo kwa uchaguzi huu umechelewa. Jiandae 2015, muhimu jua ni chama gani kinachokufaa ambacho unakubaliana na itikadi yake, pili jiandae kwa pesa hakuna bure katika uchaguzi kuna gharama mfano ukigombea CCM Unatakiwa uwe na sh. 100,0000.00 za kuchukulia fomu, kuna gharama zingine za usafiri utakapokuwa unajenga mtandao wa watu wa kukupigia debe, na wewe mwenyewe kutembelea wapigakura. Jee utatembea kwa miguu? Mimi ni mwenyeji wa Bukombe nakutahadhalisha usije huku kichwa kichwa utaambulia maumivu, kwanza hujulikani kwani huko unakoishi au ulikotoka ni wapi? kwa nini unakimbia huko kwenu wanakokujua na kukimbilia Bukombe unafikiri huku ndiko kwenye watu waliosinzia unajisumbua.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu kwa kifupi hufai kabisa maana unatamani kuwa mbunge kwa gharama zozote ingawa hujaweka wazi! Hayo maeneo yote yako na mahitaji tofauti wananchi wapiga kura wanahitaji.

  1. BUSANDA
   2.ARUSHA MJINI
   3.BUKOMBE
   4.GEITA MJINI
   5.KINONDONI
   6.SENGEREMA
  Kifupi uko kama mwanamke malaya kokote kwenye ulaji unatoa vitu. Kwani ni lazima uwe mbunge ? kama unania kweli anza kusaidia kwa utashi ulionao badala ya kujiingiza kwenye siasa ambazo huziwezi
   
 17. B

  Bandorajr Member

  #17
  May 26, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thats what I was looking.......Its all about challenges.

  What can you say about Zitto's statement that he still looking for the constituency? yes, bado hajafanya confirmation where to contest.
  Everyone knows Tanzanian politics,unaweza tangaza leo nagombea sehemu fulani then next day unaitwa marehemu au hayati(inspite ktk movements we don't care)..so inawezekana sijaweka bayana and am waiting to be surprise kwa we jimbo nitakalo gombea......
  But thanks kwa wote mlio-comment about ma' Post...
  Harakati zinaendelea
   
 18. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe Bandorajr: yaani una nia ya kugombea lakini hujui chama cha Kugombe??? Hebu Ondoa upuzi hapa! Kama kweli una nia Ungesha identify ni chama Gani kina sera nzuri. Inaonyesha wewe unakimbilia Ikulu wewe "" Hivi ikulu kuna nini? Hivi Ubunge unanini ??? Kila mtu sasa anaonyesha nia?!
   
 19. babalao

  babalao Forum Spammer

  #19
  May 27, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu it seems you are not serious. Unaogopa kuuwawa? Hupaswi kuogopa kitu kama una nia njema na unataka kutetea haki mungu atakulinda
   
 20. MANI

  MANI Platinum Member

  #20
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Kama sio mwanchama wa chama chochote mpaka sasa itakuwia vigumu kugombea naona waliopendekeza 2015 wako sahihi anza kujiunga na chama kwanza ujijenge halafu uongozi baadaye.
   
Loading...