Natafuta data za mvua na joto ya kila mwezi kwenye mikoa ya Kagera, Dodoma, Tanga kuanzia 2006 mpaka 2016

Sasa jamani hebu tuwe wenye kutumia akili walau kidogo. Mtu anafanya research na hajui data za research zake atazipata wapi? Nina mashaka sana kama hata huo utafiti anafanya yeye kama siyo kufanyiwa! Hakujiandaa kufanya utafiti?
Huyu mtoto hakupenda kufanya huu utafiti ila prof. wake kamsahauri kama siyo kumlazimisha afanye huo maana anatoka Tz.
Mwanangu amechanganyikiwa inabidi aje Bongo wakati mimi nipo porini kwenye misitu halafu hana wa kumsaidia ndo maana nikaomba msaada ndugu.
 
Mwambie mwanao aende Mwanza ofisi za Bonde la Ziwa Victoria au kama yupo DAR aende Dodoma. Pale aende Idara ya Rasilimali za Maji.

Data zikikuwa Ubungo Maji ila wamehamia Dodoma.

Wana vituo baadhi ya mikoa ambayo wanakusanya data sio hourly tu. Ila hata baada ya kila dakika 5 kwa 24 hrs kwa mwaka mzima. Hizo data kama kituo kipo kigoma zilikuwa zinatumwa kila baada ya dak 12 kwenye server Ubungo Maji. Nakumbuka vituo vilikuwa 66 kwa kuanzia nchi nzima. Ni weather platforms za hali ya juu sana Wizara ya Maji kupata.. Vituo vinatumia solar na vilituma data vyenyewe. Baadhi ya data zilizotumwa ni mvua, max/min temp/vipimo kuhusu jua/ upepo/pressure/. Mashine zilikuwa configured kutuma kila baafa ya dak 12..

Kwa mfumo huo hawezi kupata data mpaka 2019 kwasababu uamuzi wa kuhamia Dodoma ulitibua mfumo wote, kulikuwa hakuna jinsi.

Kwani lazima atumie za Kagera. Angecheki wapi data zipo kwanza ndo angeenda msituni.

Data ni bure awaone wahusika. Aende na barua ya kuomba data aione Director Water Resources, aandike kifupi ni kwanini anataka hizo data.
M
Ukikwama mtafute nwenye post #9 inaekea anajua hii habari ya data

Anzia huko halafu aendaeTMA nako kuna changamoto kibao.

Kuna watu inaelekea hawako well informed Unakuta mtu anashangaa eti kwa nini mtu unauliza data JF.

JF kuna ma GURU wengi wako humu, na wapuuzi wanaouliza maswali kama hayo wapo pia wanaodhani wanajua kila kitu.inabidi wabebwe tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu asante sana nipo nje ya nchi na mimi ila nitajitahidi kutuma ndugu waende wamsaidie mwanao/mdogo wako kupata hizo data.

Tanzania tunakosa vitu vingi sababu watafiri wanapotaka kupata data zetu tunazibania. Mwanangu anafanya research na Italian Uni ambayo imefanya utafiti hapa miaka ya zamani. They wanted to compare and contrast. Mwanangu mwingine aliulizia kuhusu maswala ya Bio Chemistry alikuja kusaidiwa na watu wa Zimbabwe. Hapa nyumbani hatusaidiani ila tunataka tufaidi. Nashukuru saaana.
 
Wana jamvi, naomba msaada wenu kupata hizi data za joto na mvua kuanzia 2006 mpaka 2016. Sipo nyumbani ila mwanangu anafanya research yake ya masters na professor wake anataka afanye hiyo kwa masters yake. Nisaidie ndugu zangu ningekua nyumbani ningekwenda kwa wahusika ila nipo porini. Please help my son. You will never know anaweza tusaidia sote kwenye haya matatizo yetu. Please.

Natanguliza shukrani zenu kwa wale watakaokunwa na hili.
Hizo data kuzipata ni rahisi sana,cha msingi mhusika anatakiwa awe anaweza kutumia software ambazo ni free toka FAO. Software hizo ni

1.CLIMWAT is a climatic database to be used in combination with the computer program CROPWAT
2.CROPWAT 8.0 for Windows is a computer program for the calculation of crop water requirements and irrigation requirements based on soil, climate and crop data.

