Natafuta data za mvua na joto ya kila mwezi kwenye mikoa ya Kagera, Dodoma, Tanga kuanzia 2006 mpaka 2016

Mkuu natumia laptop na wifi halafu nipo nje ya nchi. Nawezaje kupata kwa njia nyingine?
Siyo rahisi kuzipata online. Zile zipo kisheria na ili kuzipata ni lazima ufuate utaratibu kwa kuwasiliana na sehemu husika ambayo ni Tanzania Meteorological Agency
 
google inafanya nini,? mamlaka ya hali ya hewa haiwezi kosa data sahihi tembelea website yao au mwano awafuate walipo ni majukumu yao kutoa msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
Website nyingi za serikali hii hazina data na nyingi ya data ziko kwenye papers na hawazitoi kirahisi rahisi.
Kwenye website hatazipata aende ofisini Moja kwa Moja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mtoto hakupenda kufanya huu utafiti ila prof. wake kamsahauri kama siyo kumlazimisha afanye huo maana anatoka Tz.
Mwanangu amechanganyikiwa inabidi aje Bongo wakati mimi nipo porini kwenye misitu halafu hana wa kumsaidia ndo maana nikaomba msaada ndugu.
Pole sana. Wasiliana na Afisa wa kitengo cha Customer care. Namba yake ni 0754275571. Huyu atakushauri namna ya kulipia na kupata data zako bila kulazimika kuja TZ.
 
Wana jamvi, naomba msaada wenu kupata hizi data za joto na mvua kuanzia 2006 mpaka 2016. Sipo nyumbani ila mwanangu anafanya research yake ya masters na professor wake anataka afanye hiyo kwa masters yake. Nisaidie ndugu zangu ningekua nyumbani ningekwenda kwa wahusika ila nipo porini. Please help my son. You will never know anaweza tusaidia sote kwenye haya matatizo yetu. Please.

Natanguliza shukrani zenu kwa wale watakaokunwa na hili.
Mfanya masters ni mvivu au?
Anashindwa tafuta taharifa?
 
Data hizo pia unaweza kuzipata ofisi za Mabonde zilizo kila mkoa ofisi hizi zipo chini ya Wizara ya Maji
 
Hayo ni mapenzi ya mzazi kwa mtoto,anafikiri bado anahitajika kumsaidia mwanae wa level ya Masters,tusimlaumu sana,mtoto kwa mzazi hakui..
 
Nenda Mamlaka ya Hali ya Hewa gorofa ya tatu Ubungo Plaza. Kitengo kinachohusika ni Customer care. Hapo utapata data zote unazotaka hata kama ni kuanzia mwaka 1896. wana Archive kubwa sana na data zao ziko vizuri. Pia watakupa ushauri mzuri kutokana na matumizi yako. Huwa kuna kulipia hivyo mwambie mwanao aende kwani kwa wanafunzi bei ni ndogo. Hakuna namna nyingine unaweza kupata hizo data bila kupewa na Mamlaka ya Hali Hewa (TMA)
Nashukuru sana ila mwanangu na mimi tupo nje. Prof. wake alifanya utafiti huo zamani hapa tz. Alimpa hiyo research akijua anatoka huku ila hakujua kutoka huko aliko kuja nyumbani ni gharama.
 
Pole sana. Wasiliana na Afisa wa kitengo cha Customer care. Namba yake ni 0754275571. Huyu atakushauri namna ya kulipia na kupata data zako bila kulazimika kuja TZ.
Ubarikiwe saana. Ngoja nimtafute. I hope ana whats up nilipo hawana mawasiliano na nchi yetu. Nitatafuta njia. Thanks a lot.
 
Nimeshamfahamu huyo mtoto wako, jana nilikuwa naye alikuwa anaulizia kitu hicho hicho. Nitamsaidia mkuu usijali ila na yeye atanisaidia in kind maana mzuri kweli kweli
 
Hayo ni mapenzi ya mzazi kwa mtoto,anafikiri bado anahitajika kumsaidia mwanae wa level ya Masters,tusimlaumu sana,mtoto kwa mzazi hakui..
Asante sana kwa kulielewa hilo. Ndo maana ya kuwa mzazi.
 
Back
Top Bottom