Mrejesho data za hali ya hewa Dodoma, Tanga na Kagera.

niah

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
7,010
9,259
Napenda kuwashukuru wote mliochangia kunisaidia kuhusu mwanangu kupata data za hali ya hewa ya Dodoma, Tanga na Kagera.

Mwendo haukuwa rahisi na ilibidi tupige hodi kwa majirani Uganda ambao wana data zote mtandaoni na wanaweza kuwasiliana na mhusika moja kwa moja. Mwanangu ameweza kufanikiwa kupata data za Uganda kulingana na kanda zake. Kule kwenye mvua nyingi na kwenye ukame na mvua za kadri. Hakuhitaji kulipa chochote na amemaliza kazi yake.

Nasikitika ila sitasema zaidi maana nchi yetu bado tuna mwendo. Nilieleza nilivyokataliwa wanangu kufanya research Milembe Hosp. wakaenda kufanya nchi nyingine tena kwa kupewa accomodation, mwingine ilibidi kaka yake aingileie kati sababu anawadhifa serikalini ndo akapata research tena kwa masharti magumu ambayo ilibidi barua zilitoka mpaka kwa mwenyekiti wa CCM wa kata!!

Nashukuru wote mlionipa ushauri na sana sana nashukuru wale waliosema namdekeza mwanangu. Mungejua watoto wanaosoma nje ya nchi wanavyopata shida kukubaliwa nyumbani mungenihurumia.
cc Ndege John asante kwa ushauri na wengine.
 
Pole sana mama kwa kuhangaika, tz yetu kwenye mambo ya research bado sana. Wanahisi ukifanya research yako utaenda kupublish uozo utakaoukuta.
 
ndo akapata research tena kwa masharti magumu ambayo ilibidi barua zilitoka mpaka kwa mwenyekiti wa CCM wa kata!!
Kwamba mwenyekiti wa CCM wa Kata alitakiwa kuandika barua ya kumtambulisha mwanao somewhere ili apatiwe nafasi ya kufanya research? Tanzania hii hii CCM na research wapi na wapi? Hii ngumu kumeza.
 
Kwamba mwenyekiti wa CCM wa Kata alitakiwa kuandika barua ya kumtambulisha mwanao somewhere ili apatiwe nafasi ya kufanya research? Tanzania hii hii CCM na research wapi na wapi? Hii ngumu kumeza.
Ndo uelewe. Mimi siweze sema uongo yalinitokea ila niliona basi nalipite maana mimi sina kadi yoyote ya chama na tangu niachane na TYL sijui siasa. Hii inanikumbusha tulivyokuwa tunaenda kupata barua za mwenyekiti wa ccm ili kujiunga na chuo enzi za 80s
 
Pole kwa changamoto lakini unachosema ni sahihi kwasababu mimi nilisoma nje ya nchi na wakat nafanya research nilitaabika sana kupata takwimu za kiwango cha mvua ya wastani kwa mwaka kwa mkoa tofauti kutoka TMA. Lakini Mungu ni mwema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibu Tena niah kwa swali lolote au uhitaji wa huduma kuhusu hizi field mbili hydrology na meteorology usisite kutushirikisha kwa msaada zaidi
 
Back
Top Bottom