Cha msingi unatakiwa kufahamu coordinates na stations zilizipo Dodoma au popote pale unapotaka kukusanya hizo data
 
Sasa jamani hebu tuwe wenye kutumia akili walau kidogo. Mtu anafanya research na hajui data za research zake atazipata wapi? Nina mashaka sana kama hata huo utafiti anafanya yeye kama siyo kufanyiwa! Hakujiandaa kufanya utafiti?
Ndiyo yupo nje ila ana uchungu wa nchi ndo maana anafanya hivyo. Kama unapenda nchi yako msaidie.
 
Kumsadia nitamshauri ajaribu kupasha kichwa chake moto ili ajue data za aina hiyo atazipata wapi. Kutafuta data na kujua utazipate na wapi ni sehemu ya reseach! Yeye hakuwa na uwezo wa kuulizia kama ulivyofanya wewe? Mtu anaandika thesis ya masters kweli kweli bado analia ''mama mama nisaidie''?
 
Hizo data kuzipata ni rahisi sana,cha msingi mhusika anatakiwa awe anaweza kutumia software ambazo ni free toka FAO. Software hizo ni

1.CLIMWAT is a climatic database to be used in combination with the computer program CROPWAT
2.CROPWAT 8.0 for Windows is a computer program for the calculation of crop water requirements and irrigation requirements based on soil, climate and crop data.

Cha msingi unatakiwa kufahamu coordinates na stations zilizipo Dodoma au popote pale unapotaka kukusanya hizo data
Mkuu nipo naaza kufuailia nashukuru kwa ushauri. Nipe muda nitakupa feedback Mwanangu yupo italy na hii kapewa sababu wanajua yeye anatoka Bongo. Ameanza ku google nitakupa mrejesho. Thanks a lot.
 
Kumsadia nitamshauri ajaribu kupasha kichwa chake moto ili ajue data za aina hiyo atazipata wapi. Kutafuta data na kujua utazipate na wapi ni sehemu ya reseach! Yeye hakuwa na uwezo wa kuulizia kama ulivyofanya wewe? Mtu anaandika thesis ya masters kweli kweli bado analia ''mama mama nisaidie''?
You made my day. I wish he was a member to read this. Mimi ni mama na huyu mwenzio hakai nchini na mimi siko nchini ila aliona afanye utafiti kuhusu nchi yetu ili nasi tulikane. Nakaa bara tofauti na mwanangu na ananihitaji kumsaidia sababu yeye damu yake bado ipo Dodoma na kagera.
 
Huyu mtoto hakupenda kufanya huu utafiti ila prof. wake kamsahauri kama siyo kumlazimisha afanye huo maana anatoka Tz.
Mwanangu amechanganyikiwa inabidi aje Bongo wakati mimi nipo porini kwenye misitu halafu hana wa kumsaidia ndo maana nikaomba msaada ndugu.
Mwanao yuko nje (na assume kwenye nchi iliyoendelea ambapo Internet imetamalaki) anamlilia mama yake ambaye yuko porini amsaidie kuulizia mambo ya data kwenye internet! Mkuu usinione mimi mkorofi ila naona kama huyo mwanao siyo mtu wa kujituma au hataki kushughulisha kichwa chake. Hiki kizazi cha dotcom kweli anashindwa kuulizia mwenyewe kwenye forum kama hii? Ingekuwa mimi nisingemsaidia na ningemwambie afungue account JF (kama hana) aulizie mwenyewe! Usimwendekeze... ni kwa faida yake.
 
Unafanya research ya Tanzania na uko Italy huo tunauita mambo ya Kipu.mb.avu, anatakiwa aje Bongo na afuate taratibu za nchi katika ukusanyaji wa Data au ufanyaji research, ikiwemo kupata kibali.

Na sijui kama mwanao ni raia wa Tanzania kama siyo raia mwambie atafute na work permit
 
Naomba nikujibu bila hasira. Siyo huyu Tu hata mdogo wake 2017 nilienda naye milembe Dodoma kuomba afanye research na wagonjwa wenye matatizo ya akili, niliambiwa na mganga mkuu nimwone Waziri wa afya!
Hatukuishia hapo tukaenda miyuji sister aliyekubali mwanangu aende pale alihamishwa within a week. Ilibidi mwanangu aende Nairobi ndo alipewa nafasi. Huyu wa sasa kama kaka take asingekuwa na cheo kwenye kampuni Fulani asingepata research. Case study wanapewa kulingana na unakotoka. Hawapewi pesa za research hivyo kurudi nyumbani ni gharama. Wakija ndo mlolongo wa hapa na pale. Wangepata kwenye Google nisingekuja jf. Wanangu hawadeki Ila imefikia hawana jinsi.
 
Pole @Niah,sijui kwa nini vitu kama hivyo haviko easily accessible, anyway naona ataweka kwenye reflection kuwa Tanzania-Africa kuna ugumu kupata data inabidi mtu afanye vitu physically ambayo hata nayo kuna ugumu pia,And that's why his research is even important/worth sio contribution yake katika nchi yetu tu bali ku identify wapi kuna gap/upungufu and recommendations...
 
Am tongue tied. Siwezi sema zaidi. Ukienda nchi nyingi research wanakukaribisha vizuri hata unapewa na vivutio sababu wanataka watangazwe. Sisi kwetu ni kama wanakufaidisha hawajui research yako inaweza saidia nchi nzima.
 
Kwani tittle yake ya kwanza ilikuwaje mpaka huyo prof am-force? Angekuwa Tanzania pale SUA kuna Weather station pia wapo maprofesa wengi wa kilimo na hizo data zipo.

Masters sio mchezo sema huko mbele hawana shida SUA angepiga Masters 4years.
 
Wana jamvi, naomba msaada wenu kupata hizi data za joto na mvua kuanzia 2006 mpaka 2016. Sipo nyumbani ila mwanangu anafanya research yake ya masters na professor wake anataka afanye hiyo kwa masters yake. Nisaidie ndugu zangu ningekua nyumbani ningekwenda kwa wahusika ila nipo porini. Please help my son. You will never know anaweza tusaidia sote kwenye haya matatizo yetu. Please.

Natanguliza shukrani zenu kwa wale watakaokunwa na hili.
Bonyeza *149*01# chagua Yakwako tu kisha central zone,hapo utapata data za singida,dodoma,moro, na mikoa ya kati.

Bangi nayovuta ni mbaya
 
Mkuu natumia laptop na wifi halafu nipo nje ya nchi. Nawezaje kupata kwa njia nyingine?
 
Akya nani yani mabeberu wanaanza kuiba joto la nchi yetu uwiii Magufuli msaliti uyu hapa anasaidia mabeberu wameshindwa iba nadini sasa wanataka iba joto la nchi yetu .
 
Wana jamvi, naomba msaada wenu kupata hizi data za joto na mvua kuanzia 2006 mpaka 2016. Sipo nyumbani ila mwanangu anafanya research yake ya masters na professor wake anataka afanye hiyo kwa masters yake. Nisaidie ndugu zangu ningekua nyumbani ningekwenda kwa wahusika ila nipo porini. Please help my son. You will never know anaweza tusaidia sote kwenye haya matatizo yetu. Please.

Natanguliza shukrani zenu kwa wale watakaokunwa na hili.
Nenda Mamlaka ya Hali ya Hewa gorofa ya tatu Ubungo Plaza. Kitengo kinachohusika ni Customer care. Hapo utapata data zote unazotaka hata kama ni kuanzia mwaka 1896. wana Archive kubwa sana na data zao ziko vizuri. Pia watakupa ushauri mzuri kutokana na matumizi yako. Huwa kuna kulipia hivyo mwambie mwanao aende kwani kwa wanafunzi bei ni ndogo. Hakuna namna nyingine unaweza kupata hizo data bila kupewa na Mamlaka ya Hali Hewa (TMA)
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